TANZIA Mwanafasihi maarufu Ngugi wa Thiong'o afariki Dunia baada ya kuugua muda mrefu

TANZIA Mwanafasihi maarufu Ngugi wa Thiong'o afariki Dunia baada ya kuugua muda mrefu

RIP legend.

Nakumbuka miaka 13 iliyopita nilipokuwa form 4 mwezi wa 9 tunaelekea kufanya mtihani wa necta tuingie mtaani mwalimu wetu wa literature ambaye pia alikuwa mwalimu wa darasa (darasa letu la art tulitenganishwa na wale wa science tangu form 3) alitukuta tunapiga kelele sana kama ilivyokuwa jadi yetu, tulipomwona tukatulia kimya kama vile hatukuwa sisi tuliogeuza darasa kuwa kama kilabu cha pombe.

Tulipokuwa kwenye kilele cha utulivu mwalimu yule alitutamkia kwa upole na kwa hisia "hey everyone here, ask yourself, this time tomorrow where shall I be?" Akageuka na kuondoka zake. Alikuwa mwalimu pekee aliyebaki akitupenda bila kutukatia tamaa, huku waalimu wengine wote wakituchukia na kwapenda wale wa mkondo wa science waliokuwa na nidhamu, wasomaji na wenye performers wazuri kadhaa.

Hata hivyo somo halikutuingia kwa wakati sahihi, kwani tuliendelea na utamaduni wetu hadi tukafanya mtihani na kuambuli div 0 zaidi ya 95% ya darasa. Sasa mtaa unashughulika na sisi, japo baadhi walijipata, hasa waliokuwa wa kishua.

Basi hiyo kauli ya mwalimu nakumbuka hadi nitakapoingia kaburini. Na inanipelekea kukikumbuka kitabu na mwandishi wake.
 

Mwandishi na msomi mashuhuri wa Kenya Ngũgĩ wa Thiong'o afariki akiwa na umri wa miaka 87

Taarifa za Msiba zimethibitishwa Wanjikũ wa Ngũgĩ, ambaye ni binti wa mwanafasihi huyo mahiri barani Afrika,

Taarifa hizo zinaelezea Kuwa alikuwa na matatizo ya afya ikiwa ni pamoja na matatizo ya figo na uhamaji mdogo.

Mwandishi huyo wa vitabu, atakumbukwa kwa kazi zake mbalimbali ambazo ziliwavutia wasomaji wengi Afrika Mashariki kama vile A Grain of Wheat, Weep Not, Child, Devil on the Cross, Wizard of the Cross na Petals of Blood.

Ni kazi gani zingine za kifasihi unazozikumbuka kutoka kwa nguli huyu?
Mzee hakutaka jina la kizungu: Kutoka JAMES NGUGI hadi NGUGI WA THIONG'O
 
Back
Top Bottom