Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohamed Salman anusuruka Kuuawa huko Riyadh

Mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohamed Salman anusuruka Kuuawa huko Riyadh

Watajuta hao waliotaka kumuua, anajua ana maadui wengi sana ndio maana anashirikiana na USA na Israel kwa ulinzi zaidi.
Ww kweli hujielewi toka lini israel na USA wakawa marafiki na mtu hao wanaangalia maslahi yao tu ukienda kinyume na wao wanakuua na wameshaona sasa hv saudia anaanza kuwa upande wa Russia na kitendo cha kukubali malipo ya mafuta bila dollar hapo tayari ishakufa nongwa
 
Jaribio la kumuondoa uhai limefanyika jana. Na mpaka sasa hakuna report yeyote official ya kinachoendelea iliyotolewa na ufalme wa Saudi Arabia. Saudi Arabia imekua ni mshirika mkubwa wa Marekani na israeli katika siku za hivi karibuni hasa kwenye mgogoro huu wa Palestine na Israel. Kijana Mohamed Salman anaonekana kutaka kuleta mageuzi ndani ya nchi hiyo ya kiislamu huwenda ikawa ni sababu ya wanaopinga utawala kuamua kuchukua jukumu la la kutaka kumuua.

View attachment 2983068
Wee mgalatia uchwara hizi porojo z Twitter unatuletea huku tujadili?
 
Nani alikwambia ukitaka usife unatakiwa ulindwe ma marekani au israeli?
Shetani yuko kazini , unaweza tangulizwa kabla ya wakati wako. Kwa mfano mtu anachepuka na kupata magonjwa unafikiri ni mpango wa Mungu upate magonjwa na kufa mapema?
 
Kama na hili hujui pole sana
Inamaana hujui kwenye kurithi kiti cha ufalme sio yeye anayefuata
Aisee jamiiforum kuna watoto wengi sana

Tukio la juzi juzi mpaka yule tajiri mkubwa saud arabia mwenye asili ya ethiopia kuwekwa kuzuizini pamoja na prince karibia wote nalo tena hulijui pole sana
Kwahiyo huo ndio ushahidi wako kuwa jamaa kawekwa hapo na marekani?
 
Yatatembea Majambia Hapo Hawataamini.
Huyu jamaa maadui wake hawatoki mbali ,kawafanyia umafia sana ndugu zake mpaka kupata hiyo nyadhifa , kuna yule binamu yake ambaye alikuwa waziri wa ulinzi ndio alipaswa kutake over na kupata hiyo nyadhifa, alimteka na kumweka kwenye hotel na kumfanyia blackmail , masaudi wote wale prince wengine matajiri walifanyiwa hivyo hivyo wakawekwa kwenye hotel moja na kuzuiwa kusafiri nje ya nchi na bank accounts zao kuwa freezed na pesa zao kutolewa .
 
Marekani wakati wa trump ndo waliomuweka
Kiutaratibu wa kifalme sio yeye anayefuata na aliwaweka kizuizini maprince wote baada ya kuwa mfalme

Yule ni kibaraka wa nchi za western ndo maana katoa kibali cha kufungua duka la kuuza pombe riyadh na mabadiliko kibao anayafanya ambayo hapo nyuma hakuna aliyetegemea yatafanyika saud arabia
Ufalme wa saudia wote sio watawala halali wa hilo eneo,,,,walipewa kwa sababu walikua chawa wa wazungu enzi za kupambana na Otoman, hao jamaa walishirikiana na mabepari , na ndo maana ili waendelee kutawala hilo eneo lazima wawalambe miguu wazungu
 
Watajuta hao waliotaka kumuua, anajua ana maadui wengi sana ndio maana anashirikiana na USA na Israel kwa ulinzi zaidi.
Hao Wamarekani na Israel ndiyo wanaomtafuta huyo, niliwahi kuandika hivi:

Jaribio la kumuondoa uhai limefanyika jana. Na mpaka sasa hakuna report yeyote official ya kinachoendelea iliyotolewa na ufalme wa Saudi Arabia. Saudi Arabia imekua ni mshirika mkubwa wa Marekani na israeli katika siku za hivi karibuni hasa kwenye mgogoro huu wa Palestine na Israel. Kijana Mohamed Salman anaonekana kutaka kuleta mageuzi ndani ya nchi hiyo ya kiislamu huwenda ikawa ni sababu ya wanaopinga utawala kuamua kuchukua jukumu la la kutaka kumuua.

View attachment 2983068
Fake news
 
Saudi Arabia mgogoro wa kiutawala hautoisha. Na serikali zao hutumia nguvu nyingi sana kulinda tawala zao, wako radhi kufanya lolote na ni wakali kweli ukiwachezea. MBS ana maadui wengi ndani ya nchi yake kuliko hata nje, kwanza nje wanaomchukia ni Qatar hasa hamna mwingine. Wengineo ni Waislamu wenye msimamo mkali ambao hawajawahi penda kiongozi yeyote wa Saudi hata atoke huyu aje mwingine.
 
Kama na hili hujui pole sana
Inamaana hujui kwenye kurithi kiti cha ufalme sio yeye anayefuata
Aisee jamiiforum kuna watoto wengi sana

Tukio la juzi juzi mpaka yule tajiri mkubwa saud arabia mwenye asili ya ethiopia kuwekwa kuzuizini pamoja na prince karibia wote nalo tena hulijui pole sana
Weka ushahidi wacha talalila
 
Back
Top Bottom