Mwana FA amkana Baba yake mzazi

Hilo Jambo linaidhi mianaume inadhalilisha WANAWAKE .kuwakejeli ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka video au ushahidi tuamini lasivyo huu ni adaku kama udaku mwingine, shut up
Kiywaji anachokunywa sio kilevi- pombe ni Red Bull wanakunywa watu wengi hata wasioruhusiwa kunywa pombe. Hivyo muondolee hiyo lawama ya kumita mlevi. Ila niwambie jambo moja dogo, ukiona wazazi wako wamekutelekeza au hawajakusaidia inavyostahili lakini ukafanikiwa katika maisha, usiwalaum ila mshukuru Mungu kupitia kwao. Hiyo ndiyo hekima ya Mungu wetu.
 
Utafanikiwa sana , Mungu akupe nguvu na akuzidishie hekima.
 
wakati mwingine makosa sio ya mwanaume ila mama uliyempa mimba anakwambia mtoto si wako au nitalea mwenyewe na maneno mengine kibao hivyo baba unajisogeza pembeni.
lakini pia unakuwa na mtoto hupewi ushirikiano na mama yake sasa wewe utafanyaje?
kilicho kibaya mtoto analishwa maneno toka mdogo baba yako hakujali ni mimi tu na hii inatokea hata kama ada ulikuwa unapeleka unaweza ambiwa hivyo.
 
Na hilo neno ni kubwa sana. Kuna watu wamezaliwa na vichaa, walemavu wa viungo na wengine wamezaliwa na malaya. Lakini ukishajua huyo ni mzazi wako huna jinsi. Unamshukuru Muumba kufanya yanayo stahiki kwa wazazi wako.
Changamoto za maisha ya wazazi mtoto hawezi kuziingilia. Huwezi jua ni yupi alimkosea mwenzake na sababu ya hayo makosa ni ipi. Ukifukunyua sana unaweza kukuta huyo unayemkumbatia ndiye mkosefu.
 
Hii tabia ya utegemezi kwa watoto ni ya kulaaniwa,wazazi wajipange,hata hao watoto nao wanafamilia zao,wengine basi utakuta hata kulea watoto wao hawakujishughulisha,hata maisha ya watoto wao yanatokana na juhudi zao binafsi<kama mtoto ulimtekeleza toka utoto wake ,atakujali vipi wakati wewe hukumjali?miaka yote ulipotea leo baada ya kumuona mtoto mambo yamemnyokea ndio unakuja mbiombio kutaka msaada tena msaada wenyewe wa kulazimisha kupitia vyombo vya habari vya udaku.Kumbukeni kujijengea maisha yenu ya baadae bila kutegemea watoto.
 
Mtu mwenyewe anaomba msaada,hiyo jeuri ya kufufuana kuendesha bendi atakuwa nayo?nani siku hizi atataka kusikiliza Moro Jazz ,kwa kizazi kipi,wengine hizi ndio huita ndoto za alinacha .Ushauri mzee sasa atafute tu shamba aanze kulima matikiti maji,lakini hizo ndoto za kukufufua bendi ni kichekesho,
 
Mhh naona ma Baba wa kitanzania wanaongoza kunyimwa msaada na watoto wao, na hao ni baadhi tu kwakua watoto wao ni maarufu, kuna wengine kibao ambao hawajulikani nao ni hivohivo. jichunguzeni mnakosea wp ujanani mwenu mnaumiza watoto wenu
 
Huyu jamaa alikulia bush Muheza huko si ajabu dingi alikua hana time
Dingi alikuwa Nairobi akiburudika na akina Wanjiku kwa muda mrefu,ni kutesa tu kwa zamu,kipindi cha nyuma baba alikuwa anatesa bila msaada kwa mtoto na sasa mtoto ni zamu yake kutesa bila msaada kwa baba,huu ni mchezo usiohitaji hasira bana.Watoto wa siku hawana masikhara wanawapa baba zao kavukavu za uso
 
inasemekana FA alitelekezwa akalelewa na bibi kwa mjibu wa interview aliyowahi kufanya FA.

hivyo atumie njia nzuri ya kumfata mtoto akianza media atakua kama baba daimond na media.
Diamond,Qchief,MwanaFA hawa wote wanadai ni watekelezwa baba zao wamekuja ibuka baada ya kuwaona wanazo na masuperstar,halafu hao hao waliowatekeleza ndio wa kwanza kuwa hawasaidiwi,utasaidiwa vipi wakati walipohitaji msaada wewe ulikuwa unataoa msaada kwingine. pambaneni na hali zenu bana.
 
kaka mwananchi,
lete ushahidi basi tujue ilipoanzia .
usijekuwa umesikia kwenye daladala !
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…