kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Sisi mashabiki hatujui ukubwa wa tatizo lilisababisha Kapteni wa Yanga, Mwamnyeto kushindwa kwenda Rwanda kwenye mechi muhimu saaaaana kwa timu ya Yanga dhidi ya Al-Merreikh. Kama mchezaji kiongozi wa timu mechi hii haikuwa ya kukosa kwasababu hafifu hafifu tu na dhaifu.
Vitu pekee ambavyo vingeweza kusababisha kapteni wa timu kuikosa mechi ya muhimu kama ile ingekuwa labda kuumwa sana kwa mchezaji, mazishi ya mzazi, mke, au mtoto wako aliyefariki wakati wa maandalizi ya mechi na mpango wa kocha kwenye mechi husika, zaidi ya hapo mchezaji professional hatakiwi kukosa mechi muhimu kama ile kwasababu ndogondogo na fupifupi (trivial). Ni heri asicheze uwanjani lakini awepo kwenye benchi kwaajili ya kuwatia hamasa wachezaji wenzake.
Kukosekana kwa Kapteni wa timu kwenye mechi kunaongeza morali kwa timu pinzani na kupunguza morali kwa wachezaji wa timu yake, benchi la ufundi, uongozi na hata mashabiki wa timu, sio jambo ambalo kocha makini atalifurahia hata kidogo. Anaweza kukuchukia milele kwakuwa huaminiki (not reliable and dependable).
Hii inawezekana ni sababu kwa kocha Gamondi kutomjumuisha kwenye kikosi cha kilichocheza marudiano na Al-Merreikh pale chamazi. Wachezaji wazawa lazima muwe real professionals.