Mwanachama wa CHADEMA Iringa Mjini, Leonce Marto anashikiliwa na Polisi na kunyimwa dhamana

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
Leonce Marto anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa maagizo ya RPC afande Bwire,hajachukuliwa maelezo,kitendo cha kushikiliwa kwa ndg Marto ni Mwendelezo mwa vitendo vya Ukandamizaji, uonevu ukiukaji wa haki za binadamu wanazofanyiwa wapizani.

Leonce.jpg
 
Amefanya nini huyo mnyalu?

Ndiye aliyeshinda uchaguzi lakini hakutangazwa. Hiyo aliyetangazwa na NEC ana ghubu na hapati ushirikiano kwa wananchi, hivyo anadhani huyo jamaa ndio anamuhujumu kwakuwa ndio mwenye ushawishi kwa watu. Hivyo anamuagiza RPC amkamate ili kumjengea hofu akimbie hapo Iringa. Ni sawa na ww umpore mtu mwanamke, kisha uone mwanamke hakupendi sana, uanze kumfanyizia mpenzi wake wa kweli, maana unahisi kwakuwa jamaa yuko bado hapo mtaani ndio maana hakupi penzi lote ww.
 
Ushauri;mnapotoa taarifa kama hizi kwa jamii ni vema kama ungekuw mnaweka sababu ya kukamatwa,na nini sababu ya kunyimwa dhamana kwa mtuhumiwa.
Aidha bila kufanya hivyo habari hizi zitaonekana kama za kishabiki jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa taifa.

#jr
 
Hahaha ccm wanaitisha mikutano ya wananchi, wananchi hawatokei wakati wameshinda wao, unadhani watafanya nini zaidi ya kuwakamata makamanda wote nchi nzima?!
 
Ndiye aliyeshinda uchaguzi lakini hakutangazwa. Hiyo aliyetangazwa na NEC ana ghubu na hapati ushirikiano kwa wananchi, hivyo anadhani huyo jamaa ndio anamuhujumu kwakuwa ndio mwenye ushawishi kwa watu. Hivyo anamuagiza RPC amkamate ili kumjengea hofu akimbie hapo Iringa. Ni sawa na ww umpore mtu mwanamke, kisha uone mwanamke hakupendi sana, uanze kumfanyizia mpenzi wake wa kweli, maana unahisi kwakuwa jamaa yuko bado hapo mtaani ndio maana hakupi penzi lote ww.
Tanzania ya leo inashangaza sana!🤔🤔🤔
 
Ushauri;mnapotoa taarifa kama hizi kwa jamii ni vema kama ungekuw mnaweka sababu ya kukamatwa,na nini sababu ya kunyimwa dhamana kwa mtuhumiwa.
Aidha bila kufanya hivyo habari hizi zitaonekana kama za kishabiki jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa taifa.

#jr

Huhitaji kutumia hakiri nyingi kujua kuwa ni habari za kishabiki.
Maana km alishinda nahakutangazwa lazima angeshakata rufaa kitambo.
Tatizo ndg zetu chadema bado mnaendereza siasa za kiuanaharakati zaidi! Maana uchaguzi ulishaisha kitambo, hatujasikia hyo myaru kupinga popote, leo unakuja na haki za binadam ndani ya uchaguzi! Hyo ni wapi na wapi??

Semeni kakamatwa kwa kosa gani! Na nilini.
 
Hilo la rufaa mtasubiri sana na Mahakama zenu mlizoandaa ili ionekane wapinzani wameshindwa hata mahakamani. Hakuna wa kuwaletea hela ya bure.
 
Aiseee Zanzimana huwa hatosheki na damu za watu ataenda kaburini huku anaendelea kuzinywa .
 
Leonce Marto anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa maagizo ya RPC afande Bwire,hajachukuliwa maelezo,kitendo cha kushikiliwa kwa ndg Marto ni Mwendelezo mwa vitendo vya Ukandamizaji,uonevu ukiukaji wa haki za binadamu wanazofanyiwa wapizani.
Mwache aje yeye mwenyewe kulalamika hapa, wewe una lalamika ukiwa ni nani kwake? Akae tu huko gerezani kwani tuna amini hayupo huko kwa kusingiziwa, atakuwa muharifu tu. Akitoka na kuona Tanzania haimfai basi amfuate Lissu Ubelgiji akapakatwe.
 
Leonce Marto anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa maagizo ya RPC afande Bwire,hajachukuliwa maelezo,kitendo cha kushikiliwa kwa ndg Marto ni Mwendelezo mwa vitendo vya Ukandamizaji,uonevu ukiukaji wa haki za binadamu wanazofanyiwa wapizani.
Haya ndiyo matokeo ya ushindi wa kishindo
 
Ndiye aliyeshinda uchaguzi lakini hakutangazwa. Hiyo aliyetangazwa na NEC ana ghubu na hapati ushirikiano kwa wananchi, hivyo anadhani huyo jamaa ndio anamuhujumu kwakuwa ndio mwenye ushawishi kwa watu. Hivyo anamuagiza RPC amkamate ili kumjengea hofu akimbie hapo Iringa. Ni sawa na ww umpore mtu mwanamke, kisha uone mwanamke hakupendi sana, uanze kumfanyizia mpenzi wake wa kweli, maana unahisi kwakuwa jamaa yuko bado hapo mtaani ndio maana hakupi penzi lote ww.
Alishinda ubunge?
 
Ushauri;mnapotoa taarifa kama hizi kwa jamii ni vema kama ungekuw mnaweka sababu ya kukamatwa,na nini sababu ya kunyimwa dhamana kwa mtuhumiwa.
Aidha bila kufanya hivyo habari hizi zitaonekana kama za kishabiki jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa taifa.

#jr
Chadema wote wanashikiliwa kwa tuhuma za uhujumu uchumi, inamaana hadi uambiwe?
 
Huhitaji kutumia hakiri nyingi kujua kuwa ni habari za kishabiki.
Maana km alishinda nahakutangazwa lazima angeshakata rufaa kitambo.
Tatizo ndg zetu chadema bado mnaendereza siasa za kiuanaharakati zaidi! Maana uchaguzi ulishaisha kitambo, hatujasikia hyo myaru kupinga popote, leo unakuja na haki za binadam ndani ya uchaguzi! Hyo ni wapi na wapi??

Semeni kakamatwa kwa kosa gani! Na nilini.

Usitake kujifanya hujui ni kwanini watu hawaendi mahakamani, taifa linapofikia viongozi wakatawala huku wakipuuza sheria, na mahakama kukubali kutumikia siasa chafu, matokeo yake ni wale wanaoonewa kupoteza imani na mahakama. Mnapenda sana kutumia hili neno uanaharakati, na sehemu kubwa ni kufuata upepo tu bila kujua maana yake. Hakuna asiyeona unyanyasaji wa wapinzani hasa cdm, huku mahakama ikiingizwa kwenye hujuma hizo za kimfumo. Leo hii mahakama ni sehemu ya kutekeleza uonevu kwa maagizo ya kiongozi mwenye ulevi wa madaraka. Nenda magereza, leo hii kuna watu wako ndani humo kwa maagizo ya watawala ili kukomolewa, na mahakama inafuata amri hizo.
 
Back
Top Bottom