Mwamnyeto kuzikosa mechi muhimu sana za Al-Merreikh ni fundisho kwake na wazawa

Mwamnyeto kuzikosa mechi muhimu sana za Al-Merreikh ni fundisho kwake na wazawa

Huo ndio uswahili wenyewe kwa wachezaji wazawa. Baba akiwa mgonjwa sehemu yake sahihi ni hospitali na wajibu wa mchezaji kama Mwamnyeto ni kumkatia bima ya matibabu wazazi wake. Kwahiyo yeye alikwenda kufanya nini kwa baba yake? Je, kama mwamnyeto angekuwa anacheza mpira timu za Ulaya angerudi Tanga kumjulia hali baba yake mgonjwa kama alivyofanya? Akumbuke kuwa kocha wa Yanga sio Charles Mkwasa ambae anazifahamu mila na desturi zetu.
Acha fikra za kijinga aisee, hujui alikuwa na umuhim gani kwa wakat huo.. ni sahihi alichokifanya kuna watu familia zao ndo kila kitu kwao yuko tayari kwa kila kitu ilimradi familia yake iwe salama.. we unaona kitu kidog ila kwake nikikubwa saana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yeye ni daktari? alisaidia nini baba yake kupona? Kocha ni mzungu, na ana mipango yake. Klabu haiwezi kukosa kwenda makundi baada ya miaka 25 ya kusubiri kwasababu eti wewe baba yako ni mgonjwa tu hajafa.
Hili kumbe box,
Ndo shida za smartphone za mikopo.. sa zubaa kwenye jf usipate ela yakulipia leo wakuzimie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACHA utani,mwaka 2016 Kalidou Koulibaly mke wake alikua yupo labor anatakiwa kujifungua,siku hiyo wana game na sassuolo akamwambia Coach Sarri ampe ruhusa akamuangalie mke wake anajifungua mtoto wao wa Kwanza..Sarri akamgomea katakata na kweli hajaenda,na hakupangwa dk zote 90 bench....so hisia na kua professional vitu viwili tofauti niffah
Mifano ya hivyo ni mingi sana. Objective aliyopewa kocha Gamondi na benchi lake la ufundi ni kuipeleka Yanga makundi la sivyo kibarua chake hakitaeleweka. Mchezaji muhimu sana (Kapteni) siku ya mwisho ya maandalizi ya mechi mchezaji anamwambia kocha wake kuwa hatakwenda kucheza kwakuwa baba yake hajisikii vizuri, habari kama hiyo LAZIMA itamchanganganya kila mdau lakini sanasana kocha ambae anajua umuhimu wa Bakari kundini. Amerudi na kufikia kwenye mbao ndefu ya kocha hadi aseme.
 
Acha fikra za kijinga aisee, hujui alikuwa na umuhim gani kwa wakat huo.. ni sahihi alichokifanya kuna watu familia zao ndo kila kitu kwao yuko tayari kwa kila kitu ilimradi familia yake iwe salama.. we unaona kitu kidog ila kwake nikikubwa saana..

Sent using Jamii Forums mobile app
sawa, lakini watu makini wanaofanya scouting ya wachezaji kwa weledi kwenda kucheza timu kubwa huko nje hawezi kumchukua mchezaji mwenye sifa kama hii. Ataendelea kuwa local player hadi azeeke.
 
Umeandika uzi ukafanya na conclusion kabisa bila kujua sababu za mchezaji kusafiri na timu(ajabu hii[emoji144])
Then comment iliyofuata ukapewa ufafanuzi,na uongozi ulikuwa na option mbili aidha wakatae au wamruhusu.Nadhani waliona maelezo yake yana mashiko,wakamruhusu(ukaona kumbe ulikurupuka).... kwahiyo kuanzia utengenezaji wako wa hoja ulishafeli ila utaki kukubali unajiona mwamba mwenyewe kwa kuwakejeli watoa comments kisa wako against na wewe(kioja kingine),unakua fala km kina GENTAMYCIME
 
yeye ni daktari? alisaidia nini baba yake kupona? Kocha ni mzungu, na ana mipango yake. Klabu haiwezi kukosa kwenda makundi baada ya miaka 25 ya kusubiri kwasababu eti wewe baba yako ni mgonjwa tu hajafa.
Kocha ni mzungu!
pdx Schizophrenia
 
