Mwana FA: Kuendesha timu Kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria za uwekezaji chanzo cha Mgogoro Simba

Mwana FA: Kuendesha timu Kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria za uwekezaji chanzo cha Mgogoro Simba

Mwana FA anamjua anayekwamisha huo mchakato kukamilika?

Kuna wale viumbe wanaitwa UCC kama sijakosea hao ndio chanzo cha yote, wamekuwa wakiweka vikwazo kila mara Mo anapotaka kukamilisha mchakato.

Kwa hili Mo asilaumiwe.
Wanaitwa FCC, wameanzishwa na Fair Competition Act, No.8 ya mwaka 2003 (FCA). Wao hawaweki kikwazo kama umefata sheria maana kazi yao ni regulation. Mo hafati taratibu ndo maana waliwekwa kikwazo. Muwekezaji huwezi ukawa mmoja kwa sheria ya nchi yetu. Simba wafata utaratibu.
 
Kama hataki kufuata utaratibu basi aachane na huo mpango wa kuimiliki simba.
Ndiyo maana amesema anaidai Simba na ametaja hadi kiwango, ni vile wengi hamjamuelewa tu ni kama vile amesema mumlipe hela yake awaachieni timu.
 
Kanuni zinataka ivyo mkuu

Ni Mo mwenyewe ndie alikuja na ilo pendekezo la 51%/49%

Kigezo cha kuwepo shareholders watatu ni takwa la kisheria na Mo alitaarifa tangu mwanzo alivyo-submit katiba ya mabadiliko nakumbuka hata bakhresa alikua tayari kununua sehemu ya hisa kati izo 49%. Kama Mo alitoa pesa wakati mchakato wa mabadiliko haujakamilika hayo sasa ni makosa ya Mo mwenyewe, kwanini uwekeze pesa zako kwenye mali ambayo bado haujakamilisha taratibu za kuimiliki?
acha uongo kijana kanuni ziko wazi kuwa mwekezaji ni lazima awe na hisa 49, hii ya wadhamini kuanzia watatu HAIPO ni kauli za midomoni za kina Mwakyembe ndio maana FCC walimpa gharama MO za hisa 49 kuwa ni 19.6B, lakini MO akafunika 20B, yaani unampa mtu mpaka HATI ya kukamilisha mabadiliko badae unaongeza vitu ambavyo HAVIKUWEPO , serikali ndio wahuni namba 1 , kisha ndio waje wengine
 
Ngoja uone mbumbumbu wakianza kumpopoa mawe mwana FA, wamekuwa wakali sana siku hizi
Mwana FA hajui kuwa FCC ndio walitoa HATI ya kukamilisha mchakato ndio maana MO akaweka zile 20B, na pakuweka walimuelekeza wao serikali na gawio wanakula Simba 200M kila mwezi
 
Mwana FA hajui kuwa FCC ndio walitoa HATI ya kukamilisha mchakato ndio maana MO akaweka zile 20B, na pakuweka walimuelekeza wao serikali na gawio wanakula Simba 200M kila mwezi
Wewe muongo, FCC hawajawahi kutoa permit ya kuruhusu mchakato uendelee. In Fact, Mzigo umekwama mezani kwa FCC na ndo maana hela haijawekwa. Mtu mzima kama wewe kuwa muongo haipendezi
 
Watu wengi hawana uelewa wa masuala ya finance katika hili sakata wanafikiri sheria na kanuni za uwekezaji zimepachikwa kumkomoa Mo kumbe izo ni kanuni ambazo zinatumika kwa kila mtu.
kanuni zinataka 49 kwa mwekezaji kwenye hizi timu za wanachama, mambo ya wawe watatu ni kauli za midomoni, ndio maana hukuzisikia wakati wote wa mchakato mwanzoni
 
