TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

Status
Not open for further replies.

IMG_9145.JPG

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dotto Mzava likishushwa Kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili katika kanisa la Wasabato Manzese uzuri kwaajili ya sala ya kuombea kabla ya Mwili kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.


IMG_9166.JPG

Mchungaji wa kanisa la Adventist wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro


IMG_9175.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Maxence Mello akitoa historia fupi ya Marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.


IMG_9181.JPG

Baba Mkubwa wa marehemu Dotto Mzava akitoa maneno ya shukrani katika kanisa la Kisabato la Manzese Uzuri mara baada ya zoezi la misa kumalizika.


IMG_9201.JPG

Heshima za Mwisho zikiendelea kutolewa


IMG_9187.JPG

Majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu


IMG_9204.JPG

Mmiliki wa Fullshangwe Blog,John Bukuku akitoa heshima za mwisho


IMG_9209.JPG

Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla haujasafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwaajili ya mazishi


IMG_9212.JPG

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya Kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho


IMG_9216.JPG

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa Same Mkoani Kilimanjaro mapema leo


DSC_0334.JPG

Ibada ikiendelea


IMG_9235.JPG



IMG_9244.JPG



IMG_9254.JPG

Jeneza lenye mwili wa marehemu Dotto Mzava likipandishwa ndani ya gari tayari kwa safari ya kuelekea Same Mkoa wa Kilimanjaro leo kwaajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho


DSC_0300.JPG

Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kanisani


DSC_0306.JPG

Kwaya ya Angaza ikitoa huduma wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Dotto Mzava


DSC_0343.JPG
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto Mzava wakiwa kanisani kwenye ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Wasabato la Manzese Uzuri kabla ya Mwili kusafirishwa kwaajili ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko Kwao Same Mkoa wa Kilimanjaro
 
Pumzika kaka mi ndio najua leo. Maana tangu uchaguzi uishe kutokana na dhuluma aliyofanyiwa EL si ingii Jf wala kuona taarifa ya habari. R.I.P bro
 

Attachments

  • 1450518716597.jpg
    1450518716597.jpg
    93.3 KB · Views: 375
  • 1450518761256.jpg
    1450518761256.jpg
    78.3 KB · Views: 365
  • 1450518802688.jpg
    1450518802688.jpg
    90 KB · Views: 365
  • 1450518888401.jpg
    1450518888401.jpg
    129.3 KB · Views: 350
  • 1450518999034.jpg
    1450518999034.jpg
    111 KB · Views: 336
  • 1450519047458.jpg
    1450519047458.jpg
    98.5 KB · Views: 330
  • 1450519128099.jpg
    1450519128099.jpg
    95.9 KB · Views: 334
Last edited by a moderator:
Rafiki yetu amehitimisha safari yake
tijiulize sisi wakati Wetu utapofika tutakua upande Upi?
Jina LA bwana lihimidiwe..
 
sijui nisemeje kwa majonzi ya kuondokewa na rafiki bestito wa karibu kiasi hichi
yaani mpaka sasa naona kama ni ndoto sana, nashikwa na kigugumizi cha mikono
na kuona kama ni kitu kisichozoeleweka kweli Dotto Mnzava umetutoka hivihivi?

Ee Mungu nipe kusahau lakini ni ngumu sana kitu hichi, kusahaulika mapema hivi
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
 
Last edited by a moderator:
R.I.P Dotto.

Majonzi ya kuondokewa na mwenzetu aliyekuwa kiungo muhimu katika chombo tunachokipenda yana ni makubwa sana.
 
MHSRIP DOTTO na pole kwa wote walioguswa na msiba huu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom