Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 4,039
- 2,840
Matendo ya Mitume 3 (Biblia Takatifu)Muumini wako Mmoja wa Kike aliyepanda Kutoa Ushuhuda wake kati ya Saa 5 na Robo hadi Saa 5 na dakika 20 leo Kachemsha na Kututhibitishia kuwa ni kweli hawa Watu wa Shuhuda huwa Unawapanga na Kuwaandaa.
Mwamposa huyo Dada mbele yako akiwa anashuhudia alikuambia kuwa alikuwa na Ndugu yake Mgonjwa Hoi Mahututi, hawezi hata Kuongea, hajitambui na Macho yake alikuwa ameyafunga.
Cha Kushangaza huyo Muumini wako wa leo ambaye hukumpangia vyema Script yako ya Kutudanganya Watu ( kama Kawaida ) yako alisema ( alikuambia ) kuwa wakati wakiwa njiani kumpeleka Hospital huyo Mgonjwa wao aliyekuwa Mahututi na Hoi akawaambia wqmlete Kwako Kanisani Arise and Shine Kawe Tanganyika Packers
Pole sana Mwamposa kwani nilikuona hata Wewe Director wa hii Movie na Muandaaji wa Script yako ya Uwongo na Kutudanganya tusiojitambua Ulishtuka kwa Kukosea Kwake huko na Ukakwazika ila ukatumia Akili Kubwa kwa Kuzuga na kuanza Kuimba Wimbo wako pendwa wa ....Namshukuru Mungu..... Namshukuru Bwana...ambao hata hivyo huwa unauharibu kwa Sauti yako mbaya ya Mkwaruzano.
Nilikuwa sijui kumbe Mgonjwa aliye Hoi, Mahututi, hajitambui na amefumba Macho yake anaweza Kuwaambia waliombeba kuwa wamlete Kanisani Kwako hapo Arise and Shine Kawe Tanganyika Packers?
Haya Mfukunyuku Mbobezi MINOCYCLINE nimemaliza huku nikiendelea kuwapa Pole Waumini wako.
Kazi kweli kweli hakyanani....!!!!!!
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
⁷ Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
⁸ Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.
⁹ Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.
¹⁰ Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.
"Petro na Mitume wengine Waliponya Kwa Jina la Yesu na Si Kwa Maji na Mafuta ya Upako." Yanayopelekea Watu kutoa Viumbe hai Mwilini mwao. Eg Nyoka, Mjusi, tandu, Kobe,mdudu, Jongoo na wakati mwingine Hirizi.