Mwana FA amkana Baba yake mzazi


Hakuna kitu km hicho, uzae halafu wakulelee wengine, mzazi lazima uwajibike kwa mtoto uliemzaa. Kuna wazazi wengine wapuuzi sana. Mzazi usiyejua mtoto anakula nn, analala wapi, amevaa nn au akiumwa katibiwa na nani Kwa gharama zipi, mzazi wa hivyo huna tofauti na mnyama tena kuna baadhi ya wanyama wanalea watoto wao. Mtoto hawezi tu from nowhere asimjali mzazi lazima huyo mtu hakutimiza wajibu wake sawasawa akaachia wengine. Malipo ni hapa hapa duniani[emoji36]
 
Kama Mick Hacknal wa Simply Red
Nimekumbuka "Holding back the years"
Huyu jamaa alipitia mitihani sana lakini alikuja kuwa muimbaji ambaye ni mahiri sana

Ukiwa maarufu na maisha yako lazima yajulikane, hasa kama ulipitia maisha magumu

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Mungu akuzidishie kwa roho nyepesi!

Mungu akuongoze umsaidie anko mkuu maana kuchukua jukumu la mtu( baba ako) aliekua hai akajifanya amekufa kwa kujifanya dume la mbegu sio kazi ndogo aliyoifanya mjomba.

hii mifano tunayo mingi katika jamii zetu me nimeshuhudia mengi juu ya wababa kutelekeza watoto.

Nilitokwa na machozi siku moja nimeenda kumtembelea binamu yangu shule akiwa kidato cha pili, alikuja na rafiki yake kunipokea lakini rafiki yake alikua ana huzuni na kusononeka kuona wenzie wanakula vyakula na wazazi wao yeye hana mzazi aliekuja kumsalimia. nilipomuuliza binamu kwa lugha ya nyumbani akanambia hali ya rafiki yake ilinibidi nirudi mjini kuchukua chakula kingine ili asijione kama anadoea kwa rafiki yake.

Ambao hatuna watoto tujifunze kitu kupitia haya matukio sio kwamba vile leo wallet inazo noti za elfu kumi uwe na kibri hata kwa mtu ambae hata hajatembea kisa mama ake sio mzuri( umelala nae wa nini?) au hatuendani au ni jeuri!

kama mama ake hamuendani achana nae mapema!
 
Nakazia............
 
mdingi alikataa katakata kwamba huyo siyo mtoto wangu sasa hivi anapiga U TURN

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna uhusiano gani kati ya kukataliwa au kutelekezwa na mzazi wa kiume na kuwa na kismati au kupendwa/kufanikiwa sana na kukubalika na jamii?

Hebu chunguza hawa watu maarufu utagundua kitu.
 

Upuuzi huo mie nimeukataa kwanza hatuna bond yoyote na hata tukikaa hatuna la kuongea mi na yeye mbalimbali hana mchango wowote katika Maisha yangu, ukaribu na Mimi aliuanza baada ya kusikia niko chuo kikuu, pasipo kuwa na mchango wowote katika Safari yangu ya Maisha na kielimu. Simuhitaji kwa lolote km ushauri naupata kwa aliyenilea, awepo asiwepo it doesn’t make any difference.
 
Kujifunza kitu kwenye vitu vya kufikirika tu visivyo na uhalisia?
 
Mungu akuzidishie kwa roho nyepesi!

Mungu akuongoze umsaidie anko mkuu maana kuchukua jukumu la mtu( baba ako) aliekua hai akajifanya amekufa kwa kujifanya dume la mbegu sio kazi ndogo aliyoifanya mjomba.

Amiin mkuu.

Na wewe akubariki sana na akufanyie wepesi katika mambo yako ya kila siku yaliyo mema kwa dua yako hii
 
Fuata nafsi yako inavyopenda na usiidhulumu hata kidogo.

Unaweza ukawa unamsaidia/kumjali lakini nafsi ikawa haijaridhia, pale utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.

Kwa hiyo ni vizuri ubaki na msimamo wako huo huo uliouchagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…