Mwana FA amkana Baba yake mzazi

Mwana FA amkana Baba yake mzazi

Mhmhhh mama weeee ahhh humu JF kuna vituko, halafu mbona umechafukwa hiviiii, by the way pitia post zangu utaelewa kuwa sisapoti wanaume kuzalisha ovyo ovyo..... Ila bado haikufanyi usisamehe makosa yamefanywa na wazazi basi nawe unalipiza kisasi bila kujua sababu hasa ni nini kuna mengi yalitokea kipindi chao kabla na baada ya kuzaliwa wewe, so tusiwanyoshee vidole sana hawa wazazi live simple and God will bless you

Super hero daddy
Hilo Jambo linaidhi mianaume inadhalilisha WANAWAKE .kuwakejeli ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka video au ushahidi tuamini lasivyo huu ni adaku kama udaku mwingine, shut up
Kiywaji anachokunywa sio kilevi- pombe ni Red Bull wanakunywa watu wengi hata wasioruhusiwa kunywa pombe. Hivyo muondolee hiyo lawama ya kumita mlevi. Ila niwambie jambo moja dogo, ukiona wazazi wako wamekutelekeza au hawajakusaidia inavyostahili lakini ukafanikiwa katika maisha, usiwalaum ila mshukuru Mungu kupitia kwao. Hiyo ndiyo hekima ya Mungu wetu.
 
Ila tukumbuke mzazi ni mzazi tu...mimi kwangu haijalishi nn kilitokea huko nyuma lkn wazazi wangu niliwapa upendo sawa. Ingawa kuna miaka dingi alikuwa na mchepuko akamzingua sana maza lkn mwisho wa siku walielewana na maisha yakaendelea mpk alipofariki na muda wote wa matatizo sikuwahi kuchagua upande
Utafanikiwa sana , Mungu akupe nguvu na akuzidishie hekima.
 
Hayo ndiyo matokeo ya kuzalisha halafu unaingia mitini halafu unajiona mjanja kuwadharau single mothers. Mwanaume mwenzangu kama ulitelekeza mtoto na mama yake hakikisha hauhitaji msaada uzeeni. Watoto wa siku hizi siyo wale wa enzi zile sasa hivi JINO KWA JINO. UKINIKATAA BAADAE NITAKUKATAA
wakati mwingine makosa sio ya mwanaume ila mama uliyempa mimba anakwambia mtoto si wako au nitalea mwenyewe na maneno mengine kibao hivyo baba unajisogeza pembeni.
lakini pia unakuwa na mtoto hupewi ushirikiano na mama yake sasa wewe utafanyaje?
kilicho kibaya mtoto analishwa maneno toka mdogo baba yako hakujali ni mimi tu na hii inatokea hata kama ada ulikuwa unapeleka unaweza ambiwa hivyo.
 
Kiywaji anachokunywa sio kilevi- pombe ni Red Bull wanakunywa watu wengi hata wasioruhusiwa kunywa pombe. Hivyo muondolee hiyo lawama ya kumita mlevi. Ila niwambie jambo moja dogo, ukiona wazazi wako wamekutelekeza au hawajakusaidia inavyostahili lakini ukafanikiwa katika maisha, usiwalaum ila mshukuru Mungu kupitia kwao. Hiyo ndiyo hekima ya Mungu wetu.
Na hilo neno ni kubwa sana. Kuna watu wamezaliwa na vichaa, walemavu wa viungo na wengine wamezaliwa na malaya. Lakini ukishajua huyo ni mzazi wako huna jinsi. Unamshukuru Muumba kufanya yanayo stahiki kwa wazazi wako.
Changamoto za maisha ya wazazi mtoto hawezi kuziingilia. Huwezi jua ni yupi alimkosea mwenzake na sababu ya hayo makosa ni ipi. Ukifukunyua sana unaweza kukuta huyo unayemkumbatia ndiye mkosefu.
 
Mwanamuziki mkongwe Mohamed Mwinjuma (MAZINGAZINGA) baba yake mzazi na Khamis Mwinjuma (MWANAFA) baada ya kukataliwa na mwanae na kukosa msaada kabisa ameamua kujikita zaidi kwenye muziki na kutaka kuifufua bendi ya Moro Jazz ambayo anasema ndio ndoto yake kubwa.

