Mwana J.F..Unakula Tsh.ngapi kwa siku?

Mwana J.F..Unakula Tsh.ngapi kwa siku?

Hahah tui-round off iwe 30,000/- kwa siku. It is reasonable kabisa...



Hahaha ukiwa na mtu ndani unakula nyumbani mara nyingi.

Nakumbuka hapa juzi nilikaa na mtoto wa aunt yangu anasoma chuo. Nilikuwa nampa 250,000/- kwa mwezi yani siwazi kabisa nitakula nini.

Mwisho wa mwezi tunaenda zetu ferry tunanunua mchele, unga, sukari na mafuta...mboga anapanga ratiba mwenyewe plus kuhakikisha anapata ya kwake ya lunch akiwa chuo na iliwezekana kabisa...ndipo nikaamini hata nikioa sitapata shida sana.



hiyo ni past tense ticha lol!!!
Niliwahi kukaa na kaka yangu mwezi mmoja baada ya kumaliza chuo ikawa lunch na diner anakula nyumbani, alishangaa jinsi gharama zilivyopungua kwa huo mwezi, so inawezekana.

Hiyo past tense inabidi uirewind kwakweli[emoji12] [emoji12]

Sasa jirani inabidi nipange ratiba ya kukutembelea, hiyo bajeti inatutosha kabisa.
 
Mkuu tangu niko darasa la sita sijawahi kumjua house girl maishani mwangu so huku kulalamika nimeshazoea ila siezi kuweka housegirl wa kunifanyia kazi kwangu nikishindwa kabisa nitanunua mashine.

Mimi hata girl friend wangu (natamani angekuwa humu awathibitishie) hanifulii nguo na akipika ni kwa sababu tu yupo ila sio kwa sababu i expect her to cook!!!

Kwa ufupi tuseme ni mazoea sio kwamba kuna ubaya wowote!!!
Naomba kuijua profession yako mkuu
 
Kwa hiyo ukirudi home mnapima uzito wa chakula?

au umemaanisha kwa mfano ni wali, basi mnapima mchele kg 2???? Na huo ni wako mwenyewe au ndo familia nzima? na mko wangapi? sorry kwa maswali mengi...

Usijali. Nanunua mchele kwa mwezi mzima, nikigawa kwa siki najua imetumika kilo ngapi. Lazima niwe na bajeti nnayoilewa. Kwa iyo nikiweka home kilo 100. Najua approximation ni siku gani itakua imemaliza. Familia nzima pamoja na wanangu
 
Piga hesabu Asubuhi hiyo
14991179_702198949938535_462541079255427063_o.jpg


Screenshot_20161113-102448.jpg
 
Home 10,000
Mchepuko 15,000
Lunch 4,000
Beer 20,000
Petroleum 10,000
Vocha 2,000
Vinginevyo 10.000
Jumla 71,000 per day
 
Kwa siku natumia 48,000/=
1.Wali au Ugali (2500 au 1500)
kg per day
2.Nyama au Samaki (7000 au 10000)
3.Mkaa au mafuta au gesi (1500 au 1200 au 1700)
4.Maji (kupika kuoga kufua)=1500
6.Maji ya kunywa =1300
7.Umeme 4units per day=1500
8.Hg mshahara per day 1500
9.Mafuta ya gari per day 10000
10.Mafuta ya kupikia per day 600.
11.Chai maziwa 2000 na mkate 1000.
12.Gharama za nyumba 10000 per day.
13.Matunda 3000.

Total = ~ 48,000/=
Nimependa mchanganuo wako maana una reality ndani yake
 
Dah....
Chai + chips dume 200
Ugali + udaga + tikiti 800
Pilau + kachukachu + ndizi 1000
Jumla 2000 kiroho safi
[emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14]
 
Mi najua natumia not more than 400k per month! Labda itokee dharura kweli kweli!
 
Mchepuko wagu wenyewe mama ntilie af yupo karb na ofice so nnakuuulaje..[emoji23]
asbuui chapati8 supu ya buku2 mayai ya kuchemsha3 maarage ya jero mchana ugali6 na samaki mkubwa sana af jion kwangu/hom
 
Back
Top Bottom