fidelity
Member
- Apr 22, 2012
- 91
- 11
Inasikitisha sana kwa msomi kuchukua maamuzi magumu kama haya.Tunasubiri polisi wafike eneo la tukio ili tupate taarifa za kina.
====== Updates =========
====== Updates =========
Ni kweli hii taarifa na shuhuda wamedai ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza,kitivo cha elimu.Taarifa za awali zinatanabaisha kwamba kijana huyo alibaki chumbani peke yake na aliagana vizuri na mwenziwe (wa kiume) aliyekuwa ameelekea lecture.Rafiki yake aliporudi ndipo alipokuta mwenzie amejitundika eneo alilokuwa anakaa ni jirani ya eneo wanapopaki pikipiki juu ya hostel ya Lema (ghorofa linaloendelea kujengwa).
Kwa maelezo mengine ni kama mita 150 magharibi-kaskazini mwa hostel ya Masha.
Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa chuo wameutwaa mwili wa marehemu na kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti huku uchunguzi juu ya chanzo kujitoa uhai ukiendelea.
Taarifa kamili itakatolewa na wahusika italetwa hapa jamvini