Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Ningekuwa mzazi wa huyo dogo, mwalimu tungemalizana binafsi na ingekuwa fundisho kwa walimu wengine
 
akipata usaidizi kisheria hiyo kesi anashinda na kurudi kazini

miaka ya 78s nakumbuka kuna mtumishi alifukuzwa kazi kwa kosa la uso wa kilevi na waziri mkuu kumbe bana wala sio mnywaji mtumishi yule alirudi kazini
Mahakama tofauti..Hii uwenda alizivuka kanuni za adhabu.
Uwenda mwalimu ndio tabia yake..
Baadhi ya wanafunzi ni viburi sana....
 
Pamoja na kuwa kuna wanafunzi jeuri ila walimu wengi wa kiume rika hilo wanakuaga jau sana hasa kwa wanafunzi wa kiume. Akikuadhibu mbele la vibinti atataka either ulie utoe machozi au umnyenyekee ndio akuache.
Hivi viwalimu havinaga kabisa akili, misifa imejaa, wivu pia akiona unapendwa na madem ana kutengenezea beef. Ukipatikana na kosa ukapelekwa ofisini na mwalimu wa kike jua kiama chako kimefika, atapiga kama anaua anaconda. Shenzy kabisa walimu aina hii.
 
Pamoja na yote ila kuna kizazi tunakitengeneza majibu tutakuja kuyaona sio mbali sana. Wamarekani na watu wa Ulaya sasa hivi wanajuta sana kwa mfumo wao wa malezi kwa namna ulivyokuwa na matokeo waliyonayo leo hii, muda utasema
 
Hao wadada wanaorekodi video nao vilaza tu, eti haoni uchungu kwa sababu hajazaa.
 
Smartphone zingekuwepo miaka ya 90 nadhani 80% ya waalimu wangu wa Primary wangefukuzwa kazi. Hata sekondari pia kuna waalimu wangu wangeenda jela.
 
Naona watu wanapongeza sana, bila kujua upande wa pili, huyo dogo alitamka nini.Mwalimu naye angejitahidi ku-control hasira.
Walimu:
Achananeni na watoto wa watu: msiwe na kiherehere nao, aje amechelewa, hajaingia darasani, hasomi, kafail, fanya mambo yako & go home..subiri mshahara wako.
Siku ukijisahau uka-loose control ndo utaelewa hii dunia ilivyo.
 
Mwalimu mwenyewe kavaa kwa utovu wa nidhamu
Huyo dogo atakuwa ni mwalimu wa kujitolea. Na ndiyo maana shule ndiyo iliyo mfukuza. Angekuwa ni mwalimu wa ajira ya kudumu, basi ni lazima angekuwa ana msongo mkubwa wa mawazo.
 
Mahakama tofauti..Hii uwenda alizivuka kanuni za adhabu.
Uwenda mwalimu ndio tabia yake..
Baadhi ya wanafunzi ni viburi sana....
ukitizama picha mjongeo mwanafunzi alileta kibri hata alivyo kataa ile ng'wara nilishindwa kuelewa mafunzo hayo kayapata wapi... hili hawezi lifanya kwenye shule kama makongo
 
Hakuna mwalim mkuu anaweza kumfukuzisha Mwalimu kazi, mwalim mkuu sio Mwajiri. Labda huyo Mwalimu alikuwa anajitolea hapo...
 
shule zina kanuni,moja wapo ni adhabu za viboko,zifutwe tujiachie na watoto/wadogo zetu kwa raha zetu.
Kanuni zenyewe ndiyo hizo, mkichapa fimbo mnakutana na watukutu, wanagoma au wanawatunishia misuli, mwisho wa siku mnapandwa na hasira, mnaadhibu kinyume na hizo kanuni, mnajikuta matatizoni na kudharauliwa!

Kuepuka hayo yooote,Fanya kazi ya kufundiaha, kwa weledi, atakayeelewa well and good atakayepuuza ulichofundisha muache akafundishwe na wazazi wake, full stop!

Uzuri, wakipata zero ndo wanaowatetea wanaanza kuhangaika nao, wakati wewe kuendelea kufundisha wengine.

Huoni kuwa ni salama zaidi ukiacha kuchapa kuliko kukomalia kunyoosha maadili ya mtoto ambaye wazazi wake, jamii inayokuzunguka na hata wenye mamlaka hawaoni kama ni muhimu?

Kama tungekuwa na akili, tungetumia nguvu zetu zote kutambua watoto wakorofi kwenye kila shule, na kuwalazimisha kuelewa na kutii maadili ya taifa, (elewa NENO KUWALAZIMISHA)

Then wale wenye utii, wanakuwa motivated na kuwashauri pale wanapokosea (kwani kibinadamu,kokosea ni kawaida)

Lakini kwa kuwa tumeamua kuporomosha maadili ya taifa na kuutukuza usasa, tusubiri matokeo yake!
 
Back
Top Bottom