Mwalimu wa Kike apigwa na Mwalimu Mkuu

Kwa nini MD hana taarifa? Fateni ngazi. Kuna ofisi ya malalamiko pia , kila halmashauri ipo ofisi hyo.
 
Bila shaka huyo ticha atahamishwa sababu kisaikolojia ameshaathirika, hawezi fanya kazi hapo tena. Na kwa huyo hasira, apigwe miaka yake saba.
 
Hawa walimu nao wanashangaza kweli,sasa Mwamakula hapo msaada wake ni upi kwa jambo la kijinai? Huyo mwalimu akaripoti polisi halafu aende kwa Mkurugenzi ambaye ndo mwajiri wao. Walimu kwa kweli hamjielewi ndo maana huwa mnanyanyasika.
 
Hongera kwa kujikomboa kutoka utumwani. Headmaster anayo mamlaka ya kumsimamia ufundishaji wa mwalimu wake darasani?
 
Hao Ni wapenwapenz Mkuu wa Shule Ni mkaguzi namba MOJA was Shule.

Taarifa ya Nini akupe?
Ili uandae Nini Cha ziada ambacho Kama asingekuja usingekiandaa?

Wewe ndo hujui ualimu ,

Nguo ndefu Ni SHERIA Siyo hiyari yako,

Halafu uvae nguo FUPI ili hao wanafunzi waone Tako LAKO au? Bora ulivyoandika ualimu.
 
Hao Ni wapenwapenzi,

Wala Siyo Mambo ya kazi,

Ama mwalimu wa kike alikuwa akimchunguza huyo mwalimu mkuu Kwenye KESI za mapenzi na hao watoto ,

Au mwalimu wa kike alimtusi mkuu wake akampandisha hasira akapigwa .

UCHUNGUZI ufanyike vzr
 
Sio effects za mahaba kweli hizi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732] mseleleko
 
Mbona hapo Hospitali ya Bunge Ni karibu kabisa na ofisi za CWT kwanini asiende yspo? Pia ungeweka picha ya Mwalimu aliyempiga
 
Ila walimu wameonesha hadhira kuwa weledi wao ni mdogo.Hawakupaswa kuripoti jambo hilo kwa Askofu Mwamakula bali walitakiwa waripoti ktk taasisi za umma kama Ofisi ya Mkurugenzi wa hiyo Halmashauri, Chama cha walimu Tanzania nk.
 
Natamani nikasomee uhakimu na kuhitimu muda huu huu halafu nifanye mpango ili nipangiwe kesi ya huyu mbabe Mwalimu Mkuu
 
Mussa Hasira akapimwe akili

Habari hii nayo ya upande mmoja sijui waandishi wa aina gani hawa!?

Au kampeni meneja wa mwamakula🤣🤣🤣
 
Sio effects za mahaba kweli hizi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732] mseleleko
Mambo ya wivu wa mapenzi yamemsababishia mwalimu Hasira kupata hasira.
 
Yaani hapo mwakee hasira bini jaziba [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hapo mwalimu Hasira utakuta hasira zimeongeza baada ya kutuma na yakutolea halafu akakukumbuka pia alikatwa na tozo daaaahhhh inauma sana kwa kweli.
 
Wameshariport polisi mkuu,, nadhani polisi na huyo mwalimu mkuu wana lao moja.
Mm ninavyojua ni kwamba Polisi wanazo taratibu za kushughulika na Tatizo kama hilo na sio kukurupuka kwani mpaka hapo tayari anayo makosa matatu:- 1. Kujeruhi 2. Kudhalilisha 3. Uvunjifu wa Amani mahali pa kazi - mengine yatajitokeza huko mbele ya safari.(Mkurugenzi (DED), anatakiwa awe ameshamsimamisha Kazi)
Inasikitisha pia mtoa uzi hajatuambia Mwl. Mkuu kwa sasa yuko wapi. Je, yupo kashikiliwa/kazuiliwa kituo cha Polisi au imekaaje ? Kwa ujumla mwl. HASIRA alichokifanya ni uovu na Amejichukulia Sheria mkononi mwake. Hii sio sawa. Kwa hali hiyo inatakiwa Sheria ichukue mkondo wake dhidi ya mwl. Hasira na Haki ionekane kutendeka i.e. Anastahili apumzishwe pale Mahabusu (Polisi) wakati taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…