Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Barua ina ukakasi.

1. TAMISEMI IPO chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu?

2. Mtumishi (Mwalimu) hafukuzwi kazi bali anasimamishwa kwanza, uchunguzi unafanyika kisha Hukumu.

Sasa kama umeangalia video vizuri, unataka uchunguzi gani?
 
Kosa halilingani na adhabu hakustahili kufukuzwa, Walim acheni kupiga hivyo vitoto viendelee kulelewa kimayai mayai viishie kwenye uteja, we kula mshahara wako tulia .
 
Adhabu ya kufukuzwa tu haitoshi inatakiwa sasa hivi angekuwa nyuma ya nondo.
Huyu chizi stress zake za maisha anahamishia kwa watoto wa watu.
Tunaelewa watoto wa sasa hivi ni watukutu ila kuna namna ya kutoa adhabu kila mwalimu angekuwa anafanya upumbavu huo kusinge kuwa na shule bali uwanja wa vita.
 
Mambo yanabadilika, miaka yetu mwanafunzi ukifanya hivi wewe ndio unatimuliwa na imetokea sana.

Mitandao nayo inasaidi kuweka mambo sawa.
 
Sina uhakika na hiyo barua,
Hakuna mtumishi.wa umma anafukuzwa kazi kizembe hivyo aisee.
 
Pamoja na kufukuzwa kazi, ningekuwa mimi ni mzazi wa huyo mtoto ningempandisha kizimbani na ushahidi upo mtandaoni
 
Safi sana Bora alivyofukuzwa kazi
Mwalimu Mkuu hana mamlaka ya kumfukuza mtumishi wa kudumu kazi. Kuna ngazi na hatua mbalimbali za kufuatwa.

Bila shaka huyu ni wa kujitolea ama mkataba. Hapo ndio Mwalimu Mkuu anakuwa na mamlaka kamili ya huyo mtumishi.
 
Walimu mkae mkijua serikali haipo upande wenu . Haya matoto ya sasa ni mabroira dawa yao ni kuachana nayo.Fundisha sepa.

Halafu walimu wanachukiana sana vituoni kwahiyo wengine wanakurekodi makusudi ili kukukomoa .

Fundisha tu akuelewe asikuelewe wewe sepa fanya majukumu mengine.
 
Barua ina ukakasi.

1. TAMISEMI IPO chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu?

2. Mtumishi (Mwalimu) hafukuzwi kazi bali anasimamishwa kwanza, uchunguzi unafanyika kisha Hukumu.
Yule ni mwalimu wa kujitolea tu, mwajiri wake ni Mwalimu mkuu na kamati ya wazazi, amevuna alichostahili hawa wakifumbiwa macho ndio wauaji wa wanafunzi mashuleni.
 
Back
Top Bottom