Kaka uswahili ndio kisiki kikubwa cha wachezaji wazawa kubakia hapo walipo. ni bahati nzuri Yanga ina kikozi kipana, uzembe huu wa mwamnyeto umetoa nafasi kwa mchezaji mwingine kuaminiwa na kocha. Wewe unadhani Mohamed Husein Zimbwe jr. wa Simba yeye hauguliwi, hafiwi, haumii? Bro, malengo ya mwajili yanakaa mbele ya malengo ya mwajiliwa. Kama baba anaumwa na yuko hospitali tayari nitakwenda kumjulia hali nikirudi Rwanda kwenye maokoto kwanza. Kama baba yange angekuwa amefariki ingekuwa jambo lingine kabisa, no one angeweza kusikitika wala ku-mind. Gamondi aliendelea kumuweka nje ili amalizane na uswahili wake kwanza. Nimemsikia Gamondi akisema angetaka asajili wachezaji wengine kwaajili ya makundi na hatua nyingine, huenda kitendo cha mwamnyeto kilimshtua kwelikweli,
Hivi kifo na kuuguza kipi Bora? Nyinyi ndio Aina ya watu mgonjwa anaumwa utoi chochote Ila alifariki mnatoa michango mikubwa ya kujionyesha.
 
Umeandika uzi ukafanya na conclusion kabisa bila kujua sababu za mchezaji kusafiri na timu(ajabu hii[emoji144])
Then comment iliyofuata ukapewa ufafanuzi,na uongozi ulikuwa na option mbili aidha wakatae au wamruhusu.Nadhani waliona maelezo yake yana mashiko,wakamruhusu(ukaona kumbe ulikurupuka).... kwahiyo kuanzia utengenezaji wako wa hoja ulishafeli ila utaki kukubali unajiona mwamba mwenyewe kwa kuwakejeli watoa comments kisa wako against na wewe(kioja kingine),unakua fala km kina GENTAMYCIME
AAAh!!! Kocha ni mzungu, atakuwa ameshangazwa kusikia mchezaji amechagua kwenda kumtakia hali baba yake over kucheza mechi ya al-merreikh rwanda, baada ya kushangaa hakuwa na chakufanya zaidi ya kukubaliana nae kwakuwa kocha anafahamu kuwa mipra unachezwa mguuni na kichwani kwa pamoja. Alijua hata kama akienda nae kule hatamwamini kucheza na ku focus kwa 100% kwakuwa mchezaji tayari alishaonyesha kuwa akili ya mchezaji itakuwa nyumbani zaidi kuliko uwanjani. Ni heri aondoke na ameondoka na hakumpanga tena hadi timu imeingia makundi. Kila mchezaji duniani anatamani kucheza mechi kama zile zinazowauza kwenye timu kubwa, hivyo hakuna mchezaji mwenye upeo atafanya kitu kitakachomkosesha kucheza mechi za kimataifa kama zile.
 
Hivi kifo na kuuguza kipi Bora? Nyinyi ndio Aina ya watu mgonjwa anaumwa utoi chochote Ila alifariki mnatoa michango mikubwa ya kujionyesha.
Aaaah! Mchezaji professional anatumia akili badala ya moyo kufikiri, Mwamnyeto alitumia moyo wake kufikiria na kutenda. Bakari ni mdigo, kwao ni Tanga mjini ilipo hospitli ya mkoa ya Bombo hospital ambako baba yake angeweza kupelekwa kupata matibabu, lakini ziko hospitali zingine nzuri kama Hindu Mandal, Burhan, na nyingine nyingi ambazo angeweza kutuma pesa (delegate) matibabu ya mzazi wakati yeye anafanikisha kazi ya kuipeleka makundi timu yake kwanza, hata kama asingecheza lakini kuwepo tu kwenye kikosi ingekuwa muhimu kwa wachezaji wenzake kama kapteni. Uswahili tu kaka.
 
Niuswahili tu ila haikua lazima kuacha mechi kwakua tayar mzee yupo hospital nandugu wengine wapo...
 
Familia inayomsumbua mzungu ni ile ya mke/mume na mtoto wake, baba na mama kuna watu wengi kama mkewe, kaka, dada, wajukuu, shangazi wanaweza kwendaga huko wakati mimi ninakamilisha taratibu nyingine. Sanasana naweza kuwatumia fedha ya ambulance na matumizi/matibabu wakati mimi nikimalizia shughuli muhimu, yaani nitaungana na nyinyi baadae. hata wanafunzi vyuoni na mashuleni wakati wa mitihani huwa wanafichwa kuambiwa matukio mabaya yanayotokea nyumbani kama ugonjwa au kifo cha mwanafamilia hadi atakapomaliza mitihini yake yote, sembuse mechi ya kufuzu makundi na wewe ndiye kapteni wa timu. Uswahili tu bhana.
Nakuelewa mkuu, kuna jamaa yetu alifiwa na Mama yake kipindi tunafanya mitihani ya form Six, ilinidi afichwe japo alihisi kama Kuna kitu anafichwa. Alipomaliza mitihani ndo akaambiwa
 
Niuswahili tu ila haikua lazima kuacha mechi kwakua tayar mzee yupo hospital nandugu wengine wapo...
Ameshindwa kutofautisha kati ya mechi ya ligi na mechi ya mabingwa wa Afrika. Kama inhelikuwa mechi ya kawaida ya ligi (sio derby) isingekuwa issue sana. Kama mzazi angekuwa amefariki ingekuwa pia issue nyingine
 
Hivi unajua sababu ya yeye kutokwenda Rwanda? Mbona Klabu walitoa taarifa rasmi kuwa anauguliwa na baba yake?
Wewe unaweza kumuacha baba yako mahututi ukaenda kuitumikia klabu?
Titi camara mchezaji wa zamani wa liverpool alipewa taarifa za kifo cha babake mzazi masaa matatu kabla ya mechi na alicheza

Obi mikel akiwa chelsea baba yake alitekwa nyumbani nigeria lakini bingwa alicheza mechi na akakichafua vibaya

Hio ni mifano michache nilyokupa tena yenye sababu nzito nzito ijekuwa ya mzazi kuumwa?

Kwa mwamnyeto ndio amekuwa daktari kwamba alivyobaki ndio mzee wake akapata nafuu?

Ifikie kipindi waxhezaji wetu wajifunze kuwa professional excuse ndogo ndogo km za mzee kuumwa waachane nazo.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hivi unajua sababu ya yeye kutokwenda Rwanda? Mbona Klabu walitoa taarifa rasmi kuwa anauguliwa na baba yake?
Wewe unaweza kumuacha baba yako mahututi ukaenda kuitumikia klabu?
Hata ningekuwa mimi nisingemuacha mzazi wangu
 
Acha fikra za kijinga aisee, hujui alikuwa na umuhim gani kwa wakat huo.. ni sahihi alichokifanya kuna watu familia zao ndo kila kitu kwao yuko tayari kwa kila kitu ilimradi familia yake iwe salama.. we unaona kitu kidog ila kwake nikikubwa saana..

Sent using Jamii Forums mobile app
Local boys, pumbavu!! Kumbe ndio nyinyi mnaosababisha vijana wetu hawaendi kucheza nje ili wabaki kuwavalisha wazazi wao pampas. Kama Mzee Samantha angeugua huko mbagala rangi 3 Mbwana Samata angekuja kutoka Genk kumvisha pampas? Unaongea uharo wako.
 
Unaujua ukubwa wa familia yake? Unajua anasumbuliwa na maradhi gani? Bima ya afya inakupeleka na kukupangia foleni kwa dakitari?
Hapa naona unazungumza kama mlivyoishi huko ulaya ambako baba yako akifariki unakwenda kumzika tu kwa muda uliopangiwa na weilazi(walizi wa kukodiwa) na ukimaliza unarudi ofisini.
Swali la masingi

Mwamnyeto ni doctor?

Kwamba kubaki kwake nchini ndio mzee wake ndio akapata nafuu au?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Titi camara mchezaji wa zamani wa liverpool alipewa taarifa za kifo cha babake mzazi masaa matatu kabla ya mechi na alicheza

Obi mikel akiwa chelsea baba yake alitekwa nyumbani nigeria lakini bingwa alicheza mechi na akakichafua vibaya

Hio ni mifano michache nilyokupa tena yenye sababu nzito nzito ijekuwa ya mzazi kuumwa?

Kwa mwamnyeto ndio amekuwa daktari kwamba alivyobaki ndio mzee wake akapata nafuu?

Ifikie kipindi waxhezaji wetu wajifunze kuwa professional excuse ndogo ndogo km za mzee kuumwa waachane nazo.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Unajua kilicho kua nyuma ya story ya Baba yake Mikael Obi?
 
Nakuelewa mkuu, kuna jamaa yetu alifiwa na Mama yake kipindi tunafanya mitihani ya form Six, ilinidi afichwe japo alihisi kama Kuna kitu anafichwa. Alipomaliza mitihani ndo akaambiwa
Mtoto mdogo kama huyo kafichwa ili atimize jukumu muhimu, sembuse mechi ya kufuzu makundi. Angekuwa mm ningemvua kitambaa Cha ukapteni wa timu
 
Back
Top Bottom