Mwana FA: AY alinitosa kwenye collabo ya Zigo Remix

Mwana FA: AY alinitosa kwenye collabo ya Zigo Remix

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Pamoja na urafiki au ukaribu uliopo kati ya Mwana FA na AY lakini kumbe inapofika kwenye kazi huwa inakua tofauti. Mwana FA amesema kuna kolabo ambayo aliomba kushiriki lakini nae ‘akatoswa’ na ameitaja wazi kolabo ambayo aliomba kuifanya ni 'Zigo Remix'.

"Kolabo niliyoomba ni Zigo. Kwanza mimi niliitaka mwanzoni kabisa nikamwambia eh bwana eh mi naomba hii. Sasa AY akaitoa halafu akanipa beat fanya hiyo kama unataka. Nikamwambia umeshatoa mimi sitaki tena".

"Akaja akafanya Remix na Diamond halafu nilipoisikia nikasema eeh bwana ehe humu kama ningekuwa nimepitisha kumi na sita zangu ingekuwa fresh kweli lakini ikawa imeshatoka"

IMG_20170129_143035.JPG
 
Aliyefaa kwenye Zigo ni Platnumz, kazi ni kazi tu, ni kama vile Platnumz kamrudisha jamaa kwenye game kupitia ule wimbo, angeutoa na FA nadhani ungekua na views labda mwisho 500K kufikia leo.
Ukitaka mafanikio weka urafiki pembeni kwenye kazi, tumia logic.
 
Kwani unauza nn Dada, asanten kwa kuja, hahahahaha asingeweza
 
Ila mwana FA nae huwa ana mistari flani mizuri. Ila ukweli unabaki pale pale kua ngoma isingenoga kama alivyonogesha chibudi chibudee
 
Ay ni master plan wa bongo na mziki wake huwa anakaa kimya ila akihamua kufanya kitu the world standup for while I like his hustler
 
Aliyefaa kwenye Zigo ni Platnumz, kazi ni kazi tu, ni kama vile Platnumz kamrudisha jamaa kwenye game kupitia ule wimbo, angeutoa na FA nadhani ungekua na views labda mwisho 500K kufikia leo.
Ukitaka mafanikio weka urafiki pembeni kwenye kazi, tumia logic.
Naungana na wew mkuu
 
Ay ni master plan wa bongo na mziki wake huwa anakaa kimya ila akihamua kufanya kitu the world standup for while I like his hustler
Ni mwanamziki ambaye ni too local hata Uganda hapa hajulikani na yuko kwenye game almost 20 years na anajijua hana uwezo
 
Ha ha ha sevilla amekaa na Espanyol 3-1 ila roho inaniuma hatukutumia chance yakupunguza gap la point na nyinyi hapo
Nashukuri mme tuhakikishia usukani at least for another week.
Sevilla red imewaharibia sana ile
 
Back
Top Bottom