TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

Mkuu kwanini ukereke kwa kitu ambacho hakikupunguzii chochote kwenye maisha yako ya kila siku!? Haya "makurasa mengi" hapa yanakupunguzia nini wewe!?

Acha hizo Mkuu kama huna la maana la kuandika kufuatia kifo cha huyu mwenzetu pita kimya kimya.
anazingua huyu
 
Mkuu kwanini ukereke kwa kitu ambacho hakikupunguzii chochote kwenye maisha yako ya kila siku!? Haya "makurasa mengi" hapa yanakupunguzia nini wewe!?

Acha hizo Mkuu kama huna la maana la kuandika kufuatia kifo cha huyu mwenzetu pita kimya kimya.
Si bangi tu na kutafuta umaarufu wa kijinga. Tangu lini MTU akaitwa Tindikali???
 
Ingawa hujaniuliza mimi lakini nachoweza kusema kwa uhakika wa kiasi kikubwa, huyo si Kiranga.

Labda kama ungemwuliza yeye na Kuhani, Kuhani Mkuu, Bu'Yaka, na Kwameh ni ndugu? Ni watoto wa baba mmoja? Hapo walau kidogo swali lako lingeukaribia uhalisia.

Wengine tushamzoea na hayo mazoea yake ya kuanzisha tahanani hata pasipostahili.

Baada ya hayo niseme tu kuwa nimesikitika mno kumpoteza rafiki.

Apumzike kwa raha tele na amani bwerere huko aliko. Nitamkumbuka saaaaaaaaaana.
Nashukuru ingawa sijasema ni Kiranga ,nimeuliza kama ni watoto wa baba mmoja
 
Msiba wa Dena Amsi umetusitua wengi sana maana siku Moja kabla ya kifo chake nilipiga nae story sana nyumbani kwao. Alikuwa mzima kabisa na kiukweli alikuwa MTU wa watu kaniaaidia mambo mengi sana mpaka siku ya mwisho kuonana nae nilikuwa natafuta sanduku la posta la manispaa ya kinondoni alinisaidia akampigia rafiki yake nikalipata. Kwa wale ambao mngependa kuja kuwapa pole wafiwa msiba ulikuwa BUNJU A shule maeneo ya juleva.mungu ailaze pema roho ya Dada yetu Dena Amsi(Leah Flavian komba) jina lake halisi



Duh umenishtua sana kumbe Dena Amsi ndio Leah Komba
Binafsi namfahamu marehemu (Leah Komba) nimewahi kufanya field ofisi ambayo alikuwa anafanya kazi na nimewahi kumfanyia kazi zake nyingi nakumbuka mara ya mwisho tuliwasiliana alipata kazi Kenya akahamia Nairobi
Pumzika kwa amani Leah
 
Hii thread ni ya mwaka 2014
Mkuu una uhakika unacho kinena?Labda kama kingereza kimekupita kulia. Two days ago maana yake ni SIKU MBILI ZILIZOPITA. Maana ya siku mbili zilizopita maana yake ni juzi
1482995292876.png
 
Back
Top Bottom