Mwanadamu, ujasiri wa kumnyang'anya godoro masikini unayemdai umeupata wapi?

Niliwahi kuona Rafiki amemtendea WEMA Jirani yake,

Jirani huyo alikopa pesa bank na kuweka nyumba pekee ya familia rehani,

Aliposhindwa kulipa, Bank walitangaza mnada, Rafiki wa Jirani aliyekopa alivyosikia hivyo, alimpigia kaka yake aliyekuwa na uwezo na kumwomba amsitiri Jirani yake na fedheha Kwa kununua nyumba Ili analizane na bank Kisha aje kumrudishia nyumba Jirani yake akimaliza kulipa Polepole.

Siku ya mnada ulipofika, jamaa akanunua nyumba kimya kimya bila mkopaji kujua,

Baada ya bank kulipwa pesa Yao,

Jamaa Akaenda Kwa Jirani yake na kumwambia sisi ndio tulionunua nyumba Yako, tunakupa muda ulipe pesa Ile tuliyowalipa bank, Kisha nyumba Yako tutakurudishia.

Jamaa alilipa Polepole mkopo Ule Kwa miaka zaidi ya kumi na kufanikiwa kurudisha nyumba yake.

Niliona ubinadamu wa mtu yule Kwa UKWELI.

Na huo ndio unaitwa urafiki wa Kweli.

Ni kumfaa mtu wakati wa DHIKI.

Sasa ikiwa wewe umewahi kumkopesha maskini na kumnyanyasa, ukadiriki hata kumnyanganya godoro pekee analotumia kujisitiri na mkewe na watoto, Rudi UPYA kujitafakari.

Ubarikiwe kama pia umewahi kumfaa ndugu, jamaa au hata mtu usiyemfahamu wakati wa DHIKI yake.

Aamen.
 
Mwingine amemkopesha maskini laki Moja,

Baada ya wiki mbili kupita anaenda kuchukua friji ya laki 6 na kuona amepata.

Mungu juu Huwa anaangalia, na mabaya lazima yaje kumpata mtu yule mbeleni.
Bro! Mm alikuja kwangu fundi bomba, ambaye wanafahamiana na mke wangu alimfahamu kupitia ufundi wake.

Nami nilipohamia alipo mke wangu nikamfahamu huyo fundi , siku moja alikuja nyumbani kwangu asubuhi asubuhi, nikawa namtania leo naona umevunja rekodi yako umewahi sana kufika kazini.

Akaniuliza kwani hujaona sms yangu nikamwambia sijaona, akaniambia anaomba nimkopeshe 100,000/= maana amepata majanga.

Alikuwa anaweka HEATER kule HALMASHAURI kwa bahati mbaya imeanguka na kuharibika, hivyo Mkurugenzi kamwambia leo hiiii hiii anahitaji HEATER mpya vinginevyo atamtia ndani.

Nikamwambia akutie ndani kwa lipi? Si utalipa tu, lkn anyway kwa kuwa umeingia woga mm nakukopesha hiyo fedha.

Nikaingia ndani na kumpatia, akaahidi baada ya siku mbili atanirejeshea nikamwambia sawa. Baada ya siku mbili akarudi na kuniomba msamaha !! Mm wala sikutaka kusikia sababu zake nikamkatisha na kumwambia HAMNA SHIDA ww endelea , akashukuru na kutamka daah ahsante sana maana nilikosa RAHA.

Tulikopeshana Mm na yeye bila mtu kujua, sasa kukawa na kazi ya bomba hapa nyumbani wife akaniambia mstue fundi aje nikampigia akaahidi atafika, lkn hakuja.

Nikampigia siku nyingine akaahidi lkn hakuja, wife akaniambia umeona sasa umemkopesha ndo maana hataki kuja anaona atafanya kazi bure.

Nilikaa kimyaa maana nilishangaa wife kajuaje? Jamaa akanitumia sms kuomba msamaha kuwa amebanwa na kazi zingine, mm nikamjibu sawa sasa nirudishie ile fedha yangu.

Akaahidi atanirudishia na akauliza juu ya ile kazi ilishafanyika? Mm nikamjibu kwa sasa sihitaji mambo ya yy kuja kufanya kazi nahitaji anirudishie fedha yangu.

Kumbuka hapo sasa imekuwa zaidi ya miezi 3, basi sasa ikawa ni sababu kwenda mbele ,matatizo juu ya matatizo , nikamwambia hata mm ninayo matatizo nikimwambia hawezi hata kuyabeba cha msingi anirudishie fedha yangu.

Hivi sasa simu yangu HAPOKEI, na mm asipopokea napiga muda wote, ikikata narudia ,narudia mpaka anaamua kukata, au anapokea na kudanganya kwa kusema NAKUJA .hapo najua yupo na watu hivyo anayeyusha.

Mpaka sasa nikaribu miezi 6 imepita, leo nimemuandikia sms na kumwambia hiyo ndo sms yangu ya mwisho kukumbushia deni langu.

Kajibu hata haieleweki kwa ahadi atanilipa tu fedha yangu.

Masikini ni nani? Yeyote anayekopeshwa? Au unapokopa unapaswa ulipe?

