DOKEZO Mwalimu wa S/M Kimandafu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru amfukuza darasani mwanafunzi wa darasa la 5 siku 2 mfululizo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Malalamiko haya ni ya upande moja,hatujasikia upande wa pili unasemaje ili kuijadili kwa usahihi.
Kwa kiasi kikubwa malalamiko yako mtoa mada yamechanganya malalamiko na majungu ndani yake.

Adhabu ya kusimamishwa masomo inaendana na kosa alilofanya mwanafunzi baada ya kupitia hatua mbali mbali.

Nina maswali mengi ya kujiuliza,lakini niishie kwa kufikiri wewe unashida binafsi na huyo mwalimu.
 
Hili jambo linaonekana ni dogo na la kawaida sana. Ila wewe umeamua kulikuza na kulitolea maamuzi kabisa.

Kama Mwalimu Mkuu wa hiyo shule ni Mmasai mwenzake na unahisi hakuna wa kumfanya kitu huyo Mwalimu Gunda, kwa nini usiende kwa Afisa Elimu Kata? Au na yeye ni Mmasai?


Hayo maelezo mengine yanaonesha una chuki zisizo na msingi dhidi ya huyo mwalimu. Kama umeona ana makosa, fuata huo utaratibu wa kumuona Afisa elimu kata badala ya kuja kutoa shutuma na malalamiko ambayo ungeweza kuyamaliza huko huko shuleni.
 
Acha majungu mzee na kwa maelezo haya huyo mtoto ni mtoto wako tabia zenu zinafanana
 
Hoja yako ya msingi , lakini umechanganya na MAJUNGU.
Angedai haki ya mtoto kuliko kupenyeza tuhuma za Mwalimu zisizo na ushahidi.
Any way. Ujumbe umefika na nahisi mpaka amefikia hapa Ina maana mwl huyo kweli ni mbabe haswa.
 
Mwl mkuu wa shule hiyo na huyo mmsai mwenzake ni washirikina sana wameloga Halmashauri yote kawafanya maafisa taaluma na Elimu madondocha yake. Kuna walimu km Ulotu wanafika shuleni mara 2 tu kwa wiki hawezi ht kuwakaripia, mwl mkuu gani anachukia watoto wadogo wa shule ya msingi tena vitoto vya siku hizi vilivyo vidogo. Mwanafunzi anashinda nje akilia na yeye ni kiongozi? Ana mzungu wake fulani tapeli anaitwa madam Birgita siku anaenda shuleni wanafunzi huchangishwa sh elfu mbili mbili ndipo wapikiwe ugali maharagwe siku hiyo viboko vyote vitafichwa kumwonesha mzungu kuwa hawawachapi watoto, mnafiki mkubwa aliyevaa ngozi ya kondoo. Siku nyingine zote wanafunzi wanalishwa makukuru km nguruwe wakati shule yenye wanafunzi wengi wanaofikia hata 1500 mahindi hukobolewa na kulishwa makande. Mwl mkuu gani anatetea walimu badala ya vile vitoto vya shule ya msingi? Mwalimu anahitaji kutetewa na mwl mkuu? Serikali kuu au ya mkoa ichunguze hiyo shule maana halmashauri inashirikiana na hao wahuni kunyanyasa watoto wetu
 
Wewe utakua mwl katili
 
Utamfukuzaje mtoto asisome? Walimu wengine wana mashaka sana. Tunaomb wachangiaji msiingize udini ktk hii mada
Huwezi kuanza kuhukumu kwa kusikiliza maelezo ambayo ndani yake yanasura ya majungu , mambo ya shuleni ni mengi sana usipo kuwa na utimamu wa akili utalaumu sana ila ukifika shukeni ukasikiliza kisa vizuri unaweza kuoata maelezo tofauti kabisa na kilicho letwa hapa, tujifunze kuchunja na kutanua fikra zetu
Wewe utakua mwl katili
Acha ushoga kwanza maana unaonekana kabisa umetepeta ndio maana huelewi mada
 
Hawa walimu wapoo connected na majin kama sio mapepo.....

Nimeona taarifa moja juzi mwl kamwondoa mwanafunzi wiki 2 kisa simu

Na alieleta simu katajwa kakiri kafukuzwa

Sasa kama umejua mwenye shida wengije unafukuza wa nn...wakaenda kulalamika kwa mkuu wilaya nahisi jama kama hayuko manyara wamemtupa katavi

Alipewa amri afike kwa boss wake kwa ajili ya uhamisho
 
Wewe wakukimbilia kuita watu mashoga ndo uwe na utu!!!
 
Wewe wakukimbilia kuita watu mashoga ndo uwe na utu!!!
Sasa kama mtu hawezi kuchambua jambo kwa mapana na kichwa anacho sasa unaweza kuhisi nini kipo kichwani mwake kama sio ushoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…