Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Akiongea Jana kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha historia ya klabu ya Yanga, Mwana FA ambaye ni Naibu Waziri wa michezo, alisema kitendo cha viongozi na wanachama wa Simba kukubali kuendesha timu Kwa miaka 6 bila kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya katiba na sheria za uendeshaji wa timu hiyo kuwa kampuni ndiyo chanzo kikubwa cha Mgogoro unaoendelea Sasa.
Aliongeza kusema Kwa Sasa serikali imewaachia wanachama na viongozi waumalize wenyewe lakini itakapoona unaanza kuathiri ukuaji wa soka nchini serikali itaingilia Kati.
Binafsi naungana na Naibu Waziri kwenye hoja yake. Naamini sababu ya Mgogoro huu kuwa mkubwa na kutokuwepo Kwa taratibu zilizo Wazi za uendeshaji wa timu.
Mpaka Sasa Hakuna sheria inayoeleweka iliyoweka mamlaka ya Mwekezaji na mamlaka ya wanachama hasa baada ya mchakato wa awali wa katiba ya Simba sports club company kusitishwa na Baraza la michezo likiwataka Simba aabadilishe kipengele cha 49% ya hisa za upande wa Mwekezaji kumilikiwa na watu 3 badala ya kuhodhiwa na Mtu mmoja kama ilivyo Sasa.
Kwa maana nyingine Mwana FA anasema Simba inaendeshwa kinyemela bila katiba. Na Kwa vile Miaka minne nyuma Mambo yalikuwa yanakwenda vizuri, timu iliachwa iende bila kujua huko mbele lazima watakwama.
Hapa nailauamu serikali na mamlaka zinazosimamia michezo Kwa kitendo cha kuona timu inaendeshwa kinyume cha taratibu lakini Kwa vile inashinda Hakuna anayeshauri au kuchukua hatua. Kipindi kizuri cha kufanya mabadiliko salama ilikuwa ni kipindi timu inapata mafanikio. Kusubiri Mambo yaharibike tuseme "tulijua hawatafika mbali" siyo sahihi.
Kama wizara inajua kuna timu nyingine ina mazingira kama haya na haichukui hatua eti Kwa vile inafanya vizuri basi viongozi wa wizara na wote wanaosimamia michezo wajitafakari maana wanafunika Moto chini ya miguu yao.
Tunaona timu inaendeshwa bila kujua katiba inayotumika ni ya kampuni ambayo ilikataliwa na Baraza na ndiyo aliyotumia Abdalla Mhene "kumteua" Mo kuwa Mwenyekiti baada ya yeye kujiuzulu au ni ya zamani ya mpito kuelekea kampuni ambayo ndo Mangungu aliitumia kusema àlipojiuzulu Try Again Bodi itakaa ichague Mwenyekiti mpya?
Ushauri wangu Kwa wanasimba ni kutokubali kutafuta suluhisho la funika Kombe mwanaharamu apite ili timu itulie Kwa Muda. Wahakikishe Kila kitu kinawekwa Sawa Sasa hata kama watachelewa kupata mafanikio lakini watengeneze timu iliyojengwa kwenye misingi imara ambapo Kila upande ndani ya Simba utakuwa na HAKI na WAJIBU bila kuingilia upande mwingine.