Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Nioneshe ni sehemu gani nimesema kila kosa mtoto apigwe?
Ww ndo ulie kosea unapo sema eti fimbo hazifai haijalishi mtoto kafanya kosa gani.
Mtoto kabla ya kumchapa una muonya na kuongea nae ukiona anapuuza na hasikii ndo hatua ya kumchapa itafuata ili kuonesha msisitizo wa unacho kiongea.
Binadamu hatufanani hivyo mototo wako ww kumuelekeza kitu akakusikiliza haimaanishi watoto wote wako hivyo.

Mm natoa mfano wa familia yetu tuko watoto 6 lakini tangu najitambua mpaka hapa nilipo sijui kiboko cha baba wala mama kinafananaje kwa sababu mimi utundu sio asili yangu.
Lakini wadogo zangu wote chamoto walikipata kutokana na tabia zao ,na mzee asinge shika fimbo kisawasawa wenda sasa hivi wangekuwa majambazi wana teka watu, na wakike wangekuwa kwenye madanguro wanajiuza sasa.
Lakini fimbo ya mzee ili warudisha kwenye mstaari ulio nyooka na mpaka sasa wengine wameolewa na wanakazi zao ,mwingine anamaliza chuo mwaka huu.
Na wenyewe huwa wanasema kabisa kuwa bila ukali wa baba tungekuwa watu wa ajabu na wanampenda sana.

Tuache kujipa umuhimu kwenye familia za watu kila mtu alee mtoto atakavyo ona inafaa ,haiwezekani mm nimuadhibu mtoto wangu ili arudi kwenye mstari mzuri unasema eti namfanyia ukatili.
Mtu akiniripot kwenye suala kama hilo nikitoka mahabusu atahama mji.
 
Mwafrika mbele ya imani za kigeni amekuwa mtu wa hovyo sana. Imani gani inaambatana na ukatili wa namna hii kwa watoto wadogo. Huyo usitazi anatakiwa kufugwa ili iwe fundisho kwa wengine ambao hata saikolojia ya kukaa na watoto hawaijuwi zaidi kutumia Jazba. Wazazi pia wanaopeleka watoto maeneo hayo waongeze umakani matukio ya aina hii ili yadhibitiwe.
 
Serikali imeweka sheria mtoto akikosea ahadhibiwe bila kujali yuko sehemu gani.
Lamsingi miongozo ya adhabu kwa mujibu wa sheria ifuatwe kutokana na umri na afya ya muhusika.
Sasa mbona unajitoa ufahamu?
Umri na adhabu vinavyoonekana hapo pichani vinaendana?
 
Kosa lake liko wapi hapo mbona ameshapa sehemu sahihi na hakuonyesha hisia za kutaka kudhuru ? UZUNGU UTATUHARIBU
 
Hakukua na fimbo ya kumuua mtoto hapo
 
Kama watu ni rahisi kufundishika adhabu za kunyonga na viboko kwenye sheria zetu zimetungiwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…