Mwana JamiiForums mwenzangu, msamehe mke wako japo ni kweli alichepuka kwa mume wa shosti yake

Mwana JamiiForums mwenzangu, msamehe mke wako japo ni kweli alichepuka kwa mume wa shosti yake

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Habari viongozi, na watu wote.

Naomba kwanza ku-declare my side ni kwamba siwezi kumwacha mke wangu niliezaana nae hata mtoto mmoja tu kisa amechepuka.

Kuna ndugu yetu humu ndani amemfukuza jana mke wake huko Dar baada ya mke wa mume aliyechepuka na mke wake kuja na kundi la watu wakiwa na madela kwa lengo la kumsuta na kumchana. Tarumbeta, ngoma, filimbi na mayowe mengi yalisikika.

Kutokana na kelele nyingi dada wa kazi alitoka nje na kukuta nyimbo zinaimbwa alipouliza kuna nn? Akaishia kuulizwa mtu fulani yupo? Akajibu hayupo ila mume wake yupo, wakaona hata kama mhusika hayupo, ngoma iliendelea kwa mda mda sana.

Dada wa kazi alipoingia ndani akaulizwa na mume kuna nn nae dada kasema kila kitu. Baadae baada ya mke kuja mwana jamiiforums wenzetu amekasilika na kumfukuza mke wake kwanza ana watoto 2 pale nyumbani na pili utaratibu haujafuata na tatu hajasikiliza upande wa mke. Hasira na wivu umemjaa kiasi cha kushindwa kutumia busara na hekima katika hili.

Namshauri mke wako sio malaya na nakili ametenda kosa ila tabia yake unaijua vizuri sio muhuni.

Usimwache mke kisa kuchepuka kwani kufanya hivyo ni kutoa gome kwenye jicho la mwenzako na wakati huo ww una boriti jichoni kwako
 
Unajuaje kwamba ^amekasilika^ na wewe? Au tu ^unakili^ mambo ambayo huna uhakika nayo? Unaweza kujua nani ^muhini^ kati yako na huyo shemeji yako aliyemwacha mkewe!

NB: Punguza Frustration utakuwa vizuri tu.
Maamuzi ya kumrushia nguo nje yaani hata ndani hakuingia inathibitisha hasira aliyo/uliyokuwa nayo. Tabia ya mtu inajulikana ila makosa tumeumbiwa cc binadamu na hakuna mpaka wa makosa ,iwe kuua au kuzini
 
Bila shaka itakuwa ni ww unaomba msamaha indirect. such interesting
 
Kujiajiri kugumu ndugu zangu.

Siku hizi natembeza viatu vya kike sasa nipo hapa Manyanya nimekutana na ex wangu hivi ninavyoandika tupo kwenye bodaboda tunarudi nyumbani.

Mniombee
Muulize hajaolewa maana mwenye avatar ya blue blue kamtimua mke kimbogo mbogo,Isije akawa yy
 
Namashaka na jinsia yako..sio hivi [emoji117][emoji2523] kweli wewe
 
Mkuu mbona hueleweki

Mke wake s Malaya ila unakili kabisa amechepuka


Kuna tofaut gan Kat kuchepuka na kuwa Malaya

Ufafanuz tafadhar

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mke wake hana tabia hiyo hata mtaa unashangaa ila mm namlaumu shosti yake ambaye alikuwa anampeleka home kwake, kumbe mume wake ni fisi.

Alikuwa anamtongoza kwa sms na sms hizo zilifumwa na shosti yake na akaenda na matarumbeta nyumbani kwa mhanga.

Ndio maana nimesema ni kweli mke kachepuka kwa kuwa alikuwa na namba ya mtu mwingine ila hajawahi kutana nae kimwili.

Kwanza angemsikiliza kwanza mke wake na kuliko alichofanya badass kwa mke wake,
 
Back
Top Bottom