TANZIA Mwana JamiiForums mwenzetu Kanungila Karim amefiwa na baba yake mzazi

TANZIA Mwana JamiiForums mwenzetu Kanungila Karim amefiwa na baba yake mzazi

Amazing grace how sweet the sound
That saved a wretch like me
I once was lost, but now I'm found
Was blind but now I see
🙏🙏🙏🙏🙏
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu mwenzetu, rafiki, Kanungila Karim amefiwa na baba yake mzazi! Msiba upo Morogoro, Kilombero.

Binafsi nachukua nafasi hii kumpa pole sana sana, Mwenyezi MUNGU akawape subra na wepesi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa familia yenu.[emoji22][emoji22][emoji22]

POLE SANA RAFIKI!

ILIVYOKUWA:
Jana majira ya saa 7 usiku mzee wake alikuwa safarini kwa usafiri wa trekta akitoka nyumbani kwake Kilombero na kuelekea mashambani Mang'ula kwa ajili ya kuvuna mpunga.

Akiwa pamoja na dereva wake yeye(mzee wake) alikuwa amekaa pembeni ya trekta. Trekta ilipofika karibu na daraja la Ruaha Mkuu lilitikisika na kumtupa pembeni mzee wake na kupelekea umaiti.[emoji24][emoji24][emoji24]

Huuu ni msiba mkubwa wa pili kwake ndani ya muda wa miaka mitatu(3) tangu ampoteze mama yake kwa presha mwaka 2020.


Dedication[emoji120][emoji120]
Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.
Salama, Salama,
Rohoni, Rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.

Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani;
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.
Pole sana Karimu
 
May his soul fly high pole sana jombi KANUGILA
 
Pole sana Kanungila Karim Mungu akupe faraja katika kipindi hiki kigumu.

May his soul rest in eternal peace 🙏
 
Dah.. apumzike kwa amani mzee wetu,

Mungu amtie nguvu kipi hiki kigumu kwake ndugu yetu.
Kila mmoja atakwenda muda wake utakapofika.
 
Pole nyingi sana kwako Kanungila Karim pamoja na familia na wahusika wote.
Hitimisho la maisha ya mwanadamu na hata viumbe vingine ni kifo, japo kinauma sana lakini hakuna namna zaidi ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha aliyo tudhamini na kumshukuru pia anapoya hitimisha.
 
Back
Top Bottom