Mwamposa kunyanganywa madhabahu ya Kawe kufuatia malalamiko ya wananchi

Mwamposa kunyanganywa madhabahu ya Kawe kufuatia malalamiko ya wananchi

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Kuna taarifa zinatembea chini kwa chini kuwa huenda mtume Boneface Mwamposa akanyanganywa madhabahu ya Kawe baada ya kilio cha muda mrefu cha wananchi kuhusu namna anavyowatendea waumini wanaotoka mikoani kuja madhabahuni kwake.

Katika klipu moja inayotembea kwenye mitandao ya jamii, amenukuliwa mwananchi mmoja akilalamika kwa hisia kali jinsi Mwamposa anavyowatelekeza wafuasi wake na kuwaacha bila chakula wala mahali pa kulala na kujisaidia, hivyo kupelekea wafuasi hao kuchafua mazingira ovyo huko Kawe.

Kufuatia utelekezaji wa wafuasi na uchafuzi wa mazingira, inasemekana serikali imefikia kiwango cha mwisho cha uvumilivu, hivyo kuwa mbioni kumnyanganya eneo hilo ambalo ni mali ya serikali.

Ikumbukwe kwamba serikali ilitoa eneo hilo bure kwa Mwamposa na ilimsaidia kununua viti na vifaa vingine vya madhabahu. Sasa ushirika huu unakaribia kabisa kufikia kikomo baada ya Mwamposa kwenda kinyume na masharti aliyopewa na serikali kabla ya kukabidhiwa eneo hilo la madhabahu.

MAONI YANGU
Mimi naona ni sawa tu hata akinyanganywa eneo hilo sasa hivi itakuwa nafuu kwa wafuasi wake wa mikoani wanaoteseka kwani kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Haiwezekani mtu anavuna mabilioni ya pesa kutoka kwa waumini maskini halafu anatumia pesa zote kujenga hoteli kwa manufaa yake binafsi badala ya kujenga kanisa. Aachie eneo la serikali haraka iwezekanavyo ilitumie kwa maendeleo ya wananchi.

Nawasilisha.
​
 
Ni kweli kabisa mkuu. Hata wewe ukitaka kupata ukweli kwa macho yako mwenyewe, tembelea eneo la madhabahu uone lilivyochafuliwa. Na pia utashuhudia akina mama na watoto waliotekelezwa na Mwamposa.
Kufanya battle na watumishi wa Mungu ni hatare sanaa sanaaaaaa

Mwamposa ni msaada mkubwa na kimbilio la wengii
 
Back
Top Bottom