Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Acha nawewe ujinga. Mfano wa Serikali na kufungwa ni sawa na kosa la mtoto. Huko mahakamani kwenyewe kuna makosa ya vifungo vya nje, si kila kosa mtoto achapwe.

Ngoja nikufundishwe wewe, kuna mtoto alikuwa akichelewa shule kila siku. Anachapwa haswa, hakuna mwalimu aliyejitolea kukaa naye chini na kumhoji kwanini anachelewa ni mwendo wa viboko na adhabu za nje.

Mwalimu mpya aliyehamia hiyo shule, alikuwa na upendo sana. Aliamua kukaa na kila mtoto mwenye makosa ya kujirudia, huyu alimwambia anaishi na mama wa kambo na baba yake anaendesha magari makubwa, hayupo mara nyingi nyumbani.

Mtoto alisema anatakiwa afanye kazi zote za nyumbani, muda unakuwa unaenda akifika shule anachapwa. Ni mtoto ndiyo kaingia darasa la 5. Toka hapo wakajua tatizo lake, haya bila kuongea naye wangejua shida yake. Wakati mwingine shida si watoto ni wazazi na walezi. Wewe mtoto wako piga uwa ila jua ni mali ya Serikali.
Nioneshe ni sehemu gani nimesema kila kosa mtoto apigwe?
Ww ndo ulie kosea unapo sema eti fimbo hazifai haijalishi mtoto kafanya kosa gani.
Mtoto kabla ya kumchapa una muonya na kuongea nae ukiona anapuuza na hasikii ndo hatua ya kumchapa itafuata ili kuonesha msisitizo wa unacho kiongea.
Binadamu hatufanani hivyo mototo wako ww kumuelekeza kitu akakusikiliza haimaanishi watoto wote wako hivyo.

Mm natoa mfano wa familia yetu tuko watoto 6 lakini tangu najitambua mpaka hapa nilipo sijui kiboko cha baba wala mama kinafananaje kwa sababu mimi utundu sio asili yangu.
Lakini wadogo zangu wote chamoto walikipata kutokana na tabia zao ,na mzee asinge shika fimbo kisawasawa wenda sasa hivi wangekuwa majambazi wana teka watu, na wakike wangekuwa kwenye madanguro wanajiuza sasa.
Lakini fimbo ya mzee ili warudisha kwenye mstaari ulio nyooka na mpaka sasa wengine wameolewa na wanakazi zao ,mwingine anamaliza chuo mwaka huu.
Na wenyewe huwa wanasema kabisa kuwa bila ukali wa baba tungekuwa watu wa ajabu na wanampenda sana.

Tuache kujipa umuhimu kwenye familia za watu kila mtu alee mtoto atakavyo ona inafaa ,haiwezekani mm nimuadhibu mtoto wangu ili arudi kwenye mstari mzuri unasema eti namfanyia ukatili.
Mtu akiniripot kwenye suala kama hilo nikitoka mahabusu atahama mji.
 
Mwafrika mbele ya imani za kigeni amekuwa mtu wa hovyo sana. Imani gani inaambatana na ukatili wa namna hii kwa watoto wadogo. Huyo usitazi anatakiwa kufugwa ili iwe fundisho kwa wengine ambao hata saikolojia ya kukaa na watoto hawaijuwi zaidi kutumia Jazba. Wazazi pia wanaopeleka watoto maeneo hayo waongeze umakani matukio ya aina hii ili yadhibitiwe.
 
Serikali imeweka sheria mtoto akikosea ahadhibiwe bila kujali yuko sehemu gani.
Lamsingi miongozo ya adhabu kwa mujibu wa sheria ifuatwe kutokana na umri na afya ya muhusika.
Sasa mbona unajitoa ufahamu?
Umri na adhabu vinavyoonekana hapo pichani vinaendana?
 
Kosa lake liko wapi hapo mbona ameshapa sehemu sahihi na hakuonyesha hisia za kutaka kudhuru ? UZUNGU UTATUHARIBU
 
Mnaomtetea huyo mwalimu wa madrasa, je kama ndiyo tabia yake huwachapa kila mara? Watu wamemchoka ndiyo sababu wakamrekodi mtajuaje?

Kijana wa miaka 24, ila hana huruma na mtoto mdogo wa kike analia, anaendelea kumchapa na hapo mwishoni kamchapa mwilini. Huo ni ukatili, mtoto/watoto wakikosea njia si kupiga ongea nao na kuwakataza Mabaya.

Hivi mtoto mmoja angekuwa mgonjwa na alipochapwa hapo akanyooka mngesema hayo? Tujaribu kuongea na watoto zaidi ya kuwachapa. Mtoto wangu sijawahi mchapa, ila anasifiwa kila anapokuwepo kuwa ana nidhamu sana analelewa vizuri kinidhamu. Nimemuweka karibu, kirafiki na kuongea naye zaidi.
Hakukua na fimbo ya kumuua mtoto hapo
 
Mimi hata nikimuona mtu anamchapa Punda wake huwa namuonya na kumwambia huyu ndio anakufanya uende chooni na wanao kama unao, halafu unampiga akiwa kabeba mzigo mzito.
Kweli fimbo sio sababu ya kufundisha na sioni sababu zozote za kupiga
Wanangu siwachapi na wana nidhamu sana kwa sababu nawafundisha

Hawaibi wala kutukana na shuleni wako vizuri pia, wakija nyumbani wanajua wajibu wao, homework kwanza, mengine yanafuata

Kuna watu wanafikiri kupiga ni nidhamu ila utakuta wauwaji wengi ukiwahoji makuzi yao watakuambia tulikuwa tunapigwa mpaka mangumi ya kichwani

Kama wanafuatilia hivyo basi mashule wanapiga mpaka mtoto anakufa
Kama watu ni rahisi kufundishika adhabu za kunyonga na viboko kwenye sheria zetu zimetungiwa nani?
 
Back
Top Bottom