TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

Hakuna ubaya kuanika utambulisho wake kwa sababu kwa sasa hatunae tena pia inasaidia kuweka historia yake sawa kwa wasiomfahamu!
Wewe tiririka wasufu wake hapa, ili tumfahamu vema!

Nitakua mpumbavu sana nikifanya hayo!!
Unajua kwa nini aliamua kutumia id yake (iliyoficha utambulisho wake)? Bila shaka alikua na sababu zake!
Kama hakujianika akiwa hai, kwa nini umuanike wakati asioweza kujitetea?
Unless iwe aliacha maagizo ya kuwekwa humu....sisi ni nani hata tumuamulie?
 
Wewe umetangulia sisi tutafuata......pumzika kwa amani....kipenzi chetu.....

Siwezi kuyazuia machozi....
[emoji24]
 
Nitakua mpumbavu sana nikifanya hayo!!
Unajua kwa nini aliamua kutumia id yake (iliyoficha utambulisho wake)? Bila shaka alikua na sababu zake!
Kama hakujianika akiwa hai, kwa nini umuanike wakati asioweza kujitetea?
Unless iwe aliacha maagizo ya kuwekwa humu....sisi ni nani hata tumuamulie?
Sijakulazimisha kutelezea wasifu wa ndugu yetu Marehemu, ila kila mtu anaweza kumuelezea kwa jinsi anavyomfahamu sio kuleta hapa mawazo mfu eti tusiseme au kueleza wasifu wa ndugu Dena Amsi kwa sababu alitumia Fake ID hapa JF!!.

Akina Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, John Okello, Omari Makunganya, Chief Mkwawa wasifu wao ungefichwa leo hii watu tungeliwafahamu kweli?

Acha mawazo mfu wewe!!!
 
Poleni wafiwa na Mola ampe pumziko la milele mahali pema peponi
 
Huyu dada tulimpenda sana hapa,. hasa kule MMU. ni vizuri tungemfahamu wasifu kidogo. Hata msiba hamuwezi sema upo wapi. Anyways.... RIP.
 
Back
Top Bottom