acha uongo kijana kanuni ziko wazi kuwa mwekezaji ni lazima awe na hisa 49, hii ya wadhamini kuanzia watatu HAIPO ni kauli za midomoni za kina Mwakyembe ndio maana FCC walimpa gharama MO za hisa 49 kuwa ni 19.6B, lakini MO akafunika 20B, yaani unampa mtu mpaka HATI ya kukamilisha mabadiliko badae unaongeza vitu ambavyo HAVIKUWEPO , serikali ndio wahuni namba 1 , kisha ndio waje wengine
Hakuna kitu kama hicho mzee baba. Thamani ya simba haipo documented sasa izo 49% alizopewa Mo na FCC zilikua calculated vipi. utapataje 49% ikiwa 100% haijulikani?. Kwanza hao FCC hawajawahi kutoa hati ya kukamilisha mabadiliko. Bila shaka hapo kati uyo Mo alitaka kufanya janja janja hili suala hata Kigwangala alihoji bahati mbaya sana wanasimba walikua wamezama kwenye mahaba mazito wakaishia kumshambulia tu
 
Wewe muongo, FCC hawajawahi kutoa permit ya kuruhusu mchakato uendelee. In Fact, Mzigo umekwama mezani kwa FCC na ndo maana hela haijawekwa. Mtu mzima kama wewe kuwa muongo haipendezi
Ina maana wakati MO anatoa 20B hundi hujui kuwa FCC walikuwa mashuhuda?
 
Hakuna kitu kama hicho mzee baba. Thamani ya simba haipo documented sasa izo 49% alizopewa Mo na FCC zilikua calculated vipi. utapataje 49% ikiwa 100% haijulikani?. Bila shaka hapo kati uyo Mo alitaka kufanya janja janja hili suala hata Kigwangala alihoji bahati mbaya sana wanasimba walikua wamezama kwenye mahaba mazito wakaishia kumshambulia tu
mzee watu walishafanya kila kitu kuhusu mali za Simba na thamani zake, ndio maana siku 20B zinawekwa FCC walikuwepo
 
acha uongo kijana kanuni ziko wazi kuwa mwekezaji ni lazima awe na hisa 49, hii ya wadhamini kuanzia watatu HAIPO ni kauli za midomoni za kina Mwakyembe ndio maana FCC walimpa gharama MO za hisa 49 kuwa ni 19.6B, lakini MO akafunika 20B, yaani unampa mtu mpaka HATI ya kukamilisha mabadiliko badae unaongeza vitu ambavyo HAVIKUWEPO , serikali ndio wahuni namba 1 , kisha ndio waje wengine
Wewe acha uongo.
 
Huyo Waziri hayuko well informed kwani hata Yanga huo mchakato haujaanza kabisa kinachowabeba ni mafanikio ya kubeba ubingwa mfulululizo miaka mitatu,ikitokea wakaanza kupoteza hayo makombe na Simba wakajipata nako kutanuka tu. It's just a matter of time
 
Iyo haikua sharti la serikali bali ni taratibu za uwekezaji ndizo zinataka ivyo yaani hata ingekua yanga, azam, singada n.k nao pia wangetakiwa kufanya ivyo
Azam ina wawekezaji wangapi? Au Azam sio timu iliyopo Tanzania?
Hii ishu inaihusu Simba na Yanga na serikali ina mikono yake moja kwa moja kwavile ni timu za wanachama. Kabla ya Simba kuingia kwenye huu mchakato, wala hakukuwa na kanuni, muongozo wala kanuni yeyote ile serikali ikiwaongoza ni nini cha kufanya. Ila baada ya kuingia kwa mchakato ndio serikali kupitia BMT na FCC wakaanza kuweka pingamizi kwenye baadhi ya vitu ikiwemo idadi ya wawekezaji.
 
