Digaller
JF-Expert Member
- Oct 20, 2009
- 883
- 828
Habari,
Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ile video ya Mtume na Nabii Boniface Mwamposa akitoa ushuhuda na dokezo kuhusu kuingia chumba cha marubani na kumuuliza rubani kwanini ndege haitembei kwa speed.
Video ilienda viral kwa sababu y maelezo yake na mazingira yake ukiwa ndani ya ndege na jinsi ya kumfikia rubani wewe abiria kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani kwa hali ya kawaida.
Kabla hili halijakaa sawa naona limeibuka lingine huko mwanza nadhani la kuponya viwete. Ukiangalia yale magongo ambayo anadai walikuwa wanatumia viwete ni almost yote ni mapya, hayajawahi kutumika au kama yametumika basi ni mara moja tu, hii inaleta ukakasi kwenye kuamini maneno yake na ushuhudu wake.
Je ni end of an era au watu wake wa karibu wameshamchoka na wameanza kumuumbua? Maisha ya imani huwa na ups and down, nadhani kama kuna kitu anafanya makosa kwa sasa basi ni kuamini ataendelea kuwalisha ujinga waumini wake kwa muda wote.
As kiongozi wa dini anapaswa sana kuchunga ndimi yake, kauli zake na vitendo vyake anvyofanya katika jamii, Mimbari ni sehemu patakatifu, si sahihi kutoa maneno yanayoacha dalili za uongo hata mara moja.
Na kwa sisi waamini, As a bible says "Mtafute sana elimu, usimwache aende zake" basi yatubidi kutafuta ukweli kwa yale yatupasayo, kuendelea kulishwa uongo ni kukosa hekima na maarifa, Mwenyezi Mungu ametuumba kuwa na uwezo wa kufikiri, kuhoji na kufanya tafakari ya yale tuyaonayo, tuyasikiayo na tuambiayo.
Kama lengo la kufanya ibada ni kumfikia mwenyezi Mungu basi kumbuka nabii mwongo hawezi kukufikisha kwenye hilo lengo lako, Kamwe kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.
Kwa sisi watafuta miujiza, tuaomini ulonzi na wafuta mafanikio, Je kwa Mtume Boniface Mwamposa, ni End of an era au aliteleza tu?
NB: Usihukumu, kwa maana usije kuhukumiwa, ila usiache kukemea uovu, kwakuwa muovu siku zote ni ibilisi.