TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums & Mgombea Ubunge Lushoto(CHADEMA), Mohamedi Mtoi afariki ktk ajali

R.I.P Pigo kwa Chadema na makamanda wapenda mabadiliko wote. Mtoi hakuwahi,hajawahi na hakuwa msaliti. Na alipambana mpaka tone la mwisho la damu yake. Mods kama itawapendeza na kama utaonekana umuhimu uanzishwe uzi maalum kwa ajili ya ku pay tribute kwa Kamanda Mtoi. Tujikumbus hebposts zake muhimu. Pia utaratibu wa kufikisha rambirambi kwa familia yake kama mwana JF.
 
R.I.P....swali langu je ukawa itasimamisha mgombea mwingine au Jimbo limeshachukuliwa Na CCM kiulain.
 
MUNGU akubariki sana ndugu yangu wewe utakayeishi milele

Amin!Waambieni wachagga kafara zimetosha.Chacha Wangwe,Mtoi,Mwangosi.Wajinga ndio waliwao.Mwaka huu lazima Mbowe aongeze jumba jingine DUBAI.Ukweli mchungu....
 
Hapa uhai wa mwanadamu umetoweka.hakuna chenye thamani kama uhai.si uchadema au uccm.
 
R.I.P

Nasi tuliosalia kipindi hiking tukuenzi Kwa mengi Na hata kusambaza Na kukubali kuchagua mabadiliko.
 
Nimelia sana sana, tuliongea juzi. Kwanini afe yeye tu? Hapana aiseee. Nimelia sana tulikua pamoja, Mama yake ndio Mama yangu, familia yake ndio yangu, tukipokuwa shambalai tuliamua kuhamia wote kwenda Magamba school. Why?
 
Ndiyo Chagueni Mwingine Haraka Haraka Kwani Muda Unaenda Na Hata Hao NEC Kwa Sasa Wapo Busy Na Sidhani Kama Watakuwa Na Muda Wa Kuwasikiliza Labda Tu Mjipange Kwa Chaguzi Ijayo Ya Mwaka 2020 Na Hapo Pia Kama UKAWA Na CHADEMA Zitakuwepo Kwani Nimepata Taarifa Kuwa Baada Tu Ya Uchaguzi Mkuu Kama UKAWA Mtashindwa Basi Umoja Wenu Huo Wa KINAFIKI Utavunjika Rasmi. Ila Sisi CCM Kama Kawaida Ni Mbele Kwa Mbele.

yaani wewe nyau unatapika hadi msiba unashabekia? Huna ufunguo wa mbinguni? Hatujui saa wala dakika uwezi jua na wewe ujashindwa kushuhudia lowasa akiapishwa funga shimo lako
 
Rip Mtoi.poleni wana ukawa na wanajamii forum kwa kumpteza kamanda wetu mahiri
 
Mungu amrehemu Mtoi jamani, hili sasa ndio pigo kwa CDM/UKAWA, sio wanafiki na wasaliti wakirudisha kadi sijui... hili ni pigo, may his soul RIP. Familia yake ikapate faraja, amani na rehema za Mungu
 
Taarifa za hivi punde ni kuwa kamanda Mohamedi Mtoi amepata ajali na kufariki dunia

WAMETOKA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI TARAFA YA MLOLA.
KAMANDA MTOI AKAWAPELEKA WENZAKE MPAKA LUSHOTO MJINI KISHA AKAONDOKA KUELEKEA NYUMBANI KWAKE NDIO NJIANI GARI IKAPATA AJALI NA NDIPO KAMANDA MTOI AKAFARIKI DUNIA.

Maelezo haya yamethibitishwa na katibu wa chama wilaya Lushoto Kamanda Dulla.

========
UPDATES:

1442151153546.jpg
 
Back
Top Bottom