TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

Status
Not open for further replies.
Maisha ni mafupi sana,
Tujiheshimu,
Tuheshimu wenzetu na
Kumpenda Mungu

Inalillahi waina ilaihi rajiun

Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea.
 
Mungu amlaze mahali pema kijana wetu, sina jinsi ya kuelezea machungu niliyoyapata....
 
Mungu akupe pumziko la milele doto Mnzava.
 
Last edited by a moderator:
Hakika hatujui siku wala saa hata sekunde. Pumzika kwa Amani mdogo wetu. Umetangulia mapema.
Daima nitaikumbuka signature yako "Tulia kwa Yesu, Dhiki Kuu inakuja lakini kuna Tumaini"

Poleni wafiwa...Poleni Jamii Forums.
 
Ndugu zangu, bodaboda ni usafiri hatari sana japo unapendwa na watu wengi.

Majuzi nimenusulika kifo cha bodaboda kwa uzembe wa dereva. Madereva wa bodaboda wana mapungufu makubwa sana kupanda badaboda kwenye Highway au Main road ni hatari sana.
 
Poleni sana, wanaohusiana na marehemu,wawe na moyo wa uvumilivu.

Bodaboda wafuate sheria, ikibidi au ikiwezekana kuweke sheria umri wa kuanzia miaka 30, ndio aruhusiwe kufanya biashara ya pikipiki ya Bodaboda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom