Mwamposa Buldoza anazo nguvu za kweli

Na kuna wengine wanaona hizo ni sanaa na ndio maana wametoa hoja zao kuwa kama ni kweli basi akajaribu kuifanya hiyo miujiza ICU pale Muhimbili
 
Na kuna wengine wanaona hizo ni sanaa na ndio maana wametoa hoja zao kuwa kama ni kweli basi akajaribu kuifanya hiyo miujiza ICU pale Muhimbili
Hoja ya kwenda kufanya hiyo miujiza hospitali ni hoja nzuri hata mimi naunga mkono maana jinsi wanavyotutangazia na kutaka kutuaminisha hiyo miujiza basi ilitakiwa tuone wakienda huko hospitali na kuwaponyesha wagonjwa kwa hiyo miujiza maana watu wa dini huwa wanaendaga hospiali kuwatembelea wagonjwa na kuwapa zawadi mbalimbali hivyo inawezekana kutumia nafasi hiyo kuwaombea na kuona miujiza ya wagonjwa kupona.

Lakini pia pamoja na hayo hoja ya kuwepo Mungu na kuwepo uchawi ipo pale pale.
 
Mpaka waende hospitali maana yake hukubaliani na masimulizi ya watu

Kama hukubaliani tafsiri yake ni kuwa hayo mambo hayana uhalisia
 
Na kuna wengine wanaona hizo ni sanaa na ndio maana wametoa hoja zao kuwa kama ni kweli basi akajaribu kuifanya hiyo miujiza ICU pale Muhimbili
Sorry sijajua wewe ni wa imani gani, ila nitaongea kwa mujibu wa imani ya ki Kristo ukimuangalia Yesu alivyo kuwa akitenda kwa asilimia zaidi ya 98% ya miujiza yake alikuwa hamfuati mtu na kumtendea muujiza bali alikuwa zake mitaani busy kueahubiria watu jinsi wanavyo kombolewa, kuponywa na kuokolewa kutoka kwenye mateso na vifungo vya nguvu za giza, yaani anafundisha na kuwajaza wale watu matumaini na imani hadi mtu mwenye shida anaamini kuwa daah kumbe uponyaji ni jambo la wazi na jepesi namna hii, basi anamfuata Yesu na kuomba atendewe ndipo utendaji unafanyika. Na mara kadha wa kadha alikua akinukuliwa akitamka maneno haya IMANI YAKO IMEKUPONYA.

Hii inakuambia kwamba, nguvu ambayo ilikuwa inatumika kumfanya mtu apone ni kutoka ndani ya mtu yule yule bali Yesu alikuwa anafanya kama kuiboost maana watu wengi hata leo hii wanahisi kana kwamba muujiza ni jambo gumu kweli kweli kutokea na linatokea mara chache sana, lakini kumbe sivyo, kwahiyo Yesu alicho fanya ni kama kuwabadilisha watu mtazamo wao na kuwaambia jambo lile walilokua wana liona gumu sana kuwa ni jepesi mnoooo, basi mtu asikiaye habari hizi anazipokea na kuziamini, mbona chapu tu anapokea uponyaji, yaani hata kama alikuwa kiwete miguu imelegea kabisa, anakuja Yesu anamuambia "ndugu yangu hii miguu yako ni mizima kabisa wala haipo kama vile unavyo hisi, hivyo simama utembee, kiwete yule akiona ni Yesu aliye muambia neno lile ana lipokea na kuamini alafu anasimama papo hapo bila kuchelewa, unakuta huyoo anaenda watu wanabakinm midomo wazi.

Labda nikuambie kwa mfano huu ambao hata mimi nimeutumia mara kadhaa na umetenda kazi, ipo hivii, ukiamini haiweezekani basi hamna namna hicho kitu kita wezekana na ukiamini kuwa ina wezekana na uka focus, hakika itawezekana.

