Mwamuzi wa Mechi ya Yanga na Mamelodi awaomba Watanzania waache kumshambulia kwa Matusi kwa kuwa si yeye aliyetoa maamuzi ya Kukataa Goli

Mwamuzi wa Mechi ya Yanga na Mamelodi awaomba Watanzania waache kumshambulia kwa Matusi kwa kuwa si yeye aliyetoa maamuzi ya Kukataa Goli

Kwa mara ya kwanza Mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya juzi kati ya Mamelodi Sundowns na Yanga Beida Dahane raia wa Mauritania amefunguka kwamba
asilaumiwe kwa lolote lile kwenye sakata la goli la Aziz ki kukataliwa bali lawama zote ziwaendee waliokuwa wana-control Video Assistant Referee (VAR)

Mwamuzi huyo ameeleza hayo wakati aki-chat Instagram na Aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara...

Mwamuzi Beida Pahane ameweka wazi kuwa wakati wa faulo ya lomalisat wanao-control VAR walishindwa kutoa maamuzi hivyo walihitaji msaada wake ndio
maana aienda kuwasaidia lakini Kwenye Goli la aziz.ki hakwenda kuthibitisha kwenye VAR kwa sababu haikuwa kazi ngumu kwa wanao-control VAR kutoa maamuzi,
walimueleza mapema kuwa sio goli, hivyo kama kuna makosa yoyote walaumiwe wao.

Mwamuzi Beida Dahane amefunguka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa Watanzania kwani hakuhusika katīka maamuzi, kama kuna kosa lolote amefanya basi
ataomba msamaha kwa Mungu..

Mwamuzi Beida Dahane amesisitiza kwamba yeye ndiyo anatakiwa kuombwa msamaha maana anashambuliwa sana kutokana na sakata hili, wakati wanaotakiwa
kushambuliwa ni watu wa VAR...

View attachment 2956306

CHAT ZA DM KATI YA HAJI NA MWAMUZI..

View attachment 2956309
View attachment 2956310
View attachment 2956311
View attachment 2956312View attachment 2956313
Awaulize DP World wanajua balaa la wabongo kwenye social media.

Wabongo kwa media tupo juu sana, DP World walikua wanatukanwa hadi youtube kwenye channel yao
 
Kwa mara ya kwanza Mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya juzi kati ya Mamelodi Sundowns na Yanga Beida Dahane raia wa Mauritania amefunguka kwamba
asilaumiwe kwa lolote lile kwenye sakata la goli la Aziz ki kukataliwa bali lawama zote ziwaendee waliokuwa wana-control Video Assistant Referee (VAR)

Mwamuzi huyo ameeleza hayo wakati aki-chat Instagram na Aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Sunday Manara...

Mwamuzi Beida Pahane ameweka wazi kuwa wakati wa faulo ya lomalisat wanao-control VAR walishindwa kutoa maamuzi hivyo walihitaji msaada wake ndio
maana aienda kuwasaidia lakini Kwenye Goli la aziz.ki hakwenda kuthibitisha kwenye VAR kwa sababu haikuwa kazi ngumu kwa wanao-control VAR kutoa maamuzi,
walimueleza mapema kuwa sio goli, hivyo kama kuna makosa yoyote walaumiwe wao.

Mwamuzi Beida Dahane amefunguka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa Watanzania kwani hakuhusika katīka maamuzi, kama kuna kosa lolote amefanya basi
ataomba msamaha kwa Mungu..

Mwamuzi Beida Dahane amesisitiza kwamba yeye ndiyo anatakiwa kuombwa msamaha maana anashambuliwa sana kutokana na sakata hili, wakati wanaotakiwa
kushambuliwa ni watu wa VAR...

View attachment 2956306

CHAT ZA DM KATI YA HAJI NA MWAMUZI..

View attachment 2956309
View attachment 2956310
View attachment 2956311
View attachment 2956312View attachment 2956313
Hamna lolote.
Referee Review Area imeekwa kwaajili ya muamuzi kwenda kujiridhisha pia.
Alitakiwa aende akajiridhishe licha ya kusikia kutoka VAR.
Pia mbona kama kajichanganya??
Maana Lomalissa alivyocheza foul yeye aliamua moja kwa moja yellow card ila baada ya sekunde kadhaa VAR ndio wakamwambia akaangalie na nahisi labda wamemwambia akatizame huwenda ikawa ni possible red card ila alipotizama akakataa akasema ni yellow card.
Kwa nini asingefanya hivyo kwenye goli pia??
Kajikanyaga mwenyewe na maelezo yake.
 
Hivi ina maana mwamuzi mwenyewe haruhusiwi kwenda kwenye VAR room bila kuitwa?
Ile ilikuwa njama ndio maana kwenye kutaka kumpa Lomalisa red card alienda kwenye VAR , Ila kwenye goli alitonywa asiende maana ingekuwa aibu , halafu ukiangalia lile goli lilionyeshwa kwenye angle moja tu na wala halikurudiwa
 
Hivi ina maana mwamuzi mwenyewe haruhusiwi kwenda kwenye VAR room bila kuitwa?
Pale uwanjani pembeni kuna Referee review area video.
Pale anaenda kutizama kujiridhisha na maamuzi alioambiwa na VAR.
Ndio maana hata baada ya kumpa Lomalissa kadi ya njano dakika moja mbele VAR walimuambia akatizame upya foul huwenda ni possible red card,mbona hilo hakulikubali directly akaenda kutizama na kusema ibaki ile ile yellow card??
Kwa kujichanganya zaidi beki wa mamelody aliutoa mpira nje badala aweke kona akawapa mamelody waanzishe.
Aiseeee😂😂😂😂😂😂Afrika nzima nyosso sio bongo tu.
 
Hapa ni kama anakiri kosa sema tu anadhindwa kufunguka.
Tayari refa kafunguka na ametusaidia pakubwa sana pale anaposema there is always mistakes in football, hapo amekiri kuna makosa yalifanyika sasa tumepiga hatua moja kudai haki yetu ya mabilioni ya kuingia nusu fainali. Refa aseme ni mistake gani amemaanisha maana kuna mistakes za maksudi na bahati mbaya, refa akabwe zaidi koo akizidiwa atamwaga mboga na tupambane VAR room officials tuwapate majina tuwafuate kwenye pages zao tukawacharue na wao hadi ukweli ujulikane na Africa nzima wajue bongo hatukubali kuonewa!!

Yanga sasa tukomae na mwamuzi kutafuta jina la officer alietoa maamuzi VAR room ni nani na mpaka anakataa goli ataje alitumia vigezo gani na atuambie kwa nini VAR room hawakuchora mstari kwenye mpira au kuonesha watazamaji sababu ya kukataa goli , Manara amrudie tena mwamuzi ataje jina la alietoa maamuzi VAR kesi ianze upya!

Yaani hapa ndo kumekucha wanayanga hatutakiwi kukubali kurudishwa nyuma kisoka maisha ni vita na soka ni ajira na huleta utajiri na furaha kwa nchi, Yanga tukomae sasa na VAR room officials wa mechi hadi wafunguke, hii itasaidia kuhalalisha madai yetu ya match fixing pale na wao wakianza kujichanganya kama refa ambae hajasema ni goli au sio goli maana hata yeye hana jibu baada ya kuona ngoma imedundia ndani laivu na hakukuwa na sababu ya VAR kukataa goli!!

Nchi nyingi zinaonea wabongo this time tuwaoneshe our true colours kuwa hatuonewi na hatukimbii kesi. Tuwapuuze wanasimba wanaotubeza tunaposaka haki yetu hawa mbumbumbu mfupa wa robo fainali hawauwezi.

Dalili za ushindi ndio zimeanza kwa refa kufunguka sasa wanayanga tukomae na wengine VAR room nao wafunguke na kwakuwa wameanza kuweweseka tutaujua ukweli siku si nyingi. Refa atuambie vigezo VAR room walivyomwambia kuwa sio goli!!

Barua ya Yanga kwa CAF imesaidia sana mechi mbili za robo fainali zilizobaki jana niliziangalia na zilichezeshwa kwa haki na wenye msuli TP Mazembe na Waarabu kupita! Hongera sana uongozi wa Yanga, daima mbele, nyuma mwiko.

Ahsante Sana Bugatti
 
Pale uwanjani pembeni kuna Referee review area video.
Pale anaenda kutizama kujiridhisha na maamuzi alioambiwa na VAR.
Ndio maana hata baada ya kumpa Lomalissa kadi ya njano dakika moja mbele VAR walimuambia akatizame upya foul huwenda ni possible red card,mbona hilo hakulikubali directly akaenda kutizama na kusema ibaki ile ile yellow card??
Kwa kujichanganya zaidi beki wa mamelody aliutoa mpira nje badala aweke kona akawapa mamelody waanzishe.
Aiseeee😂😂😂😂😂😂Afrika nzima nyosso sio bongo tu.
Aibu sana
 
Kitendo cha refa kusema kwa faulo ya Lomarisa kufanya makosa wale VAR Room waliistopisha mechi ili kumpa referee muda wa kuangalia maamuzi aliyoyaamua ni sahihi.

hapa kuna hoja 2 ya mwanzo ni (i) VAR room walitaka referee kutoa Kadi nyekundu ili kuwapa unafuu mamelodi washinde mechi au (ii)hawakutaka referee kutoa kadi but kwa case kama ile lazima walitaka yachukuliwe maamuzi nagumu zaidi lakini refa hakuwa upande wao.

Mwisho wabongo tupo vizuri kwenye kushambulia waliyoweza kuvumilia mambo haya ya kusemwa ni CCM tu,pengine wao ndiyo watuma jumbe za matusi.

nchi imebarikiwa kwa kweli.
 
Mashabiki wa Yanga please mkienda kutukana mjitambulishe kama wana Yanga na si watanzania...

mnatudhalilisha sana..
.

Tunaonekana watanzania siyo wastaarabu kwasababu yenu.
Tumekusikia na from now tutajitambulisha ni wanayanga tunadai haki yetu kupokwa ushindi. Tutajitaja because we are proud of our team performance.
 
Back
Top Bottom