Pia amebainisha wala hataki tena kuomba msaada kutoka kwa mwanae huyo maana amemdhalilisha vya kutosha hivyo ameamua kupambana na hali yake.

Mpe neno mzee huyo

53545905_134281164291208_1366937534533206016_n.jpg
Hii tabia ya utegemezi kwa watoto ni ya kulaaniwa,wazazi wajipange,hata hao watoto nao wanafamilia zao,wengine basi utakuta hata kulea watoto wao hawakujishughulisha,hata maisha ya watoto wao yanatokana na juhudi zao binafsi<kama mtoto ulimtekeleza toka utoto wake ,atakujali vipi wakati wewe hukumjali?miaka yote ulipotea leo baada ya kumuona mtoto mambo yamemnyokea ndio unakuja mbiombio kutaka msaada tena msaada wenyewe wa kulazimisha kupitia vyombo vya habari vya udaku.Kumbukeni kujijengea maisha yenu ya baadae bila kutegemea watoto.
 
Mwanamuziki mkongwe Mohamed Mwinjuma (MAZINGAZINGA) baba yake mzazi na Khamis Mwinjuma (MWANAFA) baada ya kukataliwa na mwanae na kukosa msaada kabisa ameamua kujikita zaidi kwenye muziki na kutaka kuifufua bendi ya Moro Jazz ambayo anasema ndio ndoto yake kubwa.

Pia amebainisha wala hataki tena kuomba msaada kutoka kwa mwanae huyo maana amemdhalilisha vya kutosha hivyo ameamua kupambana na hali yake.

Mpe neno mzee huyo

53545905_134281164291208_1366937534533206016_n.jpg
Mtu mwenyewe anaomba msaada,hiyo jeuri ya kufufuana kuendesha bendi atakuwa nayo?nani siku hizi atataka kusikiliza Moro Jazz ,kwa kizazi kipi,wengine hizi ndio huita ndoto za alinacha .Ushauri mzee sasa atafute tu shamba aanze kulima matikiti maji,lakini hizo ndoto za kukufufua bendi ni kichekesho,
 
Mhh naona ma Baba wa kitanzania wanaongoza kunyimwa msaada na watoto wao, na hao ni baadhi tu kwakua watoto wao ni maarufu, kuna wengine kibao ambao hawajulikani nao ni hivohivo. jichunguzeni mnakosea wp ujanani mwenu mnaumiza watoto wenu
 
Huyu jamaa alikulia bush Muheza huko si ajabu dingi alikua hana time
Dingi alikuwa Nairobi akiburudika na akina Wanjiku kwa muda mrefu,ni kutesa tu kwa zamu,kipindi cha nyuma baba alikuwa anatesa bila msaada kwa mtoto na sasa mtoto ni zamu yake kutesa bila msaada kwa baba,huu ni mchezo usiohitaji hasira bana.Watoto wa siku hawana masikhara wanawapa baba zao kavukavu za uso
 
inasemekana FA alitelekezwa akalelewa na bibi kwa mjibu wa interview aliyowahi kufanya FA.

hivyo atumie njia nzuri ya kumfata mtoto akianza media atakua kama baba daimond na media.
Diamond,Qchief,MwanaFA hawa wote wanadai ni watekelezwa baba zao wamekuja ibuka baada ya kuwaona wanazo na masuperstar,halafu hao hao waliowatekeleza ndio wa kwanza kuwa hawasaidiwi,utasaidiwa vipi wakati walipohitaji msaada wewe ulikuwa unataoa msaada kwingine. pambaneni na hali zenu bana.
 
kaka mwananchi,
lete ushahidi basi tujue ilipoanzia .
usijekuwa umesikia kwenye daladala !
 
Mtu mwenyewe anaomba msaada,hiyo jeuri ya kufufuana kuendesha bendi atakuwa nayo?nani siku hizi atataka kusikiliza Moro Jazz ,kwa kizazi kipi,wengine hizi ndio huita ndoto za alinacha .Ushauri mzee sasa atafute tu shamba aanze kulima matikiti maji,lakini hizo ndoto za kukufufua bendi ni kichekesho,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom