Kwani ukifanya simple chemical reaction ya acid+ base---- salt +water
Si tayari naharibu acid kwenye vyakula hivyo na kula chakula kikiwa salama?[emoji16][emoji16]
Coz swala la kuacha mtindi litaluwa ni gum
Unajua wanasema mtego upo kwenye namna watu wanatafuta maarifa na kuyatumia. Huyu anaetoa elimu yupo sahihi kwa upande m'moja ila statement ya kusema usitumie ni statement ambayo inatumika vibaya sana.
Kuna ule usemi kuwa kila kitu hapa Duniani kina hasara na faida. Ukikitumia vibaya kinakuletea madhara ukikitumia vema kinafaida.
Bangi inatumika kama antidepressants na matumizi mengine kwenye medical field ila bangi hiyo hiyo si nzuri kuizoea kwa matumizi ya starehe za ujana.
Gari ni chombo cha usafiri chenye faida kede kede ila matumizi ambayo si sahihi ya gari yanaweza kusababishia madhara wewe na wengine na kupelekea hata kifo.
So hata hizi vyakula watu wengi hawana elimu ya kutosha kujua namna ya mwili unahitaji nini kwa wakati upi wanatumia kwa kiasi cha kupitiliza hadi inawaletea madhara kimwili na kuwapa shida za afya.
Mfano Beer unatakiwa utumie kwa kiwango kidogo per serving. Yaani umeenda zako pub unakunywa chupa zako 4 au tano. Sasa mtu anaenda anataka anywe kreti nzima pekee yake. Huo mwili unapata virutubisho gani hapo sasa kwa hiyo excessive drinking?
Au mtu mwili unaona kabisa umekuwa kibonge ila bado unakula burgers, chips yai, beer, vyakula vya kunenepesha, halafu unategemea mwili uwe salama?
Watanzania wengi ukiwaambia kula vyakula kwa style ya mzunguko yaani balanced diet wanaona kama unawapa story za kusadikika. Wakianza kuumwa magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, pressure, kiharusi, matatizo ya macho, Gauti, etc utaona wanavyohangaika kula miti shamba na kujifanya wanajua sasa kufata utaratibu wa lishe bora Pumbavu kabisa.
Ndio maana kuna msemo unasema, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Leo humu mitandaoni kuna kila aina ya elimu juu ya afya ila nenda jioni pita humo kwenye viwanja vya starehe tazama watu na ulaji wanaofanya, nenda kaulize wanaouza mafaka wakwambie watu wanasema maneno gani juu ya unga wa dona, utasikia wanasema hauna ladha, jambo ambalo si kweli, kati ya dona na unga wa sembe ni upi ambao hauna ladha?
So wanasema kiburi cha mwanadamu ndicho kitakachomuangamiza ila sio MUNGU wala shetani. Wenye kusikia watasikia na kujirekebisha wale viburi ndio watateketea.
LET THE GAME BEGIN.