Dini ni jambo linalo hitaji umakini katika kushughulika nalo bila kuleta migogoro mikubwa na chuki baina ya watu.
Hili ni tatizo linalo sumbua India sana kati ya Hindus na Muslims, Nigeria kati ya Christians na Muslims
Zungumzia kuhusu utaratibu ulioanzishwa na Xi unaolenga kusupress uhuru wa kuabudu.
Utaratibu wenu sio rafiki kwa haki za binadamu. Kama wanachama wa CCP hawatakiwi kuwa na dini kwanini msiishie hapo hapo mnalenga mpaka wasio wanachama.
Xi na selikari yake wamenzisha utaratibu ambao mi naweza kuuita "person worship " ambao unamtaka mfanyakazi ambae ni mwanachama na hata asie mwanachama kuyasoma mafundisho ya Xi? Kufanya group discussion ikimaanisha wawe wanakutana kila wiki kujadili mawazo binafsi ya Xi, na kuandika ripoti.
Hii ni inaonesha ni kwa jinsi gani CCP wanatumia mwamvuli huu ambao ni kama "cultural revolution " ili kulinda nafasi zao au unaweza kusema "Protective of their regime"
Kama umuhimu wa dini hauonekani kwenye chama ambacho kina watu milion 90 tu kwanini selikari yenu inayoongozwa na ichoicho chama inapushi ajenda hii mpaka kwa wachina wasiokuwa wanachama wa CCp? Wewe unaona hii ni sawa?
Unavyotoa maelezo yako unaeleza kama vile hili swala lipo ndani ya chama peke yake wakati huohuo unasahau kutuelezea ni kwanini mamia ya mamilioni ya waamini wa imani ya " FALUN GONG" ambao idadi yao ilikuwa na waamini wengi kuzidi chama cha CCP walikamata wakateswa wakauwawa na wengine kutolewa viungo vyako kwa lazima, je na wao ni walikuwa wanachama wa CCP? Hauoni kama hii ilifanywa ili kulinda chama na sio vinginevyo?
Haujazungumzia waisilamu wa Urygur ambao mmewaweka kwenye magereza na mnawafanyisha kazi ngumu ikiwemo pia kuwatesa, wanawake wanabakwa na pia Kuna ripoti ya kutolewa viungo vyako vya mwili kilazima "forced organ harvesting" , je na hao pia ni wanachama wa CCP?
Haujazungumzia kinachoendelea Tibet, Xi ameenda kuivuruga tibeti, watu wasiokuwa wanachama waliokuwa na uhuru wa kuabudu na wenye dini zao za karne na karne Xì na Selikari yake wameenda kuwavuruga na kuwakamata na the same kuwaweka kwenye makempu na Kuna ripoti imetoka inasema sasahivi magereza wameshaanza kukusanya DNA za watu walioko kwenye makempu wa Tibeti, ikiwa ni hatua za mwanzo zinazofanyagwa kelekea kutafuta match wa viungo vyao, je hao pia ni wanachama wa CCP?
Ukija hapa utueleze ukweli usije na propaganda zako za uongo! Ukweli ni kwamba China hakuna uhuru wa kuabudu dini yoyote isipokuwa kukiabudu chama na kumuabudu Xi, uwe mwanachama usiwe mwanachama utaratibu ndo huo!
Utaratibu wenu hauufai ulimwengu, kwasabau unavunja haki za binadamu na unamnyima binadamu haki na uhuru wa kuabudu.
Maendelo ya namna yoyote ni lazima yaheshimu haki za binadamu, maendeleo yanayokuja ambayo yanakuwa hayaheshimu haki za binadamu na uhuru wa kuabudu hayafai popote pale Duniani na ndio maana kumeongezeka wimbi kubwa la wakimbizi wa kichina kutokea China.
Mara nyingine uwe unatoa full details ikiwemo pros na cons zake sio kuisifia CCP tu hapa.