TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

TANZIA Mwana JamiiForums mkongwe, Dena Amsi afariki dunia

Mimi sio Mswahili mwenzenu, mwenzenu wewe na nani? Jiongelee mwenyewe! Usibane wigo wa msiba kwamba ni wako wewe Mswahili tu!

Halafu wewe huwezi kutathmini ufasaha wa Kiswahili ninachoandika mimi na kunipa sifa, kwa sababu wewe mwenyewe chako kimepinda! Lakini hiyo si mada ya leo.

Unasema msibani watu hujua legacy ya marehemu kwa kupiga soga hapa na pale, kwa hiyo kumbe "legacy ya marehemu" kitu hicho kipo na hujulikana, hata misiba ya Kiswahili.

Sasa hapa kuna kurasa zaenda hamsini tumejaza marudio ya RIP Dena Amsi, Inna Lillahi wa Inna, Bwana amempenda zaidi kamuua, pole sana tunakukumbaka... tunakukumbuka kwa lipi? Hakuna anaejua!

Halafu kwenye misiba, iwe ya Kiswahili au ya Ki-Spanish, kuna mtu anasimama rasmi anamuongelea marehemu kirefu, na wengine husoma eulogy kujaribu kueleza legacy ya marehemu. Usinambie ni kukutana kupiga soga, kupiga mayowe ya vilio, kuzika, kurudi kula ubwabwa, kuondoka! Mswahili wa wapi wewe?

Dunia imebadilika siku hizi, huyu Dena ambae kurasa hamsini hakuna anaemkumbukia kwa lolote tusije kuwa mithili ya waombolezaji wa kukodishwa.




Hapana ahsante, mimi nikifa msijaze kurasa ndeeefu za R.I.P na kariri za Inna Lillahi wa Inna na Bwana ametoa Bwana ametwaa kwa kumpiga limkuki la mdomo kwenye bifu na wafugaji.... no, spare me with the superstitious horse dang please kama hakutakuwa na cha mno nilichokiachia legacy zaidi ya "alikuwa mwanajamii mwenzetu..."
Wewe na Kiranga ni watoto wa baba mmoja ?
 
nimepitia thread zake nimejikuta nalia tu jamani thread zake zote sijaona.mbaya hata moja
alikuwa ametukuka hapa jf
daaah rip
Punguza kulia.

Na ujitahidi kumfanyia Maombi
 
Wewe na Kiranga ni watoto wa baba mmoja ?
Ingawa hujaniuliza mimi lakini nachoweza kusema kwa uhakika wa kiasi kikubwa, huyo si Kiranga.

Labda kama ungemwuliza yeye na Kuhani, Kuhani Mkuu, Bu'Yaka, na Kwameh ni ndugu? Ni watoto wa baba mmoja? Hapo walau kidogo swali lako lingeukaribia uhalisia.

Wengine tushamzoea na hayo mazoea yake ya kuanzisha tahanani hata pasipostahili.

Baada ya hayo niseme tu kuwa nimesikitika mno kumpoteza rafiki.

Apumzike kwa raha tele na amani bwerere huko aliko. Nitamkumbuka saaaaaaaaaana.
 
nimeandika posti mbili ndefu nikianisha swali langu, kama hujanielewa sidhani kama kuna jinsi ya kuiweka vingine.



Legacy ningeiweka kwa muktadha wa nyinyi Waswahili ningeeleweka?

Kwa hiyo huu msiba wawahusu Waswahili tu? Nitaiwekaje legacy kwenye muktadha wa legacy za Kiswahili kama labda mimi sio Mswahili?

Waswahili kuhuzunika msibani ni jambo la kawaida na kama sijahuzunika msiba haunihusu. Kwa hiyo huu ni msiba wa Kiswahili mimi siwezi kuulewa, sio?

Msiba wa Kiswahili ni kwamba hauna mambo ya kueleza kuhusu legacy za marehemu, tunamkumbukia nini marehemu, ni tunalia weee, tunazika, tunakula ubwabwa, tunajaza ma pages ya R.I.P, tuna move forward!

Sawa ndugu, labda sintakaa nikaelewa misiba ya Kiswahili!
Wakati mwingne ata ukikaa myaa napo unaeleweka..sio lazma uchangie post yoyte
 
Back
Top Bottom