Mwanadamu, ujasiri wa kumnyang'anya godoro masikini unayemdai umeupata wapi?

U may be right,

Nimewahi kushuhudia mtu mmoja tajiri alipokufa, usiku Ule Ule mwili ukiwa ndani ya nyumba,

Ndugu wa marehemu waliokuja na kuchukua ATM card ya marehemu na kuomba password ya Mke wa marehemu Ili kuhudumia Maziko,walipopewa,

Ndugu wale walikomba pesa zote na kutokomea,

Ukazuka mzozo wa ndugu na mwili hata kuzikwa Bado.

Nakushauri, saidia kilicho ndani ya uwezo wako, usikopeshe kama huna uvumilivu.

Mungu atubariki.
 
Binadam ni kiumbe hatari kuliko kiumbe kingine chochote.
 
Mithali 22:7
Tajiri humtawala maskini,
Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.

Pia pitia kumbukumbu la torati linasemaje utaona hutakiwi kumuonea huruma kabisa uliyemkopesha😁

Kumbukumbu la Torati 28:13-15,44
[13]BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
[14]msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
[15]Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.

44)Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.
 
Mithali 19:17

Amhurumiaye maskini, humkopesha BWANA.

Pia usisahau, Mungu ndiye hutajirisha na kufukarisha vile vile,

Maskini Kwa dhambi na kutotii, hupewa shuluba na kutawaliwa na tajiri Ili ajifunze.

Tajiri vile vile, asidhani maskini atakuwa pale forever, ni kama tu gwaride, nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza.

Kuwa tajiri Leo, Si Kwa uwezo wako, ni neema Umepewa Kwa muda, ni umewekwa ktk jaribu.
 
Kumjua Mungu, ndicho chanzo Cha HEKIMA na Maarifa na ufahamu.
 
Amen [emoji120] mtumishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…