Pre GE2025 Mwana FA asema atagombea tena ubunge wa jimbo la Muheza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Muheza inawatu wengi makini wakugombea Ubunge ambao wapo hapa Jijini Dsm.Watu makini wenye uwezo na sifa zisizotia shaka.Huyu Jamaa wasasa akae tu pembeni.WABONDEI TUNAKUJA KIVINGINE.
 
Siasa tamu bhana ukipatia, JAmaa amesema atarejea tena

Mbunge wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Hamis Mwinjuma "Mwana FA" amesema atagombea tena Ubunge wa Jimbo la Muheza katika mwaka huu wa Uchaguzi 2025 ili kuendelea kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Muheza

Mwana FA ameyasema hayo kwenye Kongamano la fursa na Uongozi kwa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Muheza ambapo amesema lolote linalotakiwa kufanyika ili awe mbunge wa Jimbo hilo litafanyika

"Mwaka wa uchaguzi nitagombea tena Ubunge, bado ninautaka Ubunge wa Muheza, na nautaka hatari ukiniangalia usoni unaona huyu anautaka Ubunge" amesema Hamis Mwinjuma

Amesema Mwaka 2020 wakati anaomba Ridhaa ya kuwa Mwakilishi wa la Jimbo la Muheza waliahidiana mambo yaliyokuwa yakiongozwa na kurasa 303 za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo tayari yametekelezwa kwa kiwango kikubwa
View attachment 3230473
Wacha tuone wananchi wa muheza wataamua nini!
 
Akumbuke kwamba this time hakuna kupita bila kupingwa...
Na waliomuweka hapo wote hawapo...
🚮🚮🚮🚮
 
Akae akijua ile mbeleko ya 2020 mwaka huu haipo akipigwa amepigwa.
 
Tumekuwa na wachumia tumbo bila kujali wananchi. Amefanya nini miaka mitano?

Tuwakumbushe tu pesa za burebure wenye nazo dunia ya kwanza wamesema enough is enough mjipange wenyewe.
 
Pauka...

Hakika umepiga penyewe
 
Angekamilisha barabara ya kwenda Magoroto tu mengine atulie.
 
Siasa tamu bhana ukipatia, JAmaa amesema atarejea tena

Mbunge wa Jimbo la Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Hamis Mwinjuma "Mwana FA" amesema atagombea tena Ubunge wa Jimbo la Muheza katika mwaka huu wa Uchaguzi 2025 ili kuendelea kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Muheza

Mwana FA ameyasema hayo kwenye Kongamano la fursa na Uongozi kwa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Muheza ambapo amesema lolote linalotakiwa kufanyika ili awe mbunge wa Jimbo hilo litafanyika

"Mwaka wa uchaguzi nitagombea tena Ubunge, bado ninautaka Ubunge wa Muheza, na nautaka hatari ukiniangalia usoni unaona huyu anautaka Ubunge" amesema Hamis Mwinjuma

Amesema Mwaka 2020 wakati anaomba Ridhaa ya kuwa Mwakilishi wa la Jimbo la Muheza waliahidiana mambo yaliyokuwa yakiongozwa na kurasa 303 za Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo tayari yametekelezwa kwa kiwango kikubwa
View attachment 3230473
Dah hii inchi sasa uhuru umezidi sana...naona wanasiasa sasa wamegeuka miungu watu hata hawaogopi.
 
Back
Top Bottom