Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Mwalimu kufukuzwa.jpg


Pia soma ~
Huyu ni mwalimu wa shule gani anayempiga mwanafunzi mateke​
 
View attachment 3477280
Baada ya video ya yule mwalimu mwenye stress zake akionekana anampiga mwanafunzi mateke na mangumi ametimuliwa kazini, aingia mtaani akapigane na maisha maana nguvu anazo kupiga wanafunzi


Pia soma >> Huyu ni mwalimu wa shule gani anayempiga mwanafunzi mateke
Kaonewa huyo Esta kashinikizwa huyo dogo ana tabia za Abdul, wenzie mboni wamekubari kunyooshwaa na wakatii yeye analeta adabu gani hivi hawa vinyago ndio wanapelekwa jeshini kwenda kula kula tu baada ya kumaliza six wakirudi wamenenepa mpaka unajiuliza huyu alienda jeshini kweli huyu?
 
Kumtetea huyu mtu ni ngumu kwa sababu ya huo uvaaji wake. Ila angepewa tu onyo kali. Kumfukuza kazi sio poa.
Kwanini yeye hakutoa hilo onyo kali kwa hao wanafunzi na badala yake akawa ana walamba tu mitama?

Huyo hata angepewa onyo kali asingebadilika coz anaonekana kua hiyo ni tabia yake,
sana sana angekuja kudhuru tu watoto wa watu,hafai kua mwalimu.
 
Hongera sana serikali kwa kuchukua hatua kwa uharaka sana ,ningepende msiishie kumfukuza tu kazi inabidi CPA itumike maana kuna jinai hapo afikishwe ka PILATO apate haki ya kikatiba.

Walimu kama hawa ndiyo wanaoua wanafunzi kwa vipigo ,pia inatakiwa mtembeze waraka tena kwa shule zote kukomesha kupigwa kwa wanafunzi ,kuna adhabu za kutoa kwa wanafunzi wenye makosa ,kama kufagia ,kulima bustani ,kupiga deki ofisi etc na si kumpiga kwa viboko ,mwingine anaweza kupata mstuko wa kupigwa akazima ukapata "MADAKESI".
 
Mkuu tumsamehe mwalimu kwa sababu watoto wengine washenzi mno. Kufukuzwa inatosha.
Mtoto mshenzi atafunzwa na ulimwengu ,kuna hatua za kuchukua kwa watoto washenzi ,moja wapo ni kumuita mzazi wake ili amkananye mwanae ,akiendelea ni kumfukuza shule.

mwalimu mwenyewe jinsi alivyovaa inaonyesha ni MUHUNI MUHUNI wa kitaa .anavaa suruali utafikiri KISHANDU au TATU MZUKA.
 
Walimu wanaofundisha wanafunzi wa shule za Kata kote nchini wanapitia majaribu mengi sana. Na hii ni kutokana na utovu wa nidhamu uliopitiliza, unaowahusu hao watoto walio wengi.
 
Usimnyime mtoto fimbo..

Dogo alianza na kumdindia mwalimu.

Mwalimu naye kama binadamu alishikwa na ghadhabu.

Sema haya mambo yasikie kwa mwenzio tu, kama haujawahi kufundisha wanafunzi huwezi kuelewa..
Mkuu,huyo Mwalimu yeye akaamua kutomnyima mtoto mateke na mitama!
 
Back
Top Bottom