Mwamba alietunyoosha huyu hapa

Mwamba alietunyoosha huyu hapa

Jamaa akamuomba sista watoke, sista akakubali halafu tukaenda wote., Siku nyingine ananiita mie tuanenda wote vile vile....ndio tulivokuaga yani NIITE TUJE, Pale mezani jamaa anakunywa kwa aibu tu glass haishuki anajichekesha chekesha akasema dah sawa bwana tukamuuliza sawa nini hana majibu anacheka tu tukaagiza....kula kunywa na kusaza.

Mimi namuita shemeji sista nae anamuita shemeji, akaona mambo hayawezekani tena akaachana na mapenzi ikawa urafiki tu akaswma wakati namfata mdogo ako niliona ananisumbua we umetulia, nimekufata wewe naona unasumbua mdogo ako katulia ndio tukaanza wote kumuita shemeji 😁....kila jpili tunatoka wote kwakweli alijua kutupa good time tulikua tunazunguka tu ni kula na kunywa, urafiki ulikolea akawa anakuja hadi home anatuijia na anaturudisha....

Dada angu alikua anampango wa kuanza kujitegemea, mwamba akamnunulia godoro, na vitu vidogo vidogo...tukitoka out akinunua kitu tunanunuliwa wote
Kimbembe kikaanzia hapa sasa....🙄 Dada alipata boyfriend ambae wakawa serious anakuja kumtambulisha home, mi sijui alimpiga sound gani yule sponsor wetu akaleta kreti mbili za beer, kuku wawili akampa na hela wakati hajui kuna nini kumbe ni maandalizi mchumba anakuja kumtambulishwa halafu siku hiyo tukakataa kutoka......sijui nani alikuja kumpenyezea kwamba ilikua utambulisho 🤣🤣🤣

Siku hiyo natoka school jioni kama saa kumi hivi, nakuta pale home taharuki watu wamejaa kucheki hivi namuona sponsor huyu hapa jicho jekundu mamaeeeehhh sijawahi kumuona vile napita ndani nakuta sista katepeta hafai 🤣🤣🤣 mama kakunja sura yani vurugu sista akaniambia jamaa kaja kudai vitu vyake vyote...kaja na jamaa mwingine mpambe wake sponsor kasimama kwa mbali anapaza sauti "lete godoro" hilooooo tukalibeba tukatoa nje mpambe wake akapokea "lete chaja ya simu" "lete ile nguo nilikushonea" sista akaitoa sponsor akairarua pale akaitupa pembeni mara "letee chupi zile" tobaaaaaaaa hiyo chupi ndio nipo nimeivaa 🤣🤣🤣 nikapata kijasho mama akasema hamuwezi kumpa nguo za ndani hapana.

Kichwani sista kasuka weaving jamaa ndio alitoa hela "leteee hilo wigi" uwiii akakaa chini huku natetemeka namfumua nywele tukampa sista akabaki na twende kilioni zake 😁 akasogea karibu yetu lete zile hereni za silva sista hataki kutoa anasema zimepotea kubishana bishana akajishika nyuma ya kiuno tulikimbia.....heeeee yani hereni tu ndio atutolee mguu wa kuku 😔 akaona tushajificha yule jamaa ndio kuondoka....ila watu wamejaa yani aibu noma kilo kumi.

Akatuacha na maswali what's next, bi mkubwa alitufokea mno, ikabidi sista aende polisi kutoa taarifa jamaa akaitwa akapigwa beat pale na maafande wa kike na kumchamba juu we unadai vitu kwa mwanamke ye mapenzi alokupa utalipa 🤣🤣 Kumbe masikini hata upaja hajawahi kushika

Tukachuniana baada ya mwezi akatufata tena jamani samahani kwa yote twendeni mahali tukatoe tofauti zetu....tukakataa huu ndio ulikuaga mwisho hatukurudia tulikoma yani.
 
Back
Top Bottom