Mafunzo ya Udereva
JF-Expert Member
- Aug 27, 2025
- 620
- 925
Kanuni zenyewe ndiyo hizo, mkichapa fimbo mnakutana na watukutu, wanagoma au wanawatunishia misuli, mwisho wa siku mnapandwa na hasira, mnaadhibu kinyume na hizo kanuni, mnajikuta matatizoni na kudharauliwa!
Kuepuka hayo yooote,Fanya kazi ya kufundiaha, kwa weledi, atakayeelewa well and good atakayepuuza ulichofundisha muache akafundishwe na wazazi wake, full stop!
Uzuri, wakipata zero ndo wanaowatetea wanaanza kuhangaika nao, wakati wewe kuendelea kufundisha wengine.
Huoni kuwa ni salama zaidi ukiacha kuchapa kuliko kukomalia kunyoosha maadili ya mtoto ambaye wazazi wake, jamii inayokuzunguka na hata wenye mamlaka hawaoni kama ni muhimu?
Kama tungekuwa na akili, tungetumia nguvu zetu zote kutambua watoto wakorofi kwenye kila shule, na kuwalazimisha kuelewa na kutii maadili ya taifa, (elewa NENO KUWALAZIMISHA)
Then wale wenye utii, wanakuwa motivated na kuwashauri pale wanapokosea (kwani kibinadamu,kokosea ni kawaida)
Lakini kwa kuwa tumeamua kuporomosha maadili ya taifa na kuutukuza usasa, tusubiri matokeo yake!
Shule Kama hii bila viboko haiendi