Watu huwa tuna waamini sana wataalamu (wasomi) kuwa wao wanajua vitu vingi hivyo ukipewa ushauri na msomi au mtu aliye fanikiwa katika angle fulani huwa tunaupokea haraka na kuuamini ule ushauri kuliko ushauri wa mtu mwingine tu.

Mfano wewe una umwa homa alafu ukaenda kwa daktari alafu dk hata bila kukupima akakwambia hauna homa yeyote ile rudi tu nyumbani kula vizuri, fanya mazoezi na upumzike kwa wakati utapona. Nawewe utaupokea ule ushauri kwa imani kwamba kama dct kasema hivi basi ni kweli, utaenda nyumbani na baada ya mda utajikuta kweli umepona.

Na kwa upande mwingine dct akikupa maneno ya kutisha hatakama ulikuwa na kijihoma kidogo utajikuta homa inazidi kupanda kwa kasi hadi unazidiwa.......

Sasa nachotaka kusema ni hiki, wahenga waliposema mwenye shida amfuate mganga walikua na maana kubwa sana, maana ile tu kitendo cha kutoka kwenda kwa fulani ni kwamba una imani ya uhakika kwamba nikienda pale nita saidiwa, kwaiyo kilicho kufanya usaidiwe ni ile imani yako kwamba nikienda kwa fulani nitasaidiwa.

Kitendo cha mchungaji kwenda kumponya mgonjwa hospital hakitawezekana kama mgonjwa mwenyewe hajaamini kuwa nikiombewa nitapona. Kinacho mpasa mchungaji akifika hospital awafundishe wale watu kwa upole na utaratibu mkubwa jinsi mambo ya uponyaji yanavyo tendeka, jinsi watu wanavyo weza kupokea uponyaji kisha wale watu watao amini ndio wao wenyewe watake kwamba mtumishi niwekee mkono uniombee nipone.

Sio mchungaji atoke alikotoka na kuanza kuombea kila mtu, huo ni upuuzi na ni matumizi mabaya ya nguvu za Mungu.

ANYWAYS MAMBO YA IMANI YANA MTU NA MTU, NI NGUMU SANA KWAMBA WATU WOTE TUTAKAA NA KUKUBALIANA KITU KIMOJA HIVYO, HUWA NAPENDA PIA KILA MTU ASIMAME NA LILE ANALO LIONA NI JEMA NA SAHIHI KWAKE YEYE.

Nina mengi ya kusema kuhusu hili ila kuandika kunachosha kwa yeyote anaetaka ufahamu zaidi juu ya hili anitafute kwa 0620181872
 
WAJINGA NDIO WALIWAO[emoji1784]
Washaangamia wamekosa maarifa.
 
Siamini katika imani ya dini
 
Tatzo upunguani wa akili ndio unawasumbua hata hilo wanashinndwa kujiuliza!
 
Wajanja waliowah mjini wamegundua watu wanashida nying sana wanahitaj uvumbuz wa matatzo yao kuliko kumhitaj Yesu na wakaamua kuja na huduma fake ili kujizolea Swadaka za bure.
Watu hawahitaj kwenda mbinguni wala kuyajua maandiko wao wanahitaj mseleleko imewapasa wapigwe kisawasawa.
 
Unajiponya mwenyewe, You are the master of your Life/destiny.

Sculptor of your own sculpture, You have a chisel(Mind) use it to sculpt your self.

Sculpting is the act it should be learned , Sculpting yourself Never ends ,It is a continual process, moment to moment, day to day, .

🫂
 
Mpaka waende hospitali maana yake hukubaliani na masimulizi ya watu

Kama hukubaliani tafsiri yake ni kuwa hayo mambo hayana uhalisia
Mbona nimefafanua vizuri tu mkuu kwamba msimamo wangu ni kwamba hutumika uchawi na uongo pia.
 
 
Kuna nyakati unaweza sema mungu yupo nawe kumbe upo na setani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…