Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Mnafiki! Unapinga adhabu ya viboko muda huo huo unataka kijana akafungwe unachimba chimo hili ili ufukie shimo lile
 
Kama watu ni rahisi kufundishika adhabu za kunyonga na viboko kwenye sheria zetu zimetungiwa nani?
Binadamu anafundishika,ingawa sio wote, na sheria zimetungwa kwa wale ambao wanavunja sheria
Mimi sijawahi kuwa na kosa lolote la kupelekwa mahakamani au hata polisi
Lakini hainifanyi kuwa siwezi kutenda kosa
Fimbo kuchapwa kila siku je huyo mtoto anabadilika? na je kama habadiliki utaendelea kupiga?
Nafikiri kuna wengine hawajali mafundisho bila fimbo

Ukipata mda angalia dog whisperer au dog behaving very bad
Utaona hao watu wanavyowabadili tabia za mbwa wakati wenye mbwa wameshindwa baada ya miaka
Ni mfano tu huo
Ila kwa watoto watukutu pia anaitwa Annie The Nanny akiwasaidia wazazi
Lakini pia kila mmoja anaona yuko sawa kwa anachofanya

Mtoto anadokoa nyama unamchoma mikono je una akili hapo?
 
Embu taja adhabu mbadala ambazo unaweza ukatoa kwa mtoto mtukutu
 
Embu taja adhabu mbadala ambazo unaweza ukatoa kwa mtoto mtukutu
Mkuu nimeona watoto watukutu wakipigwa sana lakini hawabadiliki, badala yake wanakuwa Nunda
Mimi sio muumini wa kufundisha kwa kupiga.
Sasa unaponiuliza hilo swali nimeishalijibu kwenye hoja iliyopita
Kuwa kila mmoja anamfundisha kwa njia anazoona yeye.
Hata wewe kama unaona ni sawa kupiga siwezi kukupangia
Mkuu kuna binadamu wabaya sana wanapopiga watoto wao au hujaona?

Kuna siku nimekaa sehemu, akapita mama mmoja akiwa na mtoto mdogo wa miaka miwili hivi
Mtoto kaamua kukaa chini kwa sababu ametoka kijijini na mama kachoka kumbeba
Akawa anampiga ili atembee.(Ni kosa)na sio suluhu hilo
Mama kachoka kumbeba mtoto, nikamuuliza umetoka nae wapi na unanda wapi
Akasema kijijini nampeleka hospital na nimechoka
Nikamuita na kuwapa maji na kuwakodishia pikipiki waende hospital

Nikamwambia najua umechoka kumbeba na yeye kachoka kutembea lakini mngepumzika kwanza
 
Akiwa Mwislamu ndiyo inakuwaje?

Ninyi mambo yenu ya kukataa hicho mnachokiita elimu dunia yanawafanya mwonekane nanii
Katika uislam hakuna elimu dunia wala elimu kuzimu, pili kwa hii tz kuna maprofesa wangapi ni waislam na wanaijua dini vizuri? Kuna shule ngapi za kiislam? Mnakaa mnazusha vitu kisha chuki tu.
 
Binafsi nimesoma madrsa na nimechapwa na sijawahi lalamika nyumbani kwa mzazi wangu, adhabu zitoke lakini kwa kiasi zinasaidia kuchangamsha mtoto, kwenye hiyo video ustaadh kazidisha adhabu.
 
Mimi ni muislam na nimeona hiyo video, ustaadh katoa adhabu kubwa kulinganisha na umri wa watoto, hao wa kike ilibidi fimbo moja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…