Shule ya msingi KIMANDAFU iko wilaya ya Arumeru Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha. Mwalimu tajwa hapo juu ni mwl mkuu msaidizi na mwl wa Hisabati darasa la 5, siku ya Alhamisi saa 2 asubuhi amlimfukuza mwanafunzi wa darasa la 5 aitwaye Angel Frank Mbise darasani ktk kipindi chake cha somo la Hisabati kwa kumwambia "Sikutaki ktk kipindi changu ondoka utoke nje" mtoto kweli aliondoka na kurudi nyumbani, mamake kuona mtoto amerudi nyumbani mapema isivyo kawaida alimhoji mwanaye kilichomsibu.
Kesho yake siku ya jana Ijumaa mama aliambatana na mwanawe shuleni kujua sababu ya mtoto wake kufukuzwa na kurudishwa nyumbani, huyu mwl katili aitwaye Gunda alimnyima mtoto nafasi ya kujieleza badala yake alimsingizia uwongo kwamba mtoto alitoroka shule na kupewa tena adhabu.
Baada ya hapo mama aliondoka kurudi nyumbani, baada tu ya mama kuondoka alimfukuza tena na kuamuru asingie kipindi chochote, mtoto alishinda nje akilia siku nzima.
Naomba serikali imsaidie huyu mtoto na kumwadabisha mwalimu husika, huyu mwalimu hakuna wa kumfanya kitu pale shuleni mwalimu mkuu ni Mmasai mwenzake ni mambo ya ukabila na ukatili shuleni. Mtu mzima km huyu mwl kumnyanyasa mtoto mdogo wa miaka 10 ni roho ya uchawi maana malengo ya uchawi ni kuharibu, kutesa na kuua. Yuko kutesa, kuharibu na kuwaua watoto wetu kielelimu na kuua future yao.
Huyu mwl ana kiburi, dharau na roho mbaya ya ubaguzi shuleni anaweza kumkosesha mwanafunzi makusudi hata km amepatia majibu sahihi ktk Hisabati au anaweza kukata tu kazi ya mwanafunzi asiisahihishe maana anajua hakuna wa kumwuliza.
Hana maadili ya utumishi wa umma. Hebu serikali isiruhusu mtumishi wa umma kukaa sehemu moja kwa muda mrefu wanajisahau hasa wakileta kujuana na kulindana kwa misingi km hii ya ukabila.