Unayedaiwa fika kwa mdai wako jadiliana naye lengo likiwa ni moja kulipa.
 
Pole sana ndugu yangu,

Wewe umetenda WEMA, lakini umelipwa mabaya,

Ni Bora kudhulumiwa kuliko kudhulumu,

Mungu atakulipa siku moja Kwa namna ambayo hutaamini, utatendewa WEMA na fadhila na usiyemfahamu kama malipo ya WEMA uliomtendea.

WEMA ni akiba na UOVU ni akiba.

Usichoke kutenda mema, maana utalipwa Kwa wakati wake usipozimia Roho.

Mungu akupe kuachilia na usonge mbele.

Ubarikiwe.
 
Mungu na awabarikie wote wasaidiao binadamu wenziwe, hiyo ndiyo IBADA na DINI ya KWELI.

HAKUNA CHA ULOKOLE WALA UKATOLIKI
BALI DINI YA KWELI NI KUSAIDIA WASIOJIWEZA
IBADA YA KWELI NI KUSAIDIA WASIO JIWEZA
DHEHEBU LA KWELI NI KUSAIDIA WASIO JIWEZA.
YAKOBO 1:27
 
Salaam,Shalom!!

(Mithali 19:17)
Akopeshaye maskini, humkopesha BWANA.

Mungu anachukia sana Umaskini, lakini anawapenda sana maskini,

Maskini wa Leo ni tajiri kesho, maana Mungu ndiye huwapandisha maskini na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwashusha wenye viburi.

Mungu amekuwa akikemea sana kuwaonea maskini, hapendi waonewe Wala kuvunjiwa Heshima Yao, kuwachokoza maskini na wajane na yatima ni kugusa mboni ya jicho la Mungu.

Hivi unawezaje kumnyang'anya godoro pekee analolalia maskini baada ya kukopa pesa ya kununulia chakula Kwa ajili ya familia yake,Ujasiri huo umeutoa wapi, watoto wa maskini watajisikiaje kuona baba Yao ananyanganywa godoro pekee la kulalia?

Ujasiri wa kwenda kumpora kanga au kitenge alichojifunika Jirani Yako Kwa sababu ameshindwa kukulipa deni lako unautoa wapi?

Maskini amekuja kwako anakuomba umkopeshe unga Ili akampikie mgeni wake aliyefika usiku huo, unampa Kwa masharti ya kukulipa siku mbili zijazo, Kwa Bahati mbaya, anashindwa kutimiza AHADI yake, ujasiri wa kwenda nyumbani kwake na kuchukua sufuria pekee analotumia kupikia chakula umeutoa wapi?

Mungu Toka juu, anakuangalia, anakudai pesa kiasi Gani Kwa kutolipa ZAKA, mbona hajawahi kukudhalilisha?

Tangu Leo, jifunze kubariki maskini,

Ukimkopesha maskini na akashindwa kulipa, mpe Muda atakulipa atakapopata, kamwe usimdhalilishe. Mungu atakufungulia mlango wa kupata pesa bila kudhalilisha binadamu mwenzio.

Mungu na awabarikie wote wasaidiao binadamu wenziwe, hiyo ndiyo IBADA na DINI ya KWELI.

Aamen
Mtu yoyote anayependa kudhalilisha wenzake ipo siku isiyokuwa na jina mungu atamdhalilisha na yeye, ni roho mbaya tu hakuna kingine
 
Niliwahi kuona Rafiki amemtendea WEMA Jirani yake,

Jirani huyo alikopa pesa bank na kuweka nyumba pekee ya familia rehani,

Aliposhindwa kulipa, Bank walitangaza mnada, Rafiki wa Jirani aliyekopa alivyosikia hivyo, alimpigia kaka yake aliyekuwa na uwezo na kumwomba amsitiri Jirani yake na fedheha Kwa kununua nyumba Ili analizane na bank Kisha aje kumrudisha nyumba Jirani yake akimaliza kulipa Polepole.

Siku ya mnada ulipofika, jamaa akanunua nyumba kimya kimya bila mkopaji kujua,

Baada ya bank kulipwa pesa Yao,

Jamaa Akaenda Kwa Jirani yake na kumwambia sisi ndio tulinunua nyumba Yako, tunakupa muda ulipe pesa Ile tuliyowalipa bank, Kisha nyumba Yako tutakurudishia.

Jamaa alilipa Polepole mkopo Ule Kwa miaka zaidi ya kumi na kufanikiwa kurudisha nyumba yake.

Niliona ubinadamu wa mtu yule Kwa UKWELI.

Na huo ndio unaitwa urafiki wa Kweli

Ni kumfaa mtu wakati wa DHIKI.

Ubarikiwe kama pia umewahi kumfaa ndugu, jamaa au hata mtu usiyemfahamu wakati wa DHIKI yake.

Aamen
Huyo jamaa ni zaidi ya binaadamu mungu aendelee kumbariki
 
Mtu yoyote anayependa kudhalilisha wenzake ipo siku isiyokuwa na jina mungu atamdhalilisha na yeye, ni roho mbaya tu hakuna kingine
Kweli kabisa,

WEMA ni akiba, na ubaya ni akiba.

