babyfancy
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 2,176
- 6,187
Kaamua kuondoka na jino la bidadaHapo mwalimu Hasira utakuta hasira zimeongeza baada ya kutuma na yakutolea halafu akakukumbuka pia alikatwa na tozo daaaahhhh inauma sana kwa kweli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaamua kuondoka na jino la bidadaHapo mwalimu Hasira utakuta hasira zimeongeza baada ya kutuma na yakutolea halafu akakukumbuka pia alikatwa na tozo daaaahhhh inauma sana kwa kweli.
Hili halihitaji kusikiliza, hakuna sheria inayotoa uhalali wa kipigo kwa mtu mwingine.Kabla ya kuhukumu siku zote ni vema kusikiliza upande wa pili.
No matter the situation.
Hadi muda huu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini na Mkuu wa Wilaya hawana taarifa.
Mwalimu Witness Makoti ameomba asaidiwe katika kulipazia sauti jambo hili aweze kupata msaada kusudi haki iweze kutendeka lakini pia ili kuokoa maisha yake.
Mkuu Sheikh23; Hilo halijaharibu kitu. Amefanya vyema ili na ss huku maporini tuweze kuwa tumelijua na kama yupo mwengine (Mwl) anayefikiri au amezoea kufanya ujinga kama huyo Hasira awe amepata Fundisho ajihadhari na kujiepusha na ukorofi kama huo.😠👿Waende tume ya utumishi wa walimu,mamlaka yao ya utatuzi wa nigogoro wanaijua,kwenda kwa askofu ilipaswa kuwa baada ya ofisi za serikali kumaliza mgogoro,pia kumleta huku JF sio sawa
PGOKama ameshaenda polisi ilitakiwa polisi wafuatilie na wamkamate huyo mwl mkuu. Kwanini polisi hawajafanya kazi yao ,hiyo inaleta mashaka.
[emoji3]
Waache wapigwe tu mkuu, mzee Pinda alisema wapigwe tu, na mimi nakazia WAPIGWE TU, maana hawa ndio wanaolindaga kura za ccm na kuiba za upinzaniHuyu madam beautiful,kuna kitu hapa
MWALIMU WA KIKE APIGWA NA MWALIMU MKUU NA KUVUNJWA JINO MOROGORO VIJIJINI. WENZAKE WAMUOMBA ASKOFU MWAMAKULA ASAIDIE KUPAZA SAUTI ILI MAWAZIRI WENYE DHAMANA WASIKIE NA KUINGILIA KATI
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Tunapenda kukujulisha tukio la kusikitisha lililomkuta mwalimu mwenzetu aitwaye Witness Makoti wa Shule ya Msingi Mkuyuni iliyopo Tarafa ya Mkuyuni katika Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoani Morogoro.
Siku ya Ijumaa, tarehe 15 Oktoba 2021 muda wa Saa 6 mchana, Mwalimu Witness Makoti ambaye ni mwanamke alikuwa akiongea na wanafunzi watatu darasani. Wakati akiongea na watoto wake, ghafla alishambuliwa na kuanza kupigwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ambaye ni mwanaume aitwaye Mussa Hasira. Alipigwa sana lakini aliokolewa na mwalimu mmoja.
Baada ya kushambuliwa na kupigwa, Witness alikwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Mkuyuni na kupewa PF3 ya kwenda Zahanati ya Mkuyuni na kupata matibabu ya awali. Baada ya hali kuendelea kuwa mbaya, leo Jumapili alikwenda Hospitali ya Nunge kwa matibabu zaidi ambapo imegundulika kuwa Witness ana vidonda mdomoni na pia amevunjwa jino.
Hali yake ya kiafya mpaka sasa siyo nzuri sana na inazidi sana na ameleza pia kuwa pressure imempanda. Hadi muda huu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini na Mkuu wa Wilaya hawana taarifa.
Mwalimu Witness Makoti anahofia usalama wa maisha yake kwani ameelezwa kuwa Mwalimu Mkuu alimfuata mwalimu aliyemgombelezea Witness akaanza kumlaumu na kusema kuwa angelimuacha bila kumgombelezea ili amuue kabisa.
Mwalimu Witness Makoti ameomba asaidiwe katika kulipazia sauti jambo hili aweze kupata msaada kusudi haki iweze kutendeka lakini pia ili kuokoa maisha yake.
Tunaambatanisha picha ya Mwalimu Witness Makoti hapa chini.
Tunakushuru sana Baba Askofu Mwamakula kwa kutupokea na tunaamini kuwa kupitia sauti yako, Witness atapata msaada anaouhitaji.
Pole mkuu kama umekula nauli ya bwana Musa Hasira rudisha tu[emoji28]Jino limeng'oka mkuu
Kwani Umemnyima nini Musa!?Jino limeng'oka mkuu
mwanamke gani hawz kujitetea?? hawa tunaolewa nao kila siku?? wnye midomo kama chuchunge??uonevu wa kijinsia mimi mara nyingi nashangaa kwanini mwanaume rijali umpige mwanamke na unajua hawezi kujitetea, piganeni na wanaume wenzenu au naukuta tabia chafu sana hii na ya kukemea ni unyanyasaji wa jinsia,sheria ifate mkondo wake awajibishwe.
Hili halihitaji kusikiliza, hakuna sheria inayotoa uhalali wa kipigo kwa mtu mwingine.
Nimemwelewa rasjeff kapita kwamba wahusika wa pande zote mbili i.e. Mlalamikaji (Mwl. Witness aliyepigwa/jeruhiwa) na Mlalamikiwa (mwl. Mkuu aliyejeruhi) katika shauri hili wapate fursa ya kusikilizwa = wajieleze mbele ya sheria. Ni kweli Hakuna Sheria inayotoa Uhalali wa kipigo kwa mtu mwingine Lakini mkuu Renegade ujue kwamba inawezekana mtu akapigwa kihalali kutokana na matendo au kauli zake mwenyewe. Mathalani mtu anakutukana, anakufanyia mizengwe na unamuonya x 2 au 3 lakini hakusikii na anafikia hatua ya kukugusa/ kukushika/kukuundia genge la mizengwe ; Je, hutapandwa na hasira ya ghafla hususan unapomkuta Red hand? Ndo maana huyo rasjeff kasema wasikilizwe ili ibainike ni nini hasa kilichojiri/kisababishi.Hili halihitaji kusikiliza, hakuna sheria inayotoa uhalali wa kipigo kwa mtu mwingine.
Kanuni za asili zinasema kabla hujahukumu sikiliza pande zote......Hili halihitaji kusikiliza, hakuna sheria inayotoa uhalali wa kipigo kwa mtu mwingine.
Mkuu; Awe amemnyima au amemzungusha au kwa vyovyote vile iwavyo; bado hiyo Haimpi Musa Uhalali wa kumpiga mwl. WitnessKwani Umemnyima nini Musa!?
Hahahaa mwalimu mwingine ndiyo Huyo Witness mkuu.Pole kwa mwalimu Witness
Kumpiga mwenzio haikubaliki hata awe mke wa ndoa, vyovyote vile itakavyokuwa.
Lakini tuelezeni ikiwa mwalimu mkuu sio kichaa kwanini aliamua kumpiga Witness na sio kumpiga mwalimu mwingine?