Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Na bila fimbo huwezi kariri
 
Nguvu inayotumika kupiga kubwa na fimbo size kubwa na panapopigwa changamoto

Swala sio idadi
Acheni mbwembwe unataka kusema huyo ustadhi ajui anachokifanya tukupe wewe fimbo uchape uone kama ni rahisi.

Hivi watz nani kawaloga mmejaa mihemko ndomaana mnaibiwa kila siku.
 
Nchi haiendeshwi kwa taratibu za dini yoyote.
Na hakuna dini yenye kibali cha kudhuru mtu kwa kigezo cha maandishi yake.
Aadhibiwe ili awe fundisho kwa wengine.
Mbona serikali yenyewe imeruhusu viboko mashuleni?
 
Nashangaa wanapowapa walimu maamuzi makubwa dhidi ya watoto wao.

Kwa mfano hao watoto wakiumia, mzazi atafurahi kuwa wamepata thawabu?
Wazazi wenyewe hata kuwalipa hao walimu ni mtihani walimu wengi wanawafundisha watoto dini kwa kujitolea tu
 
Kama hamtaki watoto wenu wagiswe muwe mnakaa nao nyumbani mnawafundisha , haiwezekani mtoto afanye makosa aangaliwe tu.
 
Hili ni tatizo la utumwa wa kifikra. Hatuwezi kuwa na watoro wasioweza kuadhibiwa.
Copral punishment ni lazima. Na kuchapa sio kuua mtoto
Nabii Suleimani a.w anasema
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Mithali 23:13
Utoro wa nini?
Kwani kuamini ni lazima?
 
Wazazi wenyewe hata kuwalipa hao walimu ni mtihani walimu wengi wanawafundisha watoto dini kwa kujitolea tu
Wanalipwa sifa kuitwa ma Ustaadhi mitaani wanajisikia raha sana kuliko kulipwa

Malipo sio lazima pesa kuna ma ustaadhi hawahitaji
 
Kwa hiyo mtoto achapwe shuleni, achapwe kwao na achapwe madrasa?
Wewe umekuzwa hivyo?
Serikali imeweka sheria mtoto akikosea ahadhibiwe bila kujali yuko sehemu gani.
Lamsingi miongozo ya adhabu kwa mujibu wa sheria ifuatwe kutokana na umri na afya ya muhusika.
 
Nchi haiendeshwi kwa taratibu za dini yoyote.
Na hakuna dini yenye kibali cha kudhuru mtu kwa kigezo cha maandishi yake.
Aadhibiwe ili awe fundisho kwa wengine.
Ndio maana mauliza zipo sheria za nchi yetu zilizovunjwa? Na zilipitishwa na bunge lipi.
Je serkali yetu haiheshimu dini na mila zetu zisizovunja katiba na miiko ya maadili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…