TANZIA Mwanachama mwenzetu Warumi afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili

TANZIA Mwanachama mwenzetu Warumi afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili

Status
Not open for further replies.
Apumzike kwa amani.
Mara ya mwisho niliona uzi wake uliokuwa unauliza "warumi ni nani "
 
Pole kwa familia yake na Wana Jf kwa ujumla binafsi warumi Ni mtu kuachana na Mambo ya ubuyu pia alikuwa mtu mwenye mawazo +ve.

Tumekutana Jf tumesaidiana mawazo Kama vile tunajuana kumbe hata sura zetu hatujuani lakini tuliaminiana tukasaidiana.

Hvyo rafiki warumi Kama kweli umeondoka Basi upumzike kwa amani na MUNGU akuweke sehemu salama huko utakapokwenda.
 
Mungu wangu Jamani 😭😭😭😭😭😭😭

Mungu ameruhusu uondoke na umri wako mdogo kabisaaa

Mungu awape faraja familia na wote walioguswa na msiba huu

Rest well💔 Rest well @warumi💔🕊🕊🕊😭🙏
 
Daah ahsante sana HOE kwa kutuwakilisha kwa binamu yetu. Ubarikiwe sana
Nimeiona thread hii jioni na I was really shocked na hii taarifa. Na mpaka sasa I am.

Nashukuru amu kwa updates na maelekezo yako maana nimeweza kufika mpaka msibani na ndio nimetoka mida hii.

Na nimetoa rambi rambi kama JamiiForums na nikawaeleza jinsi gani tuliishi nae hapa jukwaani. Dada yake amefarijika sana, na akasema tumemjua mtandaoni na tungeweza kuamua kukaa huko huko kimya tusijitokeze msibani lakini kwenda kwetu mpaka pale nyumbani inaonesha ni namna gani tuna upendo na tulikua tunamjali.

Kesho wanaaga saa 8 Muhimbili, nitakwenda pia kutoa salam za mwisho. Its too sad nimemuona sura yake when he is already gone.

Kuna muda ambao siko active JF Binamu alikua ananiandikia PM, kuniuliza naendeleaje niko salama ama nina matatizo yoyote and that meant a-lot to me.

Nimeumia kutoka rohoni.

Bado nawaza swala la rambi rambi tufanye vipi ku support familia katika wakati huu mgumu.

R.I.P Binamu
 
Kwa masikitiko makubwa ninapenda kuwapa taarifa ya mdau mwenzetu humu anayeitwa warumi amefariki usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapambana kwa ugonjwa wa figo.

Warumi alikuwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 29.

Taarifa hii nimepewa na dada yake mda huu, msiba unaelekea kwao Tegeta .

UPDATE:
Msiba upo Tegeta Nyuki, ukifika Stand unachukua boda au bajaj unawaambia wakupeleke nyumbani kwa Kiboko, maana msiba upo opposite na utaona geti jeusi liko wazi - ingia.

Msiba utasafirishwa kwenda Mbeya, Nonde Mabatini.

UPDATE.
Misa ya kumuaga itafanyika kesgo tarehe 27 August saa 8 mchana Muhimbili.
Duh..., japo mimi sio mwanachama active wa celebrity forum, ila jamaa namkubali sana na nimeguswa.

Zamani JF ilikuwa tukipoteza mwanachama, if management ilikuwa inafanya some sort of organisation, nakumbuka msiba wa Regia if tulitengeneza hadi Tshirts na tuka jiorganize hadi kuhudhuria mazishi kule Ifakara, tena kuna member alijitolea gari yake!
Hebu tazameni hapa chini

Hawa walituwakilisha vyema:
jf-team.jpg



_MG_0535.jpg

_MG_0528.jpg
Vijana wa Mtandao wa Jamii Forum wakiwa wamevalia rasmi waliposhiriki kuuaga mwaili wa aliyekuwa mwanachama wa mtandao huo, marehemu, Regia Mtema.

Naomba niishie hapa, nitaendelea kesho na tutakuwa Live kutoka Ifakara (pamoja na picha)

I don't know what happened now. Should we push for equal treatment during the demise of our members, tuweke system ya ndugu kuripoti kwa jf management kifo cha mwanachama wetu yoyote regardless umaarufu wake, kisha waweke number ya mchango, wana jf kuchangie, na siku ya kuaga jf management iwepo na kukabidhi mchango kwa wakiwa na mtu wa jf atoe neno.

Na kwenye mazishi ya wana jf wa eneo husika wahudhurie kutuwakilisha.

Kwenye mchango wa rambirambi hata tukiweka minimum TZS 1,000 tuu, kwa jinsi tulivyo wengi, hiyo fedha ina kuwa ina impact kubwa na ni faraja kwa familia kujua mpendwa wao alikuwa mwanachama wa mtandao wa jf na jf wanajali.

Na kwa vile wengi wa wana jf wanatumia pen names, ili kuheshimu the unanimity ya marehemu, humu jf tuu ndio atatajwa kwa jina lake la jf, mfano huyu warumi , lakini
pale msibani no one will mention his name, hata kwenye Salaam za jf, hatamkwi popote kwa jina, bali "marehemu alikuwa mwanachama wetu, alijinga jf lini, amechangia mada mbalimbali etc just that, na if members watakao hudhuria msiba, kwa vile kule wataliona na kulijua jina halisi, kanuni yetu na "name calling" iwe strictly observed kumuheshimu marehemu kwa kutolitaja jina lake halisi, maadam humu kwetu alikuwa warumi , then he/she will always be warumi.

Mkuu Maxence Melo , if there is anything jf can do kuhusu huyu fallen hero, let's do something kuonyesha solidarity yetu.
RIP warumi !.
P
 
Duh..., japo mimi sio mwanachama active wa celebrity forum, ila jamaa namkubali sana na nimeguswa.
I agree with you [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom