Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Makumbusho (Dar) afukuzwa kwa kosa la kutoa adhabu kali kwa Mwanafunzi

Barua ina ukakasi.

1. TAMISEMI IPO chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu?

2. Mtumishi (Mwalimu) hafukuzwi kazi bali anasimamishwa kwanza, uchunguzi unafanyika kisha Hukumu.
Kwani huyo alikuwa mtumishi au substitute?
 
Dah sjui kizazi iki kinaenda wapi...enzi tunasoma haya mambo ulikuwa kawaida sana
 
Nitawatetea walimu siku moja.

mimi sio mwalimu kitaaluma, ila angalau nimejishkiza kama patron shule fulani baada ya kuona kitaa hakieleweki. Mimi kama Patron ninapitia madudu huyo mwalimu nadhani hajawahi ona. ninafahamu anachopitia huyo ticha.

Kuna wanafunzi wanakera mpaka unatamani yani daaaaaaah.....acheni tu.
 
Nitawatetea walimu siku moja.

mimi sio mwalimu kitaaluma, ila angalau nimejishkiza kama patron shule fulani baada ya kuona kitaa hakieleweki. Mimi kama Patron ninapitia madudu huyo mwalimu nadhani hajawahi ona. ninafahamu anachopitia huyo ticha.

Kuna wanafunzi wanakera mpaka unatamani yani daaaaaaah.....acheni tu.
Tafuta mume oelewe
 
Sasa hilo lina tatizo gani? Lipi bora kuwaadhibu hawa wanafunzi washenzi wa tabia na maadili au kuwaacha kisa kufuraisha hizo taasisi za haki feki ili baadae hawa wanafunzi waje kuwa TAKATAKA?, watoto wa leo wadhaifu sana, ADHABU ndogo wanalalamika kama nini, na usishangae hata waliorecord wanahusika ktk ukatili wa watoto huko majumbani, hasa kwa mabinti wa kazi.

Failure state
 
Kwa haya ya kumhharibia mtu wako fasta sana.
Ikija kwenye suala la uhamisho au kumpandisha mtu cheo ndio utajua rangi zao.
We're hardwired to do evil things than good things, ni nature Iko ivyo ni rahisi kuchukia kuliko kupenda.kizuri kina kazi Kina maumivu Ila kibaya ndio kinakuja haraka chenyewe
 
Kaonewa huyo Esta kashinikizwa huyo dogo ana tabia za Abdul, wenzie mboni wamekubari kunyooshwaa na wakatii yeye analeta adabu gani hivi hawa vinyago ndio wanapelekwa jeshini kwenda kula kula tu baada ya kumaliza six wakirudi wamenenepa mpaka unajiuliza huyu alienda jeshini kweli huyu?
Sasa ndio umpige teke kisa kakataa viboko kuongezwa? kama amekataa adhabu unamripoti kwa mkuu sio kurusha makofi na mateke.
 
Usimnyime mtoto fimbo..

Dogo alianza na kumdindia mwalimu.

Mwalimu naye kama binadamu alishikwa na ghadhabu.

Sema haya mambo yasikie kwa mwenzio tu, kama haujawahi kufundisha wanafunzi huwezi kuelewa..
Kama mtoto hataki mfukuze shule au mpe suspension sio kurusha mateke.

Hiki kisingizio cha " hasira za kibinadamu" ndio unasikia oooh mtu kakata mtu mapanga kisa kaiba parachichi!!

Mwalimu afunguliwe kesi ya madai iwe fundisho
 
Jamii zilizokuletea hayo maneno usimnyime mtoto fimbo wao hawachapi watoto wao
jamii zipi hizo???

wanaonyima watoto wao fimbo ni wale ambao hawaamini ktk hayo maandiko,na wanaamini katika uhuru mpaka wa mtoto kuchagua jinsia.

wacha tuwaige maana ndio ujanja,halafu 2040 tutakuwa mbali kuwazidi.
 
Kwani umeenda kunyoosha watoto ama kuwafundisha maarifa, unahangaika kumchapa mtt wa mtu kazi Gani, ita mzazi wake aje amchape mbele ya parade basi, aelezwe kosa lake ,ivi hamuwezi kufundisha bila ya viboko, ukiwa unatoa maarifa huyu anaongea mtoe ama watoe nje wakaongee wakimaliza warudi darasani , mbona simple sana.
You're just complicating life just within yourself or in your own head , nimekutana na walimu hawatumij fimbo bana na wanakubalika, yaani ujue unapochapa mtt ama kutukana ina Mana akili yako imeishia hapo so una entertain emotions.
Muandikishe hata barua , huku mwalimu akisema zikifika Tano unafukuzwa shule.1
ukishindwa au ukapuuza kumchapa mtoto jeuri atakugomea hata kutoka darasani,aone utamfanya nini.

hawa watoto bila mkono wa chuma shuleni,mnawaandalia lawama za bure polisi miaka 2 mbele.
 
Kosa la kwanza ni kutoa adhabu bila kufuata utaratibu. Kosa la pili ni kuwa mwalimu. Mahakimu wanasigina sheria, polisi wanaua raia huwezi sikia filimbi nyingi namna hii. Tumepigwa upofu?.
 
Back
Top Bottom