Muhimu tutendeane mema,

Pia tumkumbuke kulipa ZAKA,hiyo ndio dawa ya Umaskini, mifumo kutoboka, chumaulete, HASARA nk nk.

Ubarikiwe🙏
 
Akikujia maskini kukukopa, ukiona anachotaka kukukopa hawezi rudisha, mpe Kasi ambacho unajua hata asiporudiaha hakitakufanya umuwazie mabaya.

Mungu atusaidie kuifanya na kuifaulu mitihani Mungu aliyotuletea maishani.
Hakuna tajiri mwenye roho iyo amini,masikini kwa Tajiri ni fursa
 
Thread Bora sana..umeandika mambo ya msingi sana..
Kuna kijana alikopa sh laki Moja akashindwa kulipa..wakaenda kuchukua vitu vyake..alipowaona wadeni wake akakimbia..wanaomdai wakapiga kelele za mwizi..chupuchupu auwawe yule kijana
 
Hao watendao hayo, wamekwisha ipata thawabu Yao,

Ni Rahisi sana ngamia kupita katika TUNDU la sindano, kuliko Mtu kama huyo kuingia Mbinguni.

Mungu atusaidie
 
Kuna binaadamu husikia raha kabisa kuongea kwamba"mimi sitaki utani na hela yangu kabisa"aina hii ya watu huwa ni toxic sana ikitokea umemkopa,si kwa sababu wanaiheshimu sana pesa,ila sababu wanaiabudu pesa.

Mambo aliyoyakataa Mungu ndio hayo,pesa hutafutwa,hupatikana,na hupotea pia,hizo ndizo kanuni zake.
 
Wengine husema ukitaka kuwa tajiri usimhurumie mtu.

Ni kana kwamba hawakuzaliwa uchi- na hawatarudi uchi- mavumbini.

Tujifunze kiutawala pesa, Si kutawaliwa na pesa.

Mungu atusaidie.
 
Thread Bora sana..umeandika mambo ya msingi sana..
Kuna kijana alikopa sh laki Moja akashindwa kulipa..wakaenda kuchukua vitu vyake..alipowaona wadeni wake akakimbia..wanaomdai wakapiga kelele za mwizi..chupuchupu auwawe yule kijana
Na ukiwauliza wakopeshaji kwanini mnafanya hivyo, watakwambia sisi tupo kwenye HAKI.

Mungu ndiye ahukumuye Kwa HAKI,

WANADAMU ni Rahisi kujihesabia HAKI ilhali tu wakosa.

Upendo husitiri wingi wa dhambi, wakopeshaji wangekuwa na Upendo, wasingetia mashakani maisha ya mkopaji kiasi kile.

Mungu ahukumuye Kwa HAKI, atusaidie.
 
Ndo maisha mkuu..niliwahi pata shida nka jipiga piga nikapata kiasi fulani ikabaki kama laki 2 kila mtu nnae muazima hana .na mshikaji wangu wa karibu sanaa nae akasema hana ika nibidi niuze simu kwa laki 4, While thamani yake ni laki 6.

kumbe yule mshikaji kusikia ivyo aka mtonya jamaa ake mwingine afu aka mpa laki 3 aje ainunue iyo simu kwa laki 3 akijua siwezi kataa na mimi bila kujua nka muuzia kwel ,zika pita kama week mbili namuona jamaa yuko na simu yangu afu ana cheka cheka uku ana jiongelesha kwamba kabadilishana simu na yule jamaa alie inunua kumbe ni movie nili chezewa.

(hii code alikuja kufunguka yule jamaa nilie muuzia )
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Naye Mungu atamlipa.

Tungekuwa WANADAMU tunachukuliana na kubebeana mizigo na shida, pasingekuwa na watu wanaokufa Kwa kukosa pesa kidogo ya matibabu hospitalini.

Tupunguze kuishi maisha ya anasa, tutenge kiasi Kwa ajili ya maskini na wahitaji wanaotuzunguka.

Amen
 
Mi naomba nitofautiane na wachangiaji wengine. Kusaidia wahitaji ni jambo jema, huleta baraka na kuna furaha katika kuchangia kupunguza ugumu wa maisha. Tatizo Afrika au niseme jamii zetu hizi msaada ni haki yao, watu wanadhani una wajibu wa kuwasaidia kwa sababu unacho kitu ambacho sio sahihi.
Mwisho ukikopa lipa. Mkiwa mnakopa mnakua na sura za upole,ukidaiwa unaona ka vile unagawa hela bure kumbe ni haki ya mtu.
Nadhani wanaokopesha waangalie ni nani wanampa pesa kwa sababu wakopaji wengi hawalipi (hasa ndugu). Kopesha ka mtu yuko mahututi asipopata hio hela atapoteza uhai au ataenda jela, kinyume na hapo atembelee taasisi za kifedha.
KATAA MADENI!
MSAADA SIO HAKI YAKO!
KAMA WE HUNA WENGINE PIA WANAWEZA KUWA HAWANA!!
TUNZA. LINDA. OKOA KIBUNDA!!
 
Back
Top Bottom