We Jinga mbona huelewi,Bil 20 haijawahi kuwekwa na mo dewji,lile bango ilikuwa ni utapeli
mzee kila mwezi Simba wanakula gawio la 200M kutoka kwenye ile 20B ebu tuambie kwanini ? inakuwaje bango la utapeli likupeke 200M na upokee
 
Azam ina wawekezaji wangapi? Au Azam sio timu iliyopo Tanzania?
Hii ishu inaihusu Simba na Yanga na serikali ina mikono yake moja kwa moja kwavile ni timu za wanachama. Kabla ya Simba kuingia kwenye huu mchakato, wala hakukuwa na kanuni, muongozo wala kanuni yeyote ile serikali ikiwaongoza ni nini cha kufanya. Ila baada ya kuingia kwa mchakato ndio serikali kupitia BMT na FCC wakaanza kuweka pingamizi kwenye baadhi ya vitu ikiwemo idadi ya wawekezaji.
Ni uhuni hakuna kanuni yeyote iliokuwa inazungumzia wawekezaji wawe watatu, wamechomekea mbele ili kukwamisha watu na kuendelea kupiga propaganda kwenye vilabu hivi
 
Azam ina wawekezaji wangapi? Au Azam sio timu iliyopo Tanzania?
Azam inamilikiwa na bakhresa group simba inamilikiwa na wanachama ni timu ambazo zinatofauti katika mifumo yao ya uendeshaji
Kabla ya Simba kuingia kwenye huu mchakato, wala hakukuwa na kanuni, muongozo wala kanuni yeyote ile serikali ikiwaongoza ni nini cha kufanya. Ila baada ya kuingia kwa mchakato ndio serikali kupitia BMT na FCC wakaanza kuweka pingamizi kwenye baadhi ya vitu ikiwemo idadi ya wawekezaji.
Mkuu acha kuongea mambo kwa hisia simba ina katiba yake TFF ina taratibu zake sasa kivipi useme hapakua na kanuni wala miongozo au unataka kusema kwamba kanuni zilikuwepo lakini kabla Mo ajaja na suala la kuimiliki simba izo kanuni hazikua zinazingatiwa? Kama hapo awali kanuni hazikuzingatiwa je tuendelee kufanya mambo kienyeji au tukate huo mnyororo na turudi kwenye mstari?
 
We Jinga mbona huelewi,Bil 20 haijawahi kuwekwa na mo dewji,lile bango ilikuwa ni utapeli
Timu ilikuwa inajiendeshaje? Kuna tatizo ni kama vile kuna utapeli unataka kufanyika. Embu tuambie maana umeandika kwa kujiamini, tumjue tapeli ni nani. Timu ilikuwa inaendeshwa kwa fedha zipi?
 
Huyo Waziri hayuko well informed kwani hata Yanga huo mchakato haujaanza kabisa kinachowabeba ni mafanikio ya kubeba ubingwa mfulululizo miaka mitatu,ikitokea wakaanza kupoteza hayo makombe na Simba wakajipata nako kutanuka tu. It's just a matter of time
Sio kweli, Yanga wameanza mchakato ila bado tu kukamilika.

Yanga wao walianza na kufanya tathimini ya mfumo sahihi wa uendeshaji wa klabu kupitia La Liga.
Mchakato huo ukakamilika kwa kupewa mapendekezo na wakaanza kuyafanyia kazi kwa kuanza na katiba mpya. Ikaandaliwa katiba mpya kisha wakaiwasilisha ili ipitiwe na kisha ipitishwe. Katiba ikapitishwa na serikali na pia wanachama wa Yanga.

Hersi Saidi aliwahi kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji kuwawameweka muundo bora wa uongozi ili kuhakikisha wawekezaji wanaokuja kuwekeza kwenye klabu hiyo wanapata manufaa wanayoyataka badala kufanyiwa ujanja ujanja.

"Tunajenga mfumo ambao mwekezaji akija anakuta muundo bora wa utawala, kimapato. Malengo yetu ni kuhakikisha kuwa na timu imara kiuchumi ili yule anayekuja awe na uhakika wa kile anachowekeza kwenye timu.

"Hivyo tumezingatia sana usalama wa biashara kwa kila ambaye ana nia ya kuwekeza kwenye Klabu yetu." Mwisho wa kumnukuu.

Tarehe 1 mwezi wa 4 Hersi akaja kuzungumzia kuwa wanaanza mchakato wa kuifanya Yanga kuwa kampuni na aliongea vyema sana kwa kutoa ufafanuzi juu ya hiyo hatua. Ila sijajua hiyo hatua imefikia wapi

Back
Top Bottom