Embu taja adhabu mbadala ambazo unaweza ukatoa kwa mtoto mtukutu
Mkuu nimeona watoto watukutu wakipigwa sana lakini hawabadiliki, badala yake wanakuwa Nunda
Mimi sio muumini wa kufundisha kwa kupiga.
Sasa unaponiuliza hilo swali nimeishalijibu kwenye hoja iliyopita
Kuwa kila mmoja anamfundisha kwa njia anazoona yeye.
Hata wewe kama unaona ni sawa kupiga siwezi kukupangia
Mkuu kuna binadamu wabaya sana wanapopiga watoto wao au hujaona?
Kuna siku nimekaa sehemu, akapita mama mmoja akiwa na mtoto mdogo wa miaka miwili hivi
Mtoto kaamua kukaa chini kwa sababu ametoka kijijini na mama kachoka kumbeba
Akawa anampiga ili atembee.(Ni kosa)na sio suluhu hilo
Mama kachoka kumbeba mtoto, nikamuuliza umetoka nae wapi na unanda wapi
Akasema kijijini nampeleka hospital na nimechoka
Nikamuita na kuwapa maji na kuwakodishia pikipiki waende hospital
Nikamwambia najua umechoka kumbeba na yeye kachoka kutembea lakini mngepumzika kwanza