Kwa masikitiko makubwa ninapenda kuwapa taarifa ya mdau mwenzetu humu anayeitwa warumi amefariki usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapambana kwa ugonjwa wa figo.
Warumi alikuwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 29.
Taarifa hii nimepewa na dada yake mda huu, msiba unaelekea kwao Tegeta .
UPDATE:
Msiba upo Tegeta Nyuki, ukifika Stand unachukua boda au bajaj unawaambia wakupeleke nyumbani kwa Kiboko, maana msiba upo opposite na utaona geti jeusi liko wazi - ingia.
Msiba utasafirishwa kwenda Mbeya, Nonde Mabatini.
UPDATE.
Misa ya kumuaga itafanyika kesgo tarehe 27 August saa 8 mchana Muhimbili.
Maria za miaka, hata kama jukwaa lako halipo ndio ukimbie??😁Rip kamanda
Alisikitisha sana huyo member, alikua anaitwa mpauko au miguu ya kuku....kaja mara kadhaa kuomba msaada hakupata, akaandika sijui anataka kujiua anaulizia sumu, comments zilizokua zinaandikwa daah 😢😢, hatimae akajinyonga.Wee!sikuona hyo ya kujinyonga!!!kuna watu wakatili sana humu kama madudu vile!
Daahh!huzuni sana!tubadilikeni jamani mtu akija kuomba msaada asaidiwe huwezi kaa kimya kumtusi au kashfa zinaumiza sana!mwingine hana uwezo wa kuhandle maumivu
Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Usifanye hivi tena mkuu.mkuu mbn humu JF tunafahamiana wengi tu ni wewe tu km utaamua kuishi safi na wengne
mfn. mm nilimfahamu mshanajr humu jamiiforum
lkn tulikuja kuwa washkaji nikaifahamu mpk familia yake na mpaka kwangu ninapoishi alikuja
ninachokushauri usiwe mropokaji wa maneno ya hovyo kwa watu
hapo awali mm na mshana tulikuwa hatuelewani nilikuwa namuattack kwa ID nyingne na siyete tu wengi tu lkn mwisho akaja kuwa mshikaji
mpk leo ile ID siitumii ilikuwa ni ya ujinga mwingi
humu JF kuna watu wanaroho nzuri mno
ambapo serious ikatokea ukwakwama ni rahisi kusaidiwa
hvyo nawashauri WANAJF wenzangu ikiwa mmetofautiana kimtazamo
msiwe na maneno ya kukwazana kwa mwezako humjui nje ipo siku utahitaji msaada ambao yeye ni rahisi kukupatia au kukupa connection
😂😂😂Saaana humu stress zimejaa balaaHumu watu wengi wana msongo wa mawazo, na ni wakari kweri kweri[emoji16][emoji849]
Sasa Mkuu Pascal Mayalla si uratibu hili suala la rambirambi?Duh..., japo mimi sio mwanachama active wa celebrity forum, ila jamaa namkubali sana na nimeguswa.
Zamani JF ilikuwa tukipoteza mwanachama, if management ilikuwa inafanya some sort of organisation, nakumbuka msiba wa Regia if tulitengeneza hadi Tshirts na tuka jiorganize hadi kuhudhuria mazishi kule Ifakara, tena kuna member alijitolea gari yake!
Hebu tazameni hapa chini
I don't know what happened now. Should we push for equal treatment during the demise of our members, tuweke system ya ndugu kuripoti kwa jf management kifo cha mwanachama wetu yoyote regardless umaarufu wake, kisha waweke number ya mchango, wana jf kuchangie, na siku ya kuaga jf management iwepo na kukabidhi mchango kwa wakiwa na mtu wa jf atoe neno.
Na kwenye mazishi ya wana jf wa eneo husika wahudhurie kutuwakilisha.
Kwenye mchango wa rambirambi hata tukiweka minimum TZS 1,000 tuu, kwa jinsi tulivyo wengi, hiyo fedha ina kuwa ina impact kubwa na ni faraja kwa familia kujua mpendwa wao alikuwa mwanachama wa mtandao wa jf na jf wanajali.
Na kwa vile wengi wa wana jf wanatumia pen names, ili kuheshimu the unanimity ya marehemu, humu jf tuu ndio atatajwa kwa jina lake la jf, mfano huyu warumi , lakini
pale msibani no one will mention his name, hata kwenye Salaam za jf, hatamkwi popote kwa jina, bali "marehemu alikuwa mwanachama wetu, alijinga jf lini, amechangia mada mbalimbali etc just that, na if members watakao hudhuria msiba, kwa vile kule wataliona na kulijua jina halisi, kanuni yetu na "name calling" iwe strictly observed kumuheshimu marehemu kwa kutolitaja jina lake halisi, maadam humu kwetu alikuwa warumi , then he/she will always be warumi.
Mkuu Maxence Melo , if there is anything jf can do kuhusu huyu fallen hero, let's do something kuonyesha solidarity yetu.
RIP warumi !.
P
Mi nakufahamu ntaleta taarifa mkuuMimi nauliza tu kumbe humu watu wanajuana? Ilikuwaje ndugu wa warumi akampigia amu simu taarifa za kifo?
Kumbe humu watu wanajuana hadi ndugu kha.
Mimi humu najuana na watu wawili tu, na hatuwasiliani mara kwa mara kwa mwaka tunaweza wasiliana mara moja au tusiwasiliane kabisa.
Sasa najiliuliza ikitokea nikafa nani atajua? Kumbuka hata hawa wawili tunawasiliana kwa nadra sana.dah
Ila mimi mkiona sijaingia humu wiki mjue labda nimekufa maana sijawahi kukosa bando na nikibiwa simu siwezi maliza wiki sijanunua.
Ni hayo tu.
Rip cha umbea wetu warumi.