- Thread starter
- #41
U may be right,Mi naomba nitofautiane na wachangiaji wengine. Kusaidia wahitaji ni jambo jema, huleta baraka na kuna furaha katika kuchangia kupunguza ugumu wa maisha. Tatizo Afrika au niseme jamii zetu hizi msaada ni haki yao, watu wanadhani una wajibu wa kuwasaidia kwa sababu unacho kitu ambacho sio sahihi.
Mwisho ukikopa lipa. Mkiwa mnakopa mnakua na sura za upole,ukidaiwa unaona ka vile unagawa hela bure kumbe ni haki ya mtu.
Nadhani wanaokopesha waangalie ni nani wanampa pesa kwa sababu wakopaji wengi hawalipi (hasa ndugu). Kopesha ka mtu yuko mahututi asipopata hio hela atapoteza uhai au ataenda jela, kinyume na hapo atembelee taasisi za kifedha.
KATAA MADENI!
MSAADA SIO HAKI YAKO!
KAMA WE HUNA WENGINE PIA WANAWEZA KUWA HAWANA!!
TUNZA. LINDA. OKOA KIBUNDA!!
Nimewahi kushuhudia mtu mmoja tajiri alipokufa, usiku Ule Ule mwili ukiwa ndani ya nyumba,
Ndugu wa marehemu waliokuja na kuchukua ATM card ya marehemu na kuomba password ya Mke wa marehemu Ili kuhudumia Maziko,walipopewa,
Ndugu wale walikomba pesa zote na kutokomea,
Ukazuka mzozo wa ndugu na mwili hata kuzikwa Bado.
Nakushauri, saidia kilicho ndani ya uwezo wako, usikopeshe kama huna uvumilivu.
Mungu atubariki.