Sio kweli, Yanga wameanza mchakato ila bado tu kukamilika.
Yanga wao walianza na kufanya tathimini ya mfumo sahihi wa uendeshaji wa klabu kupitia La Liga.
Mchakato huo ukakamilika kwa kupewa mapendekezo na wakaanza kuyafanyia kazi kwa kuanza na katiba mpya. Ikaandaliwa katiba mpya kisha wakaiwasilisha ili ipitiwe na kisha ipitishwe. Katiba ikapitishwa na serikali na pia wanachama wa Yanga.
Hersi Saidi aliwahi kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya kimfumo na kiutendaji kuwawameweka muundo bora wa uongozi ili kuhakikisha wawekezaji wanaokuja kuwekeza kwenye klabu hiyo wanapata manufaa wanayoyataka badala kufanyiwa ujanja ujanja.
"Tunajenga mfumo ambao mwekezaji akija anakuta muundo bora wa utawala, kimapato. Malengo yetu ni kuhakikisha kuwa na timu imara kiuchumi ili yule anayekuja awe na uhakika wa kile anachowekeza kwenye timu.
"Hivyo tumezingatia sana usalama wa biashara kwa kila ambaye ana nia ya kuwekeza kwenye Klabu yetu." Mwisho wa kumnukuu.
Tarehe 1 mwezi wa 4 Hersi akaja kuzungumzia kuwa wanaanza mchakato wa kuifanya Yanga kuwa kampuni na aliongea vyema sana kwa kutoa ufafanuzi juu ya hiyo hatua. Ila sijajua hiyo hatua